Prof. Tibaijuka: Mliopora maeneo jisalimisheni; aanza kwa kasi!

Kinacholeta utata katika nchi hii ni kuwa na viongozi wanaoshikiria nyadhifa zinazowapa madaraka kadha wa kadha lakini wanashindwa kutumia madaraka hayo kwa kuingiliwa visivyo halali na wakubwa zao. Ninalolitegemea kwa Prof. nikwamba, hali hiyo ikitokea kwake, ni vema akaachie ngazi kuliko kujiruhusu kuwa ngazi ya kupandia.
 
Profesor Tibaijuka atamweza Mahanga?

Katika serikali ya Tanzania kumekuwa na mtindo wa kulindana kati ya viongozi, ndiyo maana hata wakati ajenda za mafisadi na ubadhilifu mwingine wa mali za umma ulipofumuka, viongozi waliopaswa kuchukua hatua walifyata mkia.

Sasa jana (kupitia ITV news ya saa mbili usiku) Professor Tibaijuka ambaye aliteuliwa kuwa waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi alisema "wale wote waliovamia maeneo ya wazi, wajisalimishe". Mahanga ambaye ni naibu waziri katika serikali ya kikwete ni mmoja wa wananchi wanaoongoza katika kuvamia maeneo mengi ya wazi. Sasa kwa wakazi wa Tabata, wanafahamu pale Bima, kushoto ipo Nyantare Social Hall na Nyantare Bar. Zikiwa zimekamata eneo lililokuwa la wazi na lina ukubwa unaokadiriwa kuwa kama meta kati ya 400 na 600! Hilo lilikuwa eneo la wazi, kwa sasa ni kitega uchumi cha mheshimiwa!

Pale Segerea, anajenga ghorofa katika eneo la wazi. Sasa Tibaijika ataweza kumkabili kiongozi mwenziwe na kumbomolea vitega uchumi vyake?

Yetu macho, tunasubili kuona nani atamvika paka kengere!!
 
Punda haendi bila ya kusukumwa pumbafu zao, wameona mwaka huu wameshindwa uchaguzi na wamechakachua sasa ndio wanajifanya kuwa wanafanyakazi ilituwaamini tena. Subirini 2015 mtakiona cha moto chenu hatuwataki ccm ondekeni kwenye nchi yetu mmeshanshindwa kazi wapisheni wanaume :redfaces: Mmeshafanya ufisadi sana na kuiba sasa ndio mnajifanya mnataka kufanyakzi toka 1964 mlikuwa wapi kujenga nchi.
 
Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka jana aliibuka na kuwataka watu wote waliopora ardhi ya serikali na viwanja vya wazi na na kujenga katika maeno ya fukwe wajisalimishe haraka wizarani kwake kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa kuwa ni vizuri viongozi kama yeye wakaongoza kwa kuonyesha mifano ni vyema Prof Anna Tibaijuka akarejesha ardhi ya serikali zaidi ya ekari 100 aliyochukua katika ranchi ya utafiti wa magonjwa ya mifugo iliyoko wilaya ya Kinondoni.

Prof Anna Tibaijuka alitumia ardhi hiyo kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana iitwayo Barbro Johansen. Na mara tu alipochaguliwa kuwa Waziri wa Mifugo Mhe John Magufuli aliwahi kutoa wito na kuwataka wote waliomilikishwa ardhi za ranchi za taifa kurejesha ardhi husika kwa maslahi ya sekta ya mifugo.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Prof Anna Tibaijuka akaingilia na kuchukua line ya maji iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya vijiji vilivyoko jirani na shule yake. Mpaka sasa wakazi wa vijiji hivyo ambao idadi yao inakua kwa kasi sana hawana huduma ya maji ya safi ya bomba.

Najua Prof Anna Tibaijuka anaweza kujitetea kuwa ardhi ilitolewa kwa ajili ya maslahi ya taifa. Lakini kama kweli ardhi hiyo ingekuwa ni kwa maskahi ya taifa na sio binafsi, ada zinazolipwa katika shule yake zingekuwa nafuu kuwawezesha watoto kutoka familia maskini waweze kumudu kuingia shuleni hapo. Raisi Jakaya Kiwete amewahi mara kadhaa kuzitaka shule binafsi kupunguza ada wananzotoza ili kuwawezesha watoto kutoka familia maskini kumudu kusoma katika shule hizo.

Aidha kama mradi huo ungelikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio binafsi, wakazi wa vijiji jirani na shule hiyo wangepatiwa huduma ya maji safi ya bomba kutoka shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilichukua line ya maji ya vijiji na hivyo kuwakosesha wanakijiji huduma hiyo.

Naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!
 
wapunguze ada nini? Private schools are expensive everywhere, serikali itoe elimi ya sekondari bure angalau umpaka f4. Kuliko ranch mbovu bora shule atakama ni private, anachangia sekta ya elimu. Na haujatoa maelezo kama hiyo ardhi ilichukuliwa kinyume na sheria au kwa kufwata taratibu za ubinafsishaji. Watu mnakuja tuu na hoja bila kuziweka ipaswavyo...
 
hakuna taratibu zozote zilizofuatwa wala kubinafsishwa. Ni afadhali waliojenga kwenye open space kwa kuwa ni halamsauri na wizara yake ndio iliwapatia offer na Tile deeds na building permits.
 
Shule inakuwa kwa maslahi ya taifa pale tu wanafunzi wanapolipa ada ndogo? Wakilipa sana basi hakuna tena maslahi ya taifa? Uelewa wako wa maslahi ya taifa uko chini sana!
Pili, hii thread yako ni kama ya kutaka kumkomoa au kumnyamazisha waziri Tibaijuka. Unataka asikemee uozo kwa vile naye - kwa mawazo yako - aliwahi kukosea. Kwa maneno mengine unataka akae kimya. Nadhani si sahihi mtazamo wako.
 
Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof Anna Tibaijuka jana aliibuka na kuwataka watu wote waliopora ardhi ya serikali na viwanja vya wazi na na kujenga katika maeno ya fukwe wajisalimishe haraka wizarani kwake kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Kwa kuwa ni vizuri viongozi kama yeye wakaongoza kwa kuonyesha mifano ni vyema Prof Anna Tibaijuka akarejesha ardhi ya serikali zaidi ya ekari 100 aliyochukua katika ranchi ya utafiti wa magonjwa ya mifugo iliyoko wilaya ya Kinondoni.

Prof Anna Tibaijuka alitumia ardhi hiyo kwa ajili ya kujenga shule ya sekondari ya wasichana iitwayo Barbro Johansen. Na mara tu alipochaguliwa kuwa Waziri wa Mifugo Mhe John Magufuli aliwahi kutoa wito na kuwataka wote waliomilikishwa ardhi za ranchi za taifa kurejesha ardhi husika kwa maslahi ya sekta ya mifugo.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Prof Anna Tibaijuka akaingilia na kuchukua line ya maji iliyokuwa imetengwa kwa ajili ya vijiji vilivyoko jirani na shule yake. Mpaka sasa wakazi wa vijiji hivyo ambao idadi yao inakua kwa kasi sana hawana huduma ya maji ya safi ya bomba.

Najua Prof Anna Tibaijuka anaweza kujitetea kuwa ardhi ilitolewa kwa ajili ya maslahi ya taifa. Lakini kama kweli ardhi hiyo ingekuwa ni kwa maskahi ya taifa na sio binafsi, ada zinazolipwa katika shule yake zingekuwa nafuu kuwawezesha watoto kutoka familia maskini waweze kumudu kuingia shuleni hapo. Raisi Jakaya Kiwete amewahi mara kadhaa kuzitaka shule binafsi kupunguza ada wananzotoza ili kuwawezesha watoto kutoka familia maskini kumudu kusoma katika shule hizo.

Aidha kama mradi huo ungelikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya taifa na sio binafsi, wakazi wa vijiji jirani na shule hiyo wangepatiwa huduma ya maji safi ya bomba kutoka shuleni hapo hasa ikizingatiwa kuwa shule hiyo ilichukua line ya maji ya vijiji na hivyo kuwakosesha wanakijiji huduma hiyo.

Naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!

Nchi hii huwa mnaniacha hoi, tuhuma za mtu huwa zinaonekana wakati anapotaka kufanya jambo jema au kugombea nafasi ya uongozi! All in all mpaka hapo tutakapoondokana na ubinafsi ndipo Tanzania itakapoondokana na maovu, si kwa sasa watu wenye nia njema huzushiwa tuhuma ambazo hazipo: ie kupora mke, uraia, nk!
 
nchi hii huwa mnaniacha hoi, tuhuma za mtu huwa zinaonekana wakati anapotaka kufanya jambo jema au kugombea nafasi ya uongozi! All in all mpaka hapo tutakapoondokana na ubinafsi ndipo tanzania itakapoondokana na maovu, si kwa sasa watu wenye nia njema huzushiwa tuhuma ambazo hazipo: Ie kupora mke, uraia, nk!

hawa mafisadi wanataka aache kufanya kazi yake vizuri! Mwacheni afanye kazi yake hayo mengine ulikuwa wapi kusema!? Huu ndo uzushi sasa. Kwahiyo ashindwe kufanya kazi kisa alijenga shule miaka ya nyuma!
 
Mimi nilishasema huyu mama longolongo nyingi, na kitu muhimu zaidi ya huyu mama ni power structure ya serikali ya Kikwete.

Sitegemei mabadiliko yoyote ya msingi mpaka power structure ibadilike.
 
mimi nilishasema huyu mama longolongo nyingi, na kitu muhimu zaidi ya huyu mama ni power structure ya serikali ya kikwete.

Sitegemei mabadiliko yoyote ya msingi mpaka power structure ibadilike.
unayosema kilanga ni kweli but tunaposubili power structure ibadilike kwa katiba kubadilishwa huyu mama afanye kazi yake! Asiiingiliwe na mafisadi!
 
shule inakuwa kwa maslahi ya taifa pale tu wanafunzi wanapolipa ada ndogo? Wakilipa sana basi hakuna tena maslahi ya taifa? Uelewa wako wa maslahi ya taifa uko chini sana!
Pili, hii thread yako ni kama ya kutaka kumkomoa au kumnyamazisha waziri tibaijuka. Unataka asikemee uozo kwa vile naye - kwa mawazo yako - aliwahi kukosea. Kwa maneno mengine unataka akae kimya. Nadhani si sahihi mtazamo wako.

kutokana na ukubwa wa kiwango cha ada wazazi wanachotakiwa kulipwa katika shule hiyo, hoja kuwa ardhi hiyo inatumika kwa maslahi ya taifa haina mashiko kabisa. Badala yake inachingia kukua kwa matabaka kati ya walionacho na wasio nacho.

Chimbuko la yeye kupata ardhi hiyo ni maombi ya vijiji jirani kuiomba serikali ardhi kutoka ranchi hiyo ili kujenga shule ya msingi na sekondari za serikali. Wakati huo mkuu wa wilaya ya kinondni akiwa ni rita mlaki badala ya kushugulikia maombi ya wananchi wa vijiji jirani akatumia maombi ya wananchi kumpatia ardhi hiyo. Zaidi ya miaka 10 watoto kutoka maombi ya wananchi kutolewa, watoto wa wao wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufuata shule ya msingi na sekondari-na wakati mwimngine kupata ajali za magari. Hapa maslahi ya taifa yako wapi.arudishe kwanza ardhi ya serikali ndipo awe na moral authority ya kusema hayo anayosema.

Hoja kuwa nataka kumnyamazisha haina msingi. Ninachosema ni kuwa prof anna tibaijuka hana morala authority ya kufanya ahayo anayodai kutaka kuyafanya kwa kuwa naye ni sehemu ya ufisadi huo.

Taarifa zilizopo ni kuwa shule hiyo ilitakiwa kuwalenga wasichana kutoka familia zenye vipato vya chini.
 
hawa mafisadi wanataka aache kufanya kazi yake vizuri! Mwacheni afanye kazi yake hayo mengine ulikuwa wapi kusema!? Huu ndo uzushi sasa. Kwahiyo ashindwe kufanya kazi kisa alijenga shule miaka ya nyuma!

viwanja vya wazi, fukwe nk zote ni mali ya serikali na ranchi ya taifa pia n i mali ya serikali. Kama ni kurudisha kila mtu arudishe alicho nacho. Si wengine kuonewa na wengine kubaki na mali na ardhi za serikali.
 
Ndiyo maana nchi hii itaendelea kubaki underdeveloped kwa miaka mingi ijayo!!!!! Huyu mama (prof) alikuwa mwalimu wa UDSM,kufuatiwa na Ukurugenzi UN (Habitat)-hajawaelewa wabongo!!!!!!!!Muulizeni je aliweza kubadilisha gheto za Harare alipokuwa UN?

Mwambieni kwa gia hiyo hafiki mbali kwa wabongo!!!!!!!!! Hivi anawaelewa wenye viwanja halisi hivi ?? anavyojaribu kutuhadaa ili tuamini kwamba Manzese is going to turn into O'Bay??????!!! Hizi ni siasa nyepesi za akina mkwere!!! We ngoja afumue tu-atakapoanza kufikia kwa wenyewe akina EL, AC, RA, JK, Salama, Lidhwani, Miraji, Ben&Anna Co Ltd, Yusufu, nk nk nk,atanyamaza fyata!!!!!, na ndiyo atakuwa ameishia hapo mpaka 2015!!!!!!!!!! Labda mkongwe aliyevuma enzi hizo mhe. Lyatonga atamwonea huruma amnong'oneze yaliyompata na kesi ya dhahabu wakati akiwa Naibu WM enzi zake, alipokuwa akienda kwa top gia akiondoa viti maofisini asubuhi!

WanaJF matatizo yetu ya msingi origin yake ni laana kutokana na viongozi waliotangulia (miaka ya 1967) wakifuatia wote wliotangulia na kuendelezwa na mkwere kuendelea kukabidhi nchi kwa mashetani badala ya Mungu; maendeleo huletwa na Mungu, siyo mashetani-shetani kazi yake ni kuharibu; kuchukua rasilimali zote za nchi kama madini (dhahabu, uranium, bati tanzanait, na mengine utaongezea), samaki wa bahari yetu kuu, wanyama wa mbuga zetu, magogo ya miti ya misitu yetu-kuwatajirisha wairan akina RA na akina Ahmadinejad : Pale alipo mkwere, akina sheikh yahya na lile jopo la washirikina wa Bagamoyo wapatao 100 ndiyo walinzi wake!!!!-ndiyo maana ana ulinzi wa majini (mashetani) ya sheikh yahaya.!!!

Nchi hii imelaaniwa
!!!-tutasubiri bila kuona maendeleo tangu utoto wetu wa wa miaka ya 1967 mpaka siku Mungu atakapotambuliwa na kupewa heshima na utukufu wake!!!!!!!! Kabla ya hapo tutaendelea kuishi kwa kutegemea bakuli za mkwere kila kukicha!!!!!!!!

:angry:
 
Tena kama itaweza kumfikia kwamba pale Art Gallery Mbezi Beach jirani na kanisa la Assembies of God jnmba mmoja tajiri amejenga katikait ya barabara; tena jirani na flats za NSSF njemba mwingine amejenga katikati na kuziba kabisa barabara yote!!!!!! Akituondolea hawa manjemba!!!!!!!!!!!! watu wa Mbezi Beach pamoja na wanaJF tutamtumia pongezi!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ngoja tusubiri tuone kama Prof Tibaijuka 'will walk the walk'.
Nakumbuka Magufuli aliwahi 'kumlipua' naibu waziri wake Rita Mlaki (akiwa ardhi).
Prof afanye kweli vinginevyo ataanza kuumbuka mapemaaaaaa.......
 
Back
Top Bottom