Kombo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,812
- 509
My Take:
Kwa kosa alilolifanya kupeleka ombi Un Pasi na kupata baraka za baraza la wawakilishi Znz wakti anajua fika suala la ardhi sio suala la muungano ni utovu mkubwa sana wa nidhamu na kutaka kufanya ubabe na kuvunja katiba ya Muungano na ile ya Zanzibar. Kiungwana anatakiwa ajiuzuru.[/FONT][/COLOR]
Prof. Tibajuka wala hahusiki na jambo hilo kiasi cha kulazimishwa kujiuzulu. Wazanzibari wamwulize Amani Karume na Dk. Shein kuhusu jambo hilo kwani kwa nafasi zao za uongozi kule Zanzibar walihusishwa kikamilifu kwenye mchakato wote.
Kiutaratibu jambo hilo lilifikishwa kwenye Baraza la Mawaziri kwa nyakati tofauti (Karume na Shein (pamoja na Nahodha na Bilal) wakiwa sehemu ya Baraza hilo) na kujadiliwa kwa kina kabla ya kuridhiwa na kupelekwa UN. Kama kulikuwa na ulazima wa suala hilo kujadiliwa na BLW (kwa maoni yangu hakukuwepo ulazima wowote), Rais wa Zanzibar wa kipindi husika alipaswa kuelekeza hivyo.
Tuache kukariri!.