Prof Tibaijuka lazima ajiuzulu

Kumbuka kuwa hata Tanganyika haiwezi kufikisha jambo lolote Un kwa sababu haitambuliki kisharia. Na unaposema Tanzania maana yake ni Tanganyika na Zanzibar.

Tunachohoji vipi Tibaijuka waziri wa Ardhi wa Tanganyika apeleke maombi UN kwa niaba ya Tanzania pasi na kuhusisha Znz huusan watunga sharia wa nchi hizo mbili huru zilizoungana kimkataba?

CUF na BLW wameliona hilo japo Chadema wanalipinga kiaina. Kwani hilo sio tatizo kwenu kwani nia yenu ni kuidhulumu Znz na kukuza tanganyika. Znz wameliona hilo na mpaka kieleweke.

lazima mjue Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kamili kwa mujibu wa sharia za Znz. Na Muungano wanalijua hilo.



CHADEMA tena? eeh? Sikujua kama ule ujumbe uliokwenda UN ulikuwa ni chadema. Kwanini huitaji CCM hapa wakati ndiyo ma architect wa mpango mzima?
 
Taaanzania Tanzaniaaaa, nakupenda kwa moyo woooooteeeee. Nchi yangu Tanzaniaaa jina lako ni tamu sanaaa....
Mh! Huu wimbo bado upo kweli?

Huyo Jussa hata haelewi anadai nini. Yupo tu anapiga makelele mengi lakini anachokidai wala hakielewi! Walio karibu nae ni wema wakamfahamisha kuwa eneo hilo linapoongezwa Zanzibar nayo itafaidika! Uchoyo wa mafuta na gas unampofusha mpaka anajinyima mwenyewe fursa ya kupata eneo zaidi la kutafuta hayo mafuta na gas.

Jussa kumbuka kuwa eneo la Zanzibar iko ndani ya JMT!
 
Taaanzania Tanzaniaaaa, nakupenda kwa moyo woooooteeeee. Nchi yangu Tanzaniaaa jina lako ni tamu sanaaa....
Mh! Huu wimbo bado upo kweli?

Huyo Jussa hata haelewi anadai nini. Yupo tu anapiga makelele mengi lakini anachokidai wala hakielewi! Walio karibu nae ni wema wakamfahamisha kuwa eneo hilo linapoongezwa Zanzibar nayo itafaidika! Uchoyo wa mafuta na gas unampofusha mpaka anajinyima mwenyewe fursa ya kupata eneo zaidi la kutafuta hayo mafuta na gas.

Jussa kumbuka kuwa eneo la Zanzibar iko ndani ya JMT!

Hapo ndipo tunaposhangaa hizi kelele ni za ninii.
 
Mamlaka ya JMT ni kamili. Eneo la jamhuri ya Muungano ni eneo zima la bara na visiwani. Hakuna eneo lolote la 'nchi ya Zanzibar' ambalo si eneo la JMT. Kama lipo niambie. Katiba ya ZNZ inaweza kusema lolote lakini ikipingana na ile ya Muungano vipengele vyake ni batili. Zanzibar ni nchi kwa Wazanzibari tu; siyo nchi inayotambulika mahal popote duniani. Kuwa na jeshi, mahakama, na rais (mihimili mitatu ya dola) hakuifanyi ZNZ kuwa nchi vinginevyo miye ningetamba niko "nchi" ya Michigan! Kuongeza eneo la bahari kutakuwa na manufaa kwa Zanzibar na kwa Tanzania nzima. Wananchi wa ZNZ yawapasa wafurahi na kuunga mkono uamuzi huu wa serikali ya JMT.


Nakubaliana na wewe kabisa kwa muono wako,nadhani unaungana na kina Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete pamoja na walowahi kuwa magavana wa benki kuu akiwemo Mtei na vile vile kina Sitta,Tundu lisu na wenzake ktk harakati zenu za kuizika znz kabisa ktk ramani ya dunia,na naamini mna agenda za siri sana ktk mpango wenu huu

Naweza tu kusema hata kama kuna ukweli wowote ambao utafahamishwa na hata kama unaujua basi kwa kua unasimamia agenda yenu hutoweza kuukubali,na mimi siwezi kupoteza muda ati kukufahamisha wewe ktk masuala kama haya kwa kua naelewa nini lengo lenu

Nb: Nukuu ya maneno ya mzee wetu Nassor Hassan Moyo alomwambia Sitta na ujumbe wake ulokuja znz. Mwanzo wa Nukuu: Wa znz wa leo sio wa zamani,wa znz wa leo wamesoma na wanajua nini wanachokifanya na hawako tayari kuporwa nchi yao na watafanya kila njia kuhakikisha znz inarudi ktk ramani ya dunia,waachieni wenyewe na nchi yao,tumechoka na nyinyi ktk kuikandamiza znz,mumewaona hawa vijana walokuwepo hapa wote wana uchungu na nchi yao na wanaguswa ktk mioyo yao na wapo tayari kufa wote lkn znz ibaki ktk ramani ya dunia. Mwisho wa Nukuu.


My take: Wa znz tupo ktk mkao wa kula tunasubiri chakula kipakuliwe tu,tukile... SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA IDUMU HATA KAMA WATU WANAUMIA..
 
Waziri Moh'd Abood hakuwepo kwa mujibu wa picha aliyokuwepo kwene blog ya Issa Michuzi. Yule mweupe uliyemuona ni mbunge wa Mafia naye aliwakilisha Bunge la Muungano. Suala mbona hakukuwa na mwakilishi toka Baraza la wawakilishi?

Kumbuka kuwa katika Rules of Law kuna mihimili mikuu mitatu katika nchi nayo ni Bunge, Makahakama na Serikali. Tanzania iliwakilishwa na Mihimili ya Bunge na Serikali na Znz iliwakilishwa na Serikali na BLW halikuwakilishwa na kutojulishwa kuhusu suala hili.

Na at the end of the day BLW watahisishwa katika kubadili kipengele cha Katiba hususan kila cha eneo la miliki.

Ndio maana wawakilishi wmeuliza hilo kwanini wao hawakujulishwa kuhusu ombi hilo wakti linagusa muungano. Na suala la ardhi ni jambo ambalo haliko katika mambo ya muungano?

Kuna siri hapo ambayo Tibaijuka ameificha nayo lazima ijulikane na kubainishwa.

Tusubiri tu majibu ya Serikali.


usiwe kilaza wewe!!!!!!!!!! Hivi mnataka hiyo bahari ambayo haina mwenyewe ichukuliwe na ndugu zenu waarabu? Unataka kutupotosha tujue kwamba Bunge la Jamhuri ni la Wabunge wa iliyokuwa Tanganyika peke yake?? Hampati kitu!!!!

Msipoangalia tutaanza kuwachunguza uraia wenu!!!!!!
 
Kumbuka kuwa hata Tanganyika haiwezi kufikisha jambo lolote Un kwa sababu haitambuliki kisharia. Na unaposema Tanzania maana yake ni Tanganyika na Zanzibar.

Tunachohoji vipi Tibaijuka waziri wa Ardhi wa Tanganyika apeleke maombi UN kwa niaba ya Tanzania pasi na kuhusisha Znz huusan watunga sharia wa nchi hizo mbili huru zilizoungana kimkataba?

CUF na BLW wameliona hilo japo Chadema wanalipinga kiaina. Kwani hilo sio tatizo kwenu kwani nia yenu ni kuidhulumu Znz na kukuza tanganyika. Znz wameliona hilo na mpaka kieleweke.

lazima mjue Zanzibar ni nchi kamili yenye mamlaka kamili kwa mujibu wa sharia za Znz. Na Muungano wanalijua hilo.

Hapo kwenye RED ndiyo umezidi kuanika masaburi yako nje, kama mbuni. Inaelekea wewe ni mnafiki na una husuda na CDM. Mtamtambuaje Lissu, ingawa mlijadai kumpinga (CCM + CUF).

Hivi waliopeleka hilo ombi UN ni CDM? Acha masaburi bana!

Ukweli ulio dhahiri shahiri ni kwambi ombi la JMT kuongezea EEZ limepelekwa UN na Serikali ya CCM na Mshirika wake CUF kwa upande wa ZNZ. Usijidai umevuta bangi wakati umekula haluwa!
 
Nimeshindwa Kuelewa wa Znz wanataka nini hasa?
1. Je hawataki mama tibahijuka kupeleka maombi ambayo nao Kama part ya JMT watafaidika??Au hawakubali Kama wao ni sehemu ya Tanzania ?
2. Je hawakubali lolote linaloamuliwa na Tanzania wao wakiwa part ya muungano ? Nadhani wanatakiwa Kuwa wazi kwamba hawahutaki muungano basi?


Kwa Kweli nashindwa Kuelewa nini hasa Tatizo Lao? Naomba kusaidiwa...
 
Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.

Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.

Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.

Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.

Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.

Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.

sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.

Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.

Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.

Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.

Daktari,
Wacha uongo. Kuna katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Niambie tena kwamba Zanzibar na Tanganyika ziliungana kimkataba na siyo kikatiba. Uongo si sera nzuri.
 
Nimeshindwa Kuelewa wa Znz wanataka nini hasa?
1. Je hawataki mama tibahijuka kupeleka maombi ambayo nao Kama part ya JMT watafaidika??Au hawakubali Kama wao ni sehemu ya Tanzania ?
2. Je hawakubali lolote linaloamuliwa na Tanzania wao wakiwa part ya muungano ? Nadhani wanatakiwa Kuwa wazi kwamba hawahutaki muungano basi?


Kwa Kweli nashindwa Kuelewa nini hasa Tatizo Lao? Naomba kusaidiwa...
Haya maswali labda tuwapelekee kwenye ile forum yao ya kifitini(mzalendo.net) labda kutakuwa na majibu.
 
Mimi sielewi msingi wa malalamiko ya CUF kwani eneo linaloombwa kuongezwa kwa sasa liko ndani ya mipaka ya Zanzibar au ni eneo huru kwa mujibu wa sheria za kimataifa? Pili, kule UN kuna Taifa linaloitwa Zanzibar na tatu hili ombi likikubaliwa si Zanzibar watakuwa na eneo pana la kufanya uvuvi?
 
Hakika Jusa wewe ni shujaa sana kwa kuliona hili kwani kuna dhulma kubwa sana ilitaka kufanyika hapa. Ikiwemo ile ya kumega eneo la bahari kwa Znz na kuitumbukiza katika Muungano.

Lazima kieleweke na Prof lazima aondolewe hapo. Kwani ubabe hauna nafasi kwenye sheria. lazima sheria zifuatwe.
Wenzetu kazi ya kupiga domo hamjambo.
Hata mkisaidiwa kufikiri mnalalamika utafikiri dunia inaisha kesho!
Hata Nyerere aliwahi kusema angekuwa na uwezo angevivuta visiwa hivi mbali kabisa na Tanganyika.
Kwamba tumeshawachoka na maneno maneno ni dhahir , taadhali jitangazieni uhuru tujue moja.
 
kama unalijua Je unajuwa mamlaka na madaraka yao ikiwemo pamoja na mipaka ya madaraka na mamlaka yao? Tueleze basi sio tu kusema unajua kumbe wahitahi darsa.

Asiyetambua mamlaka ya Rais wa Muungano ni Padre Slaa alikataa matokeo na kumkwepa Kikwete mpaka juzi alipokimbilia chai pale ikulu kwa aibu kubwa na fedheha.

Lakin pia elewa mimi nasimamia Katiba ya Muungano wenu ambao Padre anaukana na Katiba ile ya Znz na ndipo hoja zangu zinaposimama.

Wewe tunajuwa unaabudu wazungu na sababu zinajulikana sio siri. Kumbuka kwetu wazungu tunawadharau na kuwatuma kama vibarua tu japo kwako ni mabwana.




Umeshatuambia kuwa muungano huu hauna katiba sasa unasimamiaje katiba ambayo haipo? Kajipange tena, muongo wewe!
 
Umeshatuambia kuwa muungano huu hauna katiba sasa unasimamiaje katiba ambayo haipo? Kajipange tena, muongo wewe!
Ph.D holder huyo. Sasa ukutane na mvuvi ndiyo utatoa machozi. Hivi hao akina Jussa kwanini wasipeleke kwenye baraza la wawakilishi hoja ya kuuvunja muungano badala ya kubaki kuchokonyoachokonyoa tu na kukuza vitu ili Zanzibar ionekane inaonewa kwenye huu muungano?
 
CHADEMA tena? eeh? Sikujua kama ule ujumbe uliokwenda UN ulikuwa ni chadema. Kwanini huitaji CCM hapa wakati ndiyo ma architect wa mpango mzima?
Huyo jamaa ni mnafiki kiasi kuwa hata shaitwani mwenyewe anaweza asimfikie kwa unafiki! Hapa ataitaja Chadema, atamtaja Slaa lkn hutaona anaitaja ccm wala kikwete!! Mtawatambua kwa matendo yao!! Na huyo huko kwao ni 'msomi' anaongelea madudu (kama kweli yapo) ya serikali ya ccm, lkn anailaumu Chadema!!! Jiulize utegemee nini kutoka kwa wavuvi wao masikini wasio na elimu waliozoea kukaririshwa tu mambo na 'wasomi' wao!!! Balaa duniani...
 
Itakuuma sana.

Lakin tunashangaa Je imekuwa nongwa kwa BLW kupitia Jusa kuhoji kuhusu mchakato mzima wa kupeleka hayo maombi?

Ebo kuna siri gani behind maombi hayo?

Lazima kieleweke hapo. Jusa kaza buti na komaeni hapo mpaka kieleweke.




Eboo! yaani kwa kuwa huyu jussa hajui wala hakushirikishwa, ndo uite usiri, wanaostahili kujua wanajua kutokana na hadhi yao na sio lazima hadi huyo MJUSI ajue, hana umuhimu wowote kwa taifa letu, he is just an alien like you barubaru bin waruwaru!
 
Na vile vile Tibaijuka alitakiwa aende na faili la Tanganyika sio Tanzania. Kwani Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Je unalijua hilo?

Kwani madaraka ya Tibaijuka mwisho msasani wala hayafiki Znz. Kwa kuwa amejivika kilemba cha Tanzania ndipo tunapomuhoji alipewa na nani madaraka ya kuiwakilisha kwenye jambo lisilo la muungano? Je aliowawakilisha wanalijua hilo?

Kwa vyovyote lazima kiungwana ajiuzuru.


Angeenda kama waziri wa Ardhi wa Tanzania hangepokelewa UN na makaburasha yake yangeishia jalala la UN.Kule aliwakilisha serikali ya muungano INAYOTAMBULIWA UN ndio maana alipokelewa.Alienda kama mwakilishi wa serikali ya Tanzania sio waziri wa ardhi.Hana haja ya kujiuzulu sababu hakwenda kama waziri wa ardhi .
 
Back
Top Bottom