1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.
Je zanzibar au tz bara inaweza kuomba kuomba kuongezewa eneo pasipo kutumia jina la JMT? Rais wa zanzibar ni mtawala ndani ya JMT, Bunge la JMT lina wakilishi kutoka sehem zote za JMT na Zanz ikiwemo
Naomba upitie kwanza na kujua madaraka ya Serikali ya Muungano kwa mujibu wa sharia za JMTz. na madaraka ya SMZ kwa mujibu wa katiba ya muungano. Kisha leta hoja zako kabla kuanza kutoa shutuma na matusi.
kwani mikoa mingine ilishilikishwa ktk hili?Naomba nikuweke sawa kidogo kwani kuna mambo umeyasahau kidogo.
Tanganyika na Znz zimeungana kimkataba na sio kikatiba. Kuna mambo yamo katika mkataba huo nayo ndio mambo ya muungano. Suala la ardhi na makazi si suala la Muungano na ndio maana Znz kuna waziri wa wizara hiyo na Bara yupo.
Kumbuka kuwa Mamlaka ya Tibaijuka mwisho wake ni Chumbe akiwa Znz hana mamlaka yoyote ukilinganisha na waziri wa mambo ya nje au mambo ya ndani. hawa wana malka kote kote.
Kumbuka vile vile Znz ni nchi kamili yenye mamlaka kamili na hilo limebainishwa katika katiba ya Znz. Kwa msingi huo Katiba hiyo hiyo imeanisha eneo la Znz kiufasaha kabisa. sasa kwa ombi hilo la Tibaijuka ni lazima katiba ya Znz itabidi ibadilike kwa kuongeza eneo la milki yake au kupunguza miliki yake na hapo ili kubadilisha kipengele hicho cha katiba lazima BLW litahusika vilivyo kwani wao ndio wtunzi wa sheria za Znz na mambo yote yaliyo nje ya muungano.
Kumbuka kuwa katika Picha walopiga kule UN wakti wanawakilisha alikuweo Tibaijuka, balozi wa Tz katika UN, Mbunge wa Mafia na Katibu wa wizara kutoka Znz. Kwa mantiki hiyo inaonekana wazi Prof Tibaijuka alipata baraka zote za Bunge la Muungano dio maana akachukua muwakilishi wa Bunge.
Sasa upande wa BLW hawakuwa na taarifa zozote ongezeka hilo officially na aliku husishwa kwa lolote lile kitu ambacho Jussa amehoji. Ikumbukwe kuwa maombi haya yakifanikiwa lazima BLW litahusishwa katika kupitisha sheria za ongezeko la eneo la miliki la Znz.
sasa labda tujiulize.
Je Znz itaongezewa kiasi gani katika hicho kilicho ombwa? hilo ni suala ambalo limegubikwa na utata mkubwa na alijabainishwa katika mkataba au mbi hilo.
Lakini pia lazima ufahamu kuwa Tz na Znz zote zinaongozwa na Rules of Law. Na mihimili yote mikuu inajipambanua yaani Serikali, Bunge na Mahakama bila kuingilia katika utendaji kazi wake. Kila muhimili unajitegemea.
Limeanza baraza la wawakilishi kuhoji Serikali ya Znz kisha uzi utafuata. Kwani majibu ya Serikali ndio yatatoa mwangaza kwa sakata hilo. Lakin all in all Tibaijuka lazima ajiuzuru hapo.
Kwani mtiririko wa jambo hili unakuwa sawa kabisa na ule wa Tz kujiunga na OIC.
Sharia tena? Labda Zanzibar ndio inatumia hiyo sharia lakini huku bara tunatumia sheriaNdio maana nikakuuliza je unajuwa mamlaka ya Rais wa Znz kwa mujibu wa katiba ya Muungano? Na kwa kukuongezea zaidi tafuta ujuwe mamlaka ya Bunge la Muungano kwa mujibu wa sharia na Mamlaka ya Baraza la wawakilishi kwa mujibu wa sharia?
Acha upofu wa kutosoma katiba yako vizuri.
Nitakujibu kwa kifupi na kwa kutumia mifano halisi labda utazinduka.
waziri wa Ardhi na makazi muungano ni Prof Anna Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi na makazi Znz ni Mh Ali Juma Shamuhuna.
Waziri wa Afya na Ust wa Jamii Muungano ni Dr Haji Mponda
Waziri wa Afya Znz ni Mh Juma Duni.
Je unalijua hilo? Na unajua mamlaka yao wote hapo juu.
tafakati kabla kukurupuka na kuleta hoja.
watakucheka wenzakoo wewe.
barubaru is just a coward,.rats always dump a sinking ship,mapambano ya ukombozi zanzibar yalipokuwa makali,waruwaru akakimbilia kwao uarabuni,now he talks like a true patriot...shut the hell up waachie wazalendo wanaomenyeka kule pemba na unguja waamue kuhusu the so called nchi yao sio raia wa nchi ya kigeni kama wewe..
Nadhani wewe unachotaka kuelezea ama kushawishi hapa ni upupu mtupu.Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika sasa waziri wa Tanzania anapokuwa hana mamlaka Zanzibar kwa sababu Zanzibar ni nchi,hoja yako inakosa mwelekeo.
Huwa najiuliza hivi watu kama ninyi na hao kina Jusa mnasiri gani dhidi ya wananchi! .Mtazamo wangu wananchi wanahitaji huduma bora za jamii na usalama wa maisha yao .Ila wote mnaoleta hizi chokochoko ni waroho wa madaraka, badala ya kuishauri na kuikosoa serikali kuweka uwiano wa matumizi ya rasilimali kwa manufaa ya wananchi,ninyi mpo majukwaani mkidai Zanzibar ni nchi.Mnachokitaka hakitakaa mkipate kwa sababu wengi wenu hamjui mnachohitaji.
Halafu ningewashauri wewe na hao wapiga debe wenzako kina Jusa kipindi hichi cha kubadili katiba ndio muafaka kuweza kuweka mambo sawa kwa yale yote mnayoona ni kikwazo.Ila kutokana na kuwa mna ajenda zenu za siri mnatanguliza matakwa yenu binafsi badala ya matakwa ya wananchi.
Hiyo ardhi /bahari inayoongezwa ni ya Tanganyika ama Tanzania! kwanza hiyo Tanganyika haipo sasa sijui kinachowapandisha majukwaani na kupaza sauti kama vile nyie sio watanzania.Wapemba wanaofanya biashara Kariakoo na kusaidia ndugu zao walioko Zanzibar isingekuwa huu muungano unafikiri mambo yangekuwaje! .Nadhani ni vyema kuleta hoja zenye/zilizofanyiwa utafiti na sio kutoa hoja kutokana na hulka za mrengo wa kivyama.
Kuna watu hapa wanaona karibu sana. Mhanga mkubwa wa kuvunjika kwa muungano sio Tanzania bara. Time will tell mtakavyoanza kuona makali ya kuja kujibanza na kuchuma Tanganyika halafu mnaenda kula Zenj. Huyo Jussa mwenyewe si ajabu ana majumba Tanganyika...awahi kuuvunja ili turithi bila kutolea jasho
Acha uvivu wa kufikiri wewe. Hilo unalosema ninalijua zaidi na wewe na Jusa mnalijua ila kutokana na ulemavu wa mawazo mliojipachika mnapindisha ukweli.
Kwanza unazungumzia muungano upi wakati mnajidai hamuwatambui viongozi wa muungano na maamuzi yao! ,kwamba Zanzibar iwe juu ya muungano.Nadhani unapaswa kupangilia upya hoja zako.Hakuna cha maana unachosisitizia hapa zaidi ya umimi. Ndio wale wale ,mwafrika mwisilamu anaona muaarabu aliyeko uarabuni ni ndugu ,jamaa,rafiki na jirarini yake zaidi ya mwafrika mwenzie ambaye ni Mkristo.Hivyo hivyo Mkristo mwaafrika anaona mzungu wa ulaya (mkristo) kuwa ni ndugu,jirani,jamaa yake zaidi ya mwaafrika mwenzake ambaye ni mwislamu .
Hilo aliwezekani hata kidogo. Kwani Tanganyika na Znz zimeungana KIMKATABA na sio KIKATIBA. Kuna mambo apo nje ya mkataba wa Muungano likiwemo hili la ardhi na makazi.
Sasa unapozungumzia maslahi ya eneo la milki ya arrdhi ni lazima uziusishe pande zote mbili kwani hili si suala la muungano. Alichofanya Tibaijuka ni ubabe kitu ambacho hakikubaliki. Ni mawili tu yanatakiwa hapo ima a withdraw hayo maombi na kuanza mchakato mpya kama nchi zote mbili zitakubaliana au kuanisha kila nchi itanufaika vipi in terms of eneo hilo.
kama OIC ilizimwa na Muungano kwanini na hili lisizimwe.
Tibaijuka amechamke lazima ajiuzuru tu hakuna mjadala.