Prof. Tibaijuka amjibu Jussa; adai Jussa amepotosha Wazanzibari

Kwanini tunafanya mzaha na muungano. Kwanini tunasema kama hatujuani? muugano ukivunjika leo - nani atakuwa mzanzibari? watanganyika hawanashida kubwa - sasa zanzibar kuna wazanzibari halisi, waasi, waishio bara, wakristu, wausi - itakuwaje? pemba nayo itaendelea kuwa zanzibar? ima itakuwa unguka na pemba? Ndiyo yale yalioandikwa, tukichakurana sana hapata baki kitu hapa. Umoja wa zanzibar upo kwa mahusiano yake ya bara pia- sio sababu kamili lakini unaunganisha tofauti za kihistoria za wazanzibar. Basi tuupe muungano stahili yake - mengine yaongeleke taratibu
 
Kwanini tunafanya mzaha na muungano. Kwanini tunasema kama hatujuani? muugano ukivunjika leo - nani atakuwa mzanzibari? watanganyika hawanashida kubwa - sasa zanzibar kuna wazanzibari halisi, waasi, waishio bara, wakristu, wausi - itakuwaje? pemba nayo itaendelea kuwa zanzibar? ima itakuwa unguka na pemba? Ndiyo yale yalioandikwa, tukichakurana sana hapata baki kitu hapa. Umoja wa zanzibar upo kwa mahusiano yake ya bara pia- sio sababu kamili lakini unaunganisha tofauti za kihistoria za wazanzibar. Basi tuupe muungano stahili yake - mengine yaongeleke taratibu

Umeongea hadi kipovu kimekutoka lakini kwa bahati mbaya sana hukufahamika nini umekiwasilisha! Naona mwisho umejikata ulimi na kushindwa hata kuweza kuyatamka maneno vizuri! Kuna neno umeliweka hapo juu (UNGUKA), naomba maana yake! Sio lazma sote tuchangie mada zinazowekwa kama huna hoja hata kusoma tu inatosha.
 
Hivi hakuna adhabu kwa Watu wa dizaini ya Jussa?
Kungekuwa na kipengele cha kumfuta uwakilishi mtu yeyote pindi anadanganya Umma!

Jusa mkurupukaji sana, anakimbilia kujaza watu jazba badala ya kuchimba taarifa.
Adhabu kwa mtu kama yeye zipo, lakini sioni kama ataadhibiwa, provided kwamba CUF na CCM ni wamoja sasa kule visiwani
 

Jusa mkurupukaji sana, anakimbilia kujaza watu jazba badala ya kuchimba taarifa.
Adhabu kwa mtu kama yeye zipo, lakini sioni kama ataadhibiwa, provided kwamba CUF na CCM ni wamoja sasa kule visiwani

Aadhibiwe kwa kosa lipi na hoja yake ipo wazi! Tatizo Tibaijuka ndio kakosa kumfahamu Jussa na badala yake gazeti la Mwananchi limeposha zaidi. Ningeomba tunapoweka comment hapa tuwe mwanzo tunaangalia pande zote za shilingi kabla ya kuanza kuchangia chochote. Kama huna uwelewa ulizia usichokifahamu kabla haijafika mwisho wa siku ukajikuta kauli zako mwenyewe zinakusuta!
 
Hapa cha kujiuliza.

Je Tibaijuka ana mandate kisharia kuweza kuiwakilisha Znz katika mambo ya ardhi kimataifa?

Someni katiba ya muungano muone mamlaka yake mwisho wapi? sio kukurupuka na kuongea kisiasa.
 
hivi huyu bwana aliingizwa na nani kwenye 'system', sio JK!??
huyu juha hatetei suk yeye na cuf wanatetea wageni wenzao.
Jusa mkurupukaji sana, anakimbilia kujaza watu jazba badala ya kuchimba taarifa.
Adhabu kwa mtu kama yeye zipo, lakini sioni kama ataadhibiwa, provided kwamba CUF na CCM ni wamoja sasa kule visiwani
 
bahari Bara haijali
uwepo wa Zanzibar Na Ally Saleh,
Habari ambayo ilivuma
sana wiki iliyopita ni ile
ya kuhusu suala la
Tanzania kupeleka ombi
katika Umoja wa Mataifa juu ya kuongeza
eneo la bahari la nchi hii
jambo ambalo kwa
hakika ni la kisheria.
Hatua hio ilielezwa
kuwa ni kupeleka andiko katika taasisi
hiyo yenye nguvu kuliko
zote duniani na ambayo
ndio mratibu wa
masuala yote ya
kimataifa ya kiulimwengu likiwemo
suala la bahari au
tuseme mipaka yote ya
nchi na nchi na pia ile ya
kimataifa.
Jambo hilo ni la kisheria kwa sababu linatokana
na Sheria ya Kimataifa
ya Bahari ambayo
Tanzania ni mtia saini
wake na kuwa bila ya
kuwepo kwa mkataba huo wa kimataifa hali
itakuwa ni ya vurugu
tupu. Sheria ya
kimataifa inaipa fursa
kila nchi iliyo mkabala
na bahari kupata eneo fulani za awali awali
mbele ya fukwe zake ili
zitumike pamoja na
mambo mengine kwa
ajili ya ulinzi na pia
kuwa ni eneo lake la kujidai.
Kisha kila nchi kama
hiyo inapata eneo la
maili nyengine nyingi
kuelekea bahari kuu
kwa ajili ya kulitumia kiuchumi kama vile
masuala ya uvuvi na
hata kutafuta rasilmali
chini ya bahari.
Inaeleweka kwa hakika
kuwa chini ya bahari kuna rasilimali kubwa
sana ambayo
wanadamu bado
hawajaweza kufikia,
lakini tayari kuna nchi
nyingi zimefaidi utajiri huo kwa sababu ya
uwezo wake wa
kisayansi.
Imani yangu itaichukua
nchi kama yetu ya
Tanzania miaka mingi na uwekezaji mkubwa
kuweza kufaidi fursa
kama hizo ingawa zimo
ndani ya haki yetu
mbele ya macho ya
kimataifa. Sasa bila ya umma kuwa na habari
za awali na katika hali
ambayo baadhi ya watu
hasa Wazanzibari
wameitilia shaka,
ujumbe wa Tanzania ulikabidhi katika Umoja
wa Mataifa lile ambalo
limeitwa ni andiko la
kutaka Tanzania
iongezewe eneo la
bahari kwa ajili ya uchumi.
Hatua hii ni kwa mujibu
wa Sheria ya Bahari,
ambapo kila nchi
inapewa fursa ya
kuomba eneo zaidi ya lile la maili 12 za
kwanza na maili 200 za
pili ambazo moja kwa
moja zimetolewa chini
ya Sheria ya Bahari.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri
Professa Anna Tibaijuka
na kumualika Waziri
mwenziwe wa Ardhi
wa Zanzibar Ali Juma
Shamhuna ambaye kwa kile alichokisema katika
Baraza la Wawakilishi
alitingwa na kazi,
akataka awakilishwe na
afisa wa Wizara hiyo
Ayoub Muhammed Mahmood.
Na inaonyesha pia
kuwa maandalizi ya
safari hiyo yalikuwa ya
muda mrefu kwa
sababu ya matayarisho ya nyaraka mbali mbali
na pia kuna ushahidi wa
ushiriki wa Zanzibar
kupitia afisa wa
kisheria kutoka Afisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.
Lakini suala hilo, likija
wakati huu wa mjadala
wa kitaifa wa
mabadiliko ya katiba,
lilishitua watu wengi upande mmoja wa
Muungano, lakini zaidi
pia Wajumbe wa Baraza
la Wawakilishi ambao
walisema
wanashangazwa na ukimya wa Serikali ya
Zanzibar juu ya suala
hilo. Waziri Ali Juma
Shamhuna alijikuta
matatani kwa kujua
taarifa hiyo lakini hadi timu inakwenda New
York inaaminika Baraza
la Mawziri halijui kitu
na hali kadhalika Baraza
la Wawakilishi, jambo
ambalo Wajumbe wamesema lina
umuhimu mkubwa kwa
nchi kwenda kimya
kimya wakati kuna haki
ya Zanzibar inatishiwa.
Haki ipi ya Zanzibar inayotishiwa? Katika
hali ya kawaida na ya
kisheria itaonekana
kuwa suala mipaka ni
suala la Muungano na
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungnao
na kwa hivyo suala hilo
likimalizwa na Jamhuri
ya Muungano basi
Zanzbiar pia itakuwa
imewakilishwa. Lakini Wazanzibari hawaoni
hivyo kabisa. Kwa
mtizamo wao ni kuwa
kwa Tanzania kwenda
kujiombea eneo la ziada
la bahari huko kuna maanisha kuipunja
Zanzibar au hata
kuichukulia haki yake ya
bahari na hivyo kutishia
Muungano wenyewe.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2009 Baraza la
Wawakilishi lilipitisha
hoja ya kutaka Serikali
ya Zanzibar isimamie
wenyewe haki zake
zote zinazohusiana na mambo ya bahari na
kutia kishindo kikubwa
kwenye Sheria ya
Bahari ya Tanzania.
Dhana ya Zanzibar ni
kuwa kweli kuna Jamhuri ya Muungano,
lakini ni kweli pia kuna
Zanzibar ambayo ina
mahitaji kamili kama
nchi na kwa hivyo
uwepo utaratibu wa kugawana rasilmali
kwa nchi mbili ziliomo
kwenye Muungano.
Kwamba ni kweli kuwa
suala la mipaka ya
bahari kama ilivyo mipaka mengine ni la
Tanzania kama nchi,
lakini lazima kuwepo na
utaratibu na hasa
makubaliano wa kujua
mipaka ya Zanzibar ni ipi kama nchi ndani ya
Muungano na haki zake
za mipaka ni zipi ndani
ya Muungano.
Ndani ya Muungano huu
Zanzibar inajisimamia kila kitu chake katika
kuendesha Serikali na
maslahi ya watu wake
na moja katika utajiri
au rasilmali ambayo
Zanzibar inayo na imeiganda ni ile ya
bahari na kwa hivyo
lazima sio tu ijue
mipaka lakini iwe na
haki kamilifu ya kuvuna
chochote kutoka bahari iliozunguka Visiwa.
Ikumbukwe kuwa
haikuwa bahati mbaya
pale mwaka jana
Zanzibar ilipofanya
mabadiliko ya 10 ya Katiba na kuingiza
kipengele kuwa eneo la
Zanzibar ni lile lote
ambalo lilikuwa eneo la
Zanzibar kabla ya
Muungano wa 1964. Kwa maana nyengine
ndani ya Muungano wa
Tanzania kunahitajika
kuwepo na mipaka ya
ndani bahari baina ya
washirika wawili. Na hili ingepaswa pia
likaririwe ndani ya
Katiba ya Muungano
kama ilivyo ndani ya
Katiba ya Zanzibar.
Zanzibar ina fikra kuwa iwe na umemiliki wa
maili zake 12 za
mwanzo upande wa
Bagomoyo na Unguja na
Tanga na Wete na kisha
iwe na maili 12 nyengine kuelekea
bahari kuu. Pia kama
ambavyo Tanzania ina
maili 200 za Continental
Shelf ambazo ni za
kiuchumi, basi ufanywe utaratibu wa ndani
ambao utatambua eneo
la Zanzibar ndani ya
eneo kubwa la
Tanzania.
Katika hili Wazanzibari hawakatai kuwa
mipaka ni ya Tanzania
na kuwa Zanzibar ni
sehemu ya Tanzania,
lakini kwa kuwa
tumekubaliana kuwa kuna nchi ya Zanzibar
ipo, basi ipate haki zake
za kinchi. Ndipo
Wazanzibari wengi
wanasubiri mshindo wa
Hoja Binafsi ambayo iliwasilishwa Jumatatu
ambayo inaitaka
Serikali ya Zanzibar
kufuatilia na kutoa
maelezo ya kina juu ya
suala hilo la mipaka ya bahari au ni vipi
Zanzibar itafaidika
katika uongezaji wa
eneo la bahari la
Tanzania.
Wengi wanaona imekuwa vyema na
kheri jambo hilo kuzuka
wakati huu kwa sababu
litapata fursa ya
kujadiliwa kwa umakini
zaidi maana inashangaza kuwa
upande wa Tanzania
Bara haujali sana
kuwepo kwa Zanzibar
kama ambapo
imedhihirika katika mambo mengi lakini la
karibu kabisa ni
kutotajwa kabisa
Zanzibar katika kitabu
cha maendeleo ya
Jumuia ya Afrika Mashariki na kupelekea
Waziri Abubakar
Khamis Bakary
kulalamika kwa Serikali
ya Muungano.
 
Hapa cha kujiuliza.

Je Tibaijuka ana mandate kisharia kuweza kuiwakilisha Znz katika mambo ya ardhi kimataifa?

Someni katiba ya muungano muone mamlaka yake mwisho wapi? sio kukurupuka na kuongea kisiasa.
Jussa alisema ukweli? Siyo unataka kupindua mada. Hapa hatuzungumzii kama Tibaijuka ana mamlaka au hana, alichosema Jussa ni kwamba ZNZ hawakushirikishwa kwenye mchakato mzima. Jee alisema Ukweli?
 
Sio Jussa peke yake na wale Wawakilishi wengine waliochangia michango ya ajabu ajabu, ina maana walikuwa wanaongea tu bila kujua ukweli au? Mimi nilidhani mtu kabla ya kuchangia hoja unatakiwa angalau uwe na taarifa hata za uchunguzi kidogo kuhusu issue yenyewe. Kama hali yenyewe ya Wawakilishi wetu ndio hiyo ya kupiga kelele tu bila kuwa na data hata kidogo basi tusishangae hii hali tuliyo nayo watanzania ni halali yetu.
 
Jussa alisema ukweli? Siyo unataka kupindua mada. Hapa hatuzungumzii kama Tibaijuka ana mamlaka au hana, alichosema Jussa ni kwamba ZNZ hawakushirikishwa kwenye mchakato mzima. Jee alisema Ukweli?

Na lingekuwa BLW limeshirikishwa katika maamuzi mazito kama haya hata Jusa asingeuliza na kumtia matatani Prof Tibaijuka?

Lakin pia Je Prof ana mandate yoyote kisheria kuiwakilisha Znz kuhusu mambo ya ardhi kimataifa?

Pitia katiba yenu ya Muungano uone alivyovunja sharia.

 
Sio Jussa peke yake na wale Wawakilishi wengine waliochangia michango ya ajabu ajabu, ina maana walikuwa wanaongea tu bila kujua ukweli au? Mimi nilidhani mtu kabla ya kuchangia hoja unatakiwa angalau uwe na taarifa hata za uchunguzi kidogo kuhusu issue yenyewe. Kama hali yenyewe ya Wawakilishi wetu ndio hiyo ya kupiga kelele tu bila kuwa na data hata kidogo basi tusishangae hii hali tuliyo nayo watanzania ni halali yetu.
 
Na lingekuwa BLW limeshirikishwa katika maamuzi mazito kama haya hata Jusa asingeuliza na kumtia matatani Prof Tibaijuka?

Lakin pia Je Prof ana mandate yoyote kisheria kuiwakilisha Znz kuhusu mambo ya ardhi kimataifa?

Pitia katiba yenu ya Muungano uone alivyovunja sharia.

Kimataifa ipo TANZANIA, ZANZIBAR haipo. Ipo kwenye ramani ya Tanzania kama ilivyo Mafia.
 
Hapa cha kujiuliza.

Je Tibaijuka ana mandate kisharia kuweza kuiwakilisha Znz katika mambo ya ardhi kimataifa?

Someni katiba ya muungano muone mamlaka yake mwisho wapi? sio kukurupuka na kuongea kisiasa.
Kwani Zanzibar ni TAIFA? TAIFA ni TANZANIA tu. Au SUK batili imewapandisha hadhi wenzetu kimyakimya? Balozi wenu UN ni nani vile? Nikumbushe Mzee Barubaru.
 
EEZ SI HOJA YA JUSSA NI
YA WAZANZIBARI Written by Ahmed Omar
Khamis // 26/01/2012
// Habari // No
comments Mhe. Ismai Jussa Ladhu
ambae ni Naibu Katibu
Mkuu wa Chama Cha
Wananchi – CUF na
Mwakilishi wa Jimbo la
mji Mkongwe ni mwanasiasa makini
asiyeyumbayumba,
hodari mchapa kazi na
mwenye uzoefu wa
kutosha katika fani yake
ya siasa. Jussa ni bingwa wa kulimudu
jukwaa na kumvutia
kila anaemsikiiza kwa
ufasaha na utamaduni
wake wa kuzungumza
mambo kwa uchambuzi na kwa msingi wa hoja.
Jussa katika harakati
zake za kisiasa na hata
katika utendaji wa
shughuli zake
anangozwa na kanuni ya kuweka mbele uwazi
na ukweli. Hii ndio
maana wasiompenda
yeye binafsi au
wasiopenda uwajibikaji
humuona Jussa ni kipingamizi au mara
nyengine adui wa
mambo yao. Mhe Jussa si mtu wa
kukurupuka bali ni
mtafiti na muweka
mbele nguvu ya hoja
katika kauli zake,
nadharia zake, maoni yake, falsafa zake na
hata matendo yake. Hii
ndio maana hamasa za
wana- CUF mara zote
huwa juu pale
mwanasiasa huyu anapopanda katika
jukwaa. Baada ya kuwa
mjumbe wa baraza la
wawakiishi ndani ya
serikali ya Umoja wa
kitaifa ya Zanzibar matumaini ya watu
kwa Jussa yametanuka
kwa kasi mno kutoka
kwa wana- CUF hadi
kwa wazanzibari wote
baada ya kuamini kwamba mwanasiasa
huyu ni mkweli na
mtetezi wa maslahi ya
wazanzibari kwa
ujumla wao na
hamugopi yeyote katika kutekeleza majukumu
yake hayo. Wazanzibari
wote kwa ujumla wao
sasa hawana wasiwasi
wakifahamu katika
chombo chao cha kuwatetea, baraza la
wawakiishi, kuna
mwanasiasa makini
Ismail Jussa ambae
huhoji bila woga jambo
lote isilokwenda sambamba na matashi
ya wazanzibari.
Tukisema hivi
hatumaanishi hakuna
wengine katika baraza
la wawakiishi au ndani ya Zanzibar ambao
wazanzibari
wamejenga matumaini
yao, wapo, lakini kwa
wanasiasa wa rika lake
yeye bado mpaka sasa anabakia kama nyota
ing’arayo. Jussa ni mtaalamu wa
siasa kwa nadharia na
utendaji na mwenye
uzoefu wa muda mrefu.
Amekuwa
akikiunganisha chama cha CUF na mataifa ya
nje kwa muda mrefu na
hivyo kuwa mtu
mweledi wa siasa za
kilimwengu na hivyo
kuweza kumudu vyema mazingira yote ya
kisiasa pamoja na
changamoto za kisiasa
za kila nyakati ndani ya
nchi yetu na kuzaa fikra
za mabadiliko ya msingi katika mwelekeo wa
siasa na utawala ndani
ya chama na nchi yetu.
Jussa ni mweledi wa
historia ya ndani ya nchi
yetu na ya ulimwengu kiujumla, hivyo si rahisi
kumburuza na kumtoa
katika uhalisia wa
mambo mbali mbali
yaliyojiri na yanayojiri
ndani ya nchi yetu. Kupitia udadisi wake
makini wa kihistoria
amekuwa ni mtu
anaeifahamu sana
Zanzibar. Pia
anaifahamu sana Tanganyika na
halkadhalika
anaifahamu sana
Tanzania. Hii ndio
maana mara nyingi
anapotoa hoja yoyote yenye msingi wa
kihistoria, kisiasa au
kitaifa basi hupita
vyema katika uhalisia
wake na sio
kukurupuka, hivyo kuibuka kuzipiku hoja
dhaifu hata zinazotlewa
na watu wenye vyeo
vikubwa hapa nchini. Katiaka makala yake
inaysema Jussa:
Zanzibar ni koloni la
Tanzania?
Aliyoichapisha katika
gazeti a Mwanahalisi la tarehe 25-31 Januari
2012, Mbasha Asenga
ameandika kuhusu
Ismail Jussa akimsifu na
wakati huo huo
akimponda. Lakini haishangazi kwani
mwandishi huyu wa
makala ni hodari wa
kuandika makala zisizo
na nguvu ya hoja, zisizo
na kichwa wala miguu na zinazoandikwa kwa
madhumuni ya
kukichafua chama cha
CUF na viongozi wake
na kukifagilia chama
cha CHADEMA. Hivyo basi, mwandishi yupo
zaidi kutumikia siasa za
CHADEMA na sio kueleza
uhalisia wa mambo.
Katika Makala yake hiyo
mwandishi amepotosha mengi, basi nimeonelea
ni vyema nikatumia
makala yangu hii
kumsahihisha juu ya
kile alichokiandika ili
yeye na wasomaji wake wapate kuelewa
uhalisia wa
alichokiandika badala
ya kuendekeza ushabiki
wake na upotoshaji.
Katika makala hii hatutafundishana
historia ya Zanzibar, ya
Tanganyika wala ya
Muungano kwa kuwa
sio maudhui yake ila
nitazichambua hoja dhaifu za Mbasha
Asenga kwa kutumia
suala hili hili alilolitumia
yeye lililozuka hivi
karibuni, ambalo ni
hatua ya Jamhuri ya Munngano kupeleka
ombi katika Umoja wa
mataifa kutaka
kuongezewa ziada ya
eneo la bahari
(Exclussive Economic Zone- EEZ). Mwandishi
ametumia suala hilo na
kujenga hoja
zinazolenga kumchafua
Mhe Jussa binafsi na
Chama cha CUF kwa maslahi na ushabiki wa
chama cha CHADEMA.
Lengo la Mbasha Asenga
ni kufanikisha kujenga
picha potofu kwa
Watanzania ya kwamba chama cha CUF na
vingozi wake
wanaonekana
hawaitaki na
wanaichukia
Tanganyika kama vile CHADEMA ilivyokuwa
haiitaki na inaichukia
Zanzibar. Kwa mujibu wa makala
yake, Mbasha Asenga
anaonekana haijui
vyema historia ya
Muungano wetu wa
Tanzania na kwa maaana hiyo siachi
wasiwasi wangu
kwamba hajui historia
ya Zanzibar nchi
ambayo ilikuwepo
karne nyingi kabla ya Tanganyika. Kama
wasiwasi wangu huu ni
kweli basi simshangai
Mbasha Asenga
kutokukujua kwamba
Nyrere na Karume walipounganisha nchi
mbili ya Tanganyika na
Zanzibar hawakuiweka
bahari katika orodha ya
mambo ya Muungano.
Na hata baada ya Tanganyika
kuuchakachua mkataba
wa muungano wa
kimataifa kati ya
Zanzibar na Tanganyika,
kwa kuongeza mambo ya muungano
kinyemela bila ya
kuishirikisha Zanzibar
kama nchi mwenza
(partner state) katika
Muungano ambapo kufanya hivyo ni kosa
kwa sheria za
kimataifa, suala la
bahari bado mpaka sasa
lingali si suala la
Muungano. Sasa nije katika hoja
zake mwandishi
alizozitoa katika makala
yake hiyo kama vile 1.
Jussa hajafunguka
kisiasa, 2. Jussa anaamini katika himaya
ndogo ndogo, yaani
Uzanzibari na si
Utanzania, 3. CUF
inapigania Uzanzibari
na si Utanzania, 4. Jussa kupinga Tanzania
kuongezewa eneo zaidi
la bahari na hoja
nyengine kama hizo. Tanzania ni nchi mbili,
Tanganyika na Zanzibar.
Nchi zote mbii hizi zina
mipaka yake na
mamlaka yake. Mipaka
na mamlaka ya Zanzibar yameelezwa vizuri
katika katiba ya
Zanzibar. Katiba ya
Zanzibar, Ibara ya 1
inaeleza, “Zanzibar ni
nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo
lote la visiwa vya
Unguja na Pemba
pamoja na visiwa
vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar
ikiitwa Jamhuri ya
Watu wa Zanzibar”.
Hivyo basi katika
Jamhuri ya muungano kuna nchi ya Zanzibar,
na ukiitoa nchi hiyo
inabaki nchi ya
Tanganyika. Kwa bahati
mbaya sana upande wa
Tanganyika wameikataa nchi yao
na kulikataa hata jina
lake la Tanganyika na
kutunga jina jipya
linaloitwa Tanzania
bara. Kama suala la upande wa Tanganyika
kutupa nchi yao na
kufuta jina si la bahati
mbaya na linaonekana
ni sawa basi kwa
upande wa Zanzibar si sawa hata kidogo. Kwa
wazanzibari ni kosa
kubwa lisilosameheka
kwa mtu yoyote
kujaribu kuondoa nchi
au jina la Zanzibar. Kwa maana hiyo kama
Watanganyika hawapo
tena basi ni tofauti
kabisa kwa upande wa
pili. Wazanzibari wapo
na ni wazalendo kikwelikweli wa
kizanzibari kwanza
halafu ndio unafuata
Utanzania. Wazanzibari
wana utamaduni wao
na historia yao tofauti na Tanganyika au nchi
nyengine za Afrika ya
Mashariki inayopaswa
kulindwa na kuenziwa
kwa maslahi ya
wazanzibari. Hoja ya kupinga
Jamhuri ya muungano
kuongezwa eneo la
bahari jambo ambalo
kimsingi halimo katika
orodha ya mambo ya muungano si hoja ya
Jussa bali ni hoja ya
wazanzibari wote.
Mbasha Asenga
anaonekana si
mfuatiliaji mzuri wa yale yanayojiri Zanzibar
kama upande wa pili
wa Jamhuri ya
Muungano. Halkadhalika
anaonekana hafahamu
kama huku Zanzibar kuna Serikali yenye
katiba yake, yenye
mamlaka yake, yenye
Rais wake, yenye
Baraza la Mapinduzi
(Baraza la Mawaziri la Zanzibar), yenye Baraza
la Wawakiishi (Bunge la
Zanzibar), yenye
Mahakama zake na
mambo yote mengine
muhimu ya kiutawala. Mbasha hajui kwamba
Zanzibar inatunga sera
zake za kuendesha nchi,
ina bajeti yake,
inapitisha maamuzi
yake ya kinchi kwa maslahi ya watu wake,
yaani wazanzibari na
ndio Serikali ambayo
wazanzibari
wanayoitambua kama
mdhamini wa mambo yao yote. Mwaka 2009 Baraza la
Mapinduzi lilipitisha
uwamuzi wa kuliondoa
suala la mafuta na gesi
asilia katika orodha ya
mambo ya muungano, wakati huo Jussa si
mwakiishi wala chama
chake CUF si mdau wa
Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar. Kuhusu suala
la bahari kuu, na Eneo tengefu la kiuchumi
(Exclussive economic
Zone – EEZ) nalo Baraza
la wawakiishi katika
kikao chake cha tarehe
08 Aprili, 2009, (Baraza la Saba, Mkutano wa
Kumi na Tano), lilikuwa
na mjadala mzito wa
siku tatu mfululizo
kuhusu ‘Taarifa ya
Mapendekezo ya Serikali kuhusu Ripoti
ya Mshauri Muelekezi
juu ya Utafutaji na
Uchimbaji wa Mafuta na
Gesi Asilia’ ambapo
kutokana na uzito wake, wajumbe 49
wakiwemo
Waheshimiwa Mawaziri
wengi wa wakati ule na
pia Waheshimiwa
Mawaziri wengi tulio nao sasa walichangia
mjadala huo, tena kwa
hisia kali za kizalendo
na mapenzi ya kweli
kwa nchi yetu tukufu.
Baada ya mjadala huo, hatimaye Mheshimiwa
Spika aliwahoji
Wajumbe kuhusiana na
maazimio matatu
yaliyowasilishwa na
Serikali. Azimio la tatu lilikuwa ni lile la kutaka
“exclussive ecnmic
zone” (EEZ) isiwe ya
mashirikiano kati ya
serikali ya Jamhuri ya
muungano na serikali ya Zanzibar bali suala
hilo lishughuikiwe na
Zanzibar Peke yake.
Kwa msingi huo
ingetegemewa basi na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano isichukue
hatua zozote
zitakazopelekea
kuyafanya maazimio
haya ya Baraza la
Wawakilishi ambayo ndiyo msimamo rasmi
wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar
yakawa hayana maana
tena. Kitendo cha
kupeleka maombi Umoja wa Mataifa
kutaka kuongezewa
ukanda wa bahari kuu
ambao tayari Zanzibar
imeamua kila upande
isimamie wenyewe, ni kwenda kinyume na
dhamira (spirit) hiyo na
hakiashirii kuwepo kwa
nia njema. Masuala hayo mawili
yalioamuliwa na
mihimii miwili mikuu
ya seriakli ya Mapinduzi
ya Zanzibar mwaka
2009 ndio ambayo Jussa alilikumbushia
katika Baraza a
wawakiishi hivi juzi.
Hivyo basi
kinachotengua hatua ya
Jamhuri ya muungano kuomba eneo hilo
katika Umoja wa
Mataifa si hoja ya Jussa
bali ni uwamuzi wa
SMZ. Liko wapi kosa la
Jussa hapo kwa hatua yake ya kukumbusha
maamuzi ya SMZ
ambayo yeye
mwenyewe hakushiriki
kuyafanya? Kwa nini
Mbasha Asenga asiseme seriakali ya Mapinduzi
ya Zanzibar iliyotoa
msimamo na maamuzi
hayo tokea mwaka
2009 ndio inayoamini
himaya ndogo ndogo (Uzanzibari ) na
kupuuza Utanzania?
Baraza la Mapinduzi la
Zanzibar la mwaka
2009 lilikuwa na
Mawaziri kutoka CCM tu Pale Iilipoamua
kuyaondoa mafuta na
gesi asilia kutoka katika
orodha ya mambo ya
muungano, jee CCM
hapa haitetei Uzanzibari na kupuuza Utanzania
kwa mujibu wa hoja ya
Asenga? Jee CCM hapa
kwa hoja hiyo hiyo
haiamini mamlaka
ndogo ndogo? Baraza la Wawakiishi la Zanzibar
wakati azimio la EEZ
linapitishwa mwaka
2009 lilikuwa na
theluthi 2 ya wajumbe
kutoka CCM ambao wana uwezo wa
kupitisha maamuzi
yeyote bila ya kura za
wajumbe wa CUF,
kinyume na sasa
ambapo hakuna chama kati ya CCM na CUF
kinachofikisha theluthi
2 za wajumbe katika
Baraza hilo. Utawezaje
kuuita uwamuzi huo au
msimamo huo wa mwaka 2009 kuwa ni
wa CUF? Hoja ya hivi
juzi ya Mhe Jussa
ambayo ndio
inayomuumiza kichwa
Mbasha Asenga ya kukumbushia lazimio la
Baraza la Wawakilishi la
mwaka 2009 iliungwa
mkono kwa hisia kali na
wajumbe 8 wa Baraza
la Wawakilishi, kwa uwiano sawa kwa sawa
kutoka CUF na CCM, tena
inakuwaje hata CUF
peke yake katika hoja
hii ndiyo inayotetea
Uzanzibari na siyo CCM? Hapa ndipo ninaposema
Mbasha Asenga ni
mwana propaganda safi
wa CHADEMA na sio
mchambuzi na wala
haelewi kitu katika uchambuzi wa mambo
haya ya siasa za
Tanzania katika uhalisia
wake, na si mwenye
lengo la
kuwafahamisha Watanzania ukweli.
Maoni yangu kwa
Asenga asiamini
kwamba Wazanzibari
wakipigania haki za
nchi yao wameukataa Muungano bali kilicho
muhimu kwake ni
kwamba na yeye
aamini kama ni
Mtanganyika na hivyo
ana kila sababu ya kudai nchi yake iliyofutwa
jina lake na Nyerere.
 
mpemba mbishi
bahari Bara haijali uwepo wa Zanzibar​
Na Ally Saleh,
Habari ambayo ilivuma sana wiki iliyopita ni ile ya kuhusu suala la Tanzania kupeleka ombi katika Umoja wa Mataifa juu ya kuongeza eneo la bahari la nchi hii jambo ambalo kwa hakika ni la kisheria. Hatua hio ilielezwa kuwa ni kupeleka andiko katika taasisi hiyo yenye nguvu kuliko zote duniani na ambayo ndio mratibu wa masuala yote ya kimataifa ya kiulimwengu likiwemo suala la bahari au tuseme mipaka yote ya nchi na nchi na pia ile ya kimataifa.Jambo hilo ni la kisheria kwa sababu linatokana na Sheria ya Kimataifa ya Bahari ambayo Tanzania ni mtia saini wake na kuwa bila ya kuwepo kwa mkataba huo wa kimataifa haliitakuwa ni ya vurugutupu.

Sheria ya kimataifa inaipa fursa kila nchi iliyo mkabala na bahari kupata eneo fulani za awali awali mbele ya fukwe zake ili zitumike pamoja na mambo mengine kwa ajili ya ulinzi na pia kuwa ni eneo lake la kujidai. Kisha kila nchi kama hiyo inapata eneo la maili nyengine nyingi kuelekea bahari kuu kwa ajili ya kulitumia kiuchumi kama vile masuala ya uvuvi na hata kutafuta rasilmali
chini ya bahari.Inaeleweka kwa hakika kuwa chini ya bahari kuna rasilimali kubwa sana ambayo wanadamu bado hawajaweza kufikia, lakini tayari kuna nchi nyingi zimefaidi utajiri huo kwa sababu ya uwezo wake wa kisayansi. Imani yangu itaichukua
nchi kama yetu ya Tanzania miaka mingi na uwekezaji mkubwa kuweza kufaidi fursa kama hizo ingawa zimo ndani ya haki yetu
mbele ya macho ya kimataifa.

Sasa bila ya umma kuwa na habari za awali na katika hali ambayo baadhi ya watu hasa Wazanzibari
wameitilia shaka, ujumbe wa Tanzania ulikabidhi katika Umoja wa Mataifa lile ambalo limeitwa ni andiko la kutaka Tanzania iongezewe eneo la bahari kwa ajili ya uchumi.Hatua hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Bahari, ambapo kila nchi inapewa fursa ya kuomba eneo zaidi ya lile la maili 12 za kwanza na maili 200 za pili ambazo moja kwa moja zimetolewa chini ya Sheria ya Bahari.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri Professa Anna Tibaijuka na kumualika Waziri mwenziwe wa Ardhi wa Zanzibar Ali Juma
Shamhuna ambaye kwa kile alichokisema katika Baraza la Wawakilishi alitingwa na kazi, akataka awakilishwe na afisa wa Wizara hiyo Ayoub Muhammed Mahmood.

Na inaonyesha pia kuwa maandalizi ya safari hiyo yalikuwa ya muda mrefu kwa sababu ya matayarisho ya nyaraka mbali mbali na pia kuna ushahidi wa ushiriki wa Zanzibar kupitia afisa wa kisheria kutoka Afisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.Lakini suala hilo, likija wakati huu wa mjadala wa kitaifa wa mabadiliko ya katiba, lilishitua watu wengi upande mmoja wa Muungano, lakini zaidipia Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ambao walisema wanashangazwa na ukimya wa Serikali yaZanzibar juu ya suala hilo. Waziri Ali Juma Shamhuna alijikuta matatani kwa kujua taarifa hiyo lakini hadi timu inakwenda New York inaaminika Baraza la Mawziri halijui kitu na hali kadhalika Baraza la Wawakilishi, jambo ambalo Wajumbe wamesema lina umuhimu mkubwa kwa nchi kwenda kimya kimya wakati kuna haki ya Zanzibar inatishiwa. Haki ipi ya Zanzibar inayotishiwa? Katika hali ya kawaida na ya kisheria itaonekana kuwa suala mipaka ni suala la Muungano na Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungnao na kwa hivyo suala hilo likimalizwa na Jamhuri ya Muungano basi Zanzbiar pia itakuwa imewakilishwa.

Lakini Wazanzibari hawaoni hivyo kabisa. Kwa mtizamo wao ni kuwa kwa Tanzania kwenda kujiombea eneo la ziada la bahari huko kuna maanisha kuipunja Zanzibar au hata kuichukulia haki yake ya bahari na hivyo kutishia Muungano wenyewe. Itakumbukwa kuwa mwaka 2009 Baraza la Wawakilishi lilipitisha hoja ya kutaka Serikali ya Zanzibar isimamie wenyewe haki zake zote zinazohusiana na mambo ya bahari nakutia kishindo kikubwa kwenye Sheria ya Bahari ya Tanzania. Dhana ya Zanzibar ni kuwa kweli kuna Jamhuri ya Muungano, lakini ni kweli pia kuna Zanzibar ambayo ina mahitaji kamili kama nchi na kwa hivyo uwepo utaratibu wa kugawana rasilmali kwa nchi mbili ziliomo kwenye Muungano. Kwamba ni kweli kuwa suala la mipaka ya bahari kama ilivyo mipaka mengine ni la Tanzania kama nchi, lakini lazima kuwepo na utaratibu na hasa makubaliano wa kujua mipaka ya Zanzibar ni ipi kama nchi ndani ya Muungano na haki zake za mipaka ni zipi ndani ya Muungano. Ndani ya Muungano huu Zanzibar inajisimamia kila kitu chake katika kuendesha Serikali na maslahi ya watu wake na moja katika utajiri au rasilmali ambayo Zanzibar inayo na imeiganda ni ile yabahari na kwa hivyo lazima sio tu ijue mipaka lakini iwe na haki kamilifu ya kuvuna chochote kutoka bahari iliozunguka Visiwa.

Ikumbukwe kuwa haikuwa bahati mbaya pale mwaka jana Zanzibar ilipofanya mabadiliko ya 10 ya Katiba na kuingiza kipengele kuwa eneo la Zanzibar ni lile lote ambalo lilikuwa eneo la Zanzibar kabla ya Muungano wa 1964. Kwa maana nyengine ndani ya Muungano wa Tanzania kunahitajika kuwepo na mipaka ya ndani bahari baina ya washirika wawili. Na hili ingepaswa pia likaririwe ndani ya Katiba ya Muungano kama ilivyo ndani ya Katiba ya Zanzibar. Zanzibar ina fikra kuwa iwe na umemiliki wa maili zake 12 za
mwanzo upande wa Bagomoyo na Unguja na Tanga na Wete na kisha iwe na maili 12 nyengine kuelekea bahari kuu. Pia kama ambavyo Tanzania ina maili 200 za Continental Shelf ambazo ni za kiuchumi, basi ufanywe utaratibu wa ndani ambao utatambua eneo la Zanzibar ndani ya eneo kubwa la Tanzania.

Katika hili Wazanzibari hawakatai kuwa mipaka ni ya Tanzania na kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, lakini kwa kuwa tumekubaliana kuwa kuna nchi ya Zanzibar ipo, basi ipate haki zake za kinchi. Ndipo Wazanzibari wengi wanasubiri mshindo wa Hoja Binafsi ambayo iliwasilishwa Jumatatu ambayo inaitaka Serikali ya Zanzibar kufuatilia na kutoa maelezo ya kina juu ya suala hilo la mipaka ya bahari au ni vipi Zanzibar itafaidika katika uongezaji wa eneo la bahari la Tanzania. Wengi wanaona imekuwa vyema na kheri jambo hilo kuzuka wakati huu kwa sababu litapata fursa ya kujadiliwa kwa umakini zaidi maana inashangaza kuwa upande wa Tanzania Bara haujali sana kuwepo kwa Zanzibar kama ambapoimedhihirika katika mambo mengi lakini la karibu kabisa ni kutotajwa kabisa Zanzibar katika kitabu cha maendeleo ya Jumuia ya Afrika Mashariki na kupelekea Waziri Abubakar Khamis Bakarykulalamika kwa Serikaliya Muungano.

MPEMBA MBISHI NIMEKUSAIDIA KUHARIRI

 
Hapa cha kujiuliza.

Je Tibaijuka ana mandate kisharia kuweza kuiwakilisha Znz katika mambo ya ardhi kimataifa?

Someni katiba ya muungano muone mamlaka yake mwisho wapi? sio kukurupuka na kuongea kisiasa.

sasa ulitaka nani aiwakilishe tuambie
 
sasa ulitaka nani aiwakilishe tuambie


Kisharia zenu alitakiwa kuwasilisha ni waziri wa Mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa. Kwani yeye ana mamlaka kisheria kuwakilisha mambo ya muungano katika shughuli za mahusiano ya kimataifa.

Tibaijuka amevunja sharia hapo. Na ndipo tunapodai lazima awajibishwe na kujiuzuru
 
Back
Top Bottom