Prof Shivji: Uwaziri ni kujuana tu.

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
Send to a friend
Tuesday, 30 November 2010 23:47
0
digg
Sadick Mtulya
MHADHIRI maarufu wa masuala ya
kisiasa na kijamii, Prof Issa Shivji
ameliponda baraza jipya la mawaziri
akisema kuwa limeundwa kwa utashi
wa kisiasa ili kulipana fadhila.
Prof Shivji, ambaye ni mwenyekiti wa
Kigoda cha Mwalimu Nyerere ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam, pia aliungana
na wadau wengine wanaolilia
mabadiliko ya katiba akisema
suluhisho la matatizo mengi nchini ni
kuundwa na katiba mpya
itakayotokana na utashi wa
wananchi.Maoni yake yametokana na
uteuzi wa baraza lenye mawaziri 50
uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete
ambaye aliongeza mawaziri wapya 24
na kutema tisa baada ya kuchaguliwa
kuongoza nchi kwa miaka mitano ya
mwisho ya serikali ya awamu ya nne.
Baraza hilo lilianza kazi zake rasmi
jana, lakini katika mahojiano na kituo
cha televisheni cha Channel Ten Shivji,
ambaye amebobea kwenye sheria
lakini ambaye amejishughulisha sana
na siasa, alilizungumzia baraza hilo
kuwa ni limeundwa kwa lengo la
kulipa fadhila na si kwa kuzingatia
uwezo.
“Kimsingi na kimantiki uteuzi na
ukubwa wa baraza la mawaziri kwa
nchi nyingi za Kiafrika na hata hili la
Tanzania unatokana na utashi wa
kisiasa hasa undugu na urafiki kwa
lengo la kulipa fadhila," alisema
Profesa Shivji.
"Mara chache uteuzi huzingatia
mahitaji ya wananchi na maslahi ya
taifa kwa ujumla. Ukubwa wa baraza si
kipimo cha utendaji bora. ’’
Profesa Shivji, ambaye alikuwa
mhadhiri wa UDSM, alifafanua kwamba
ndio maana wagombea ubunge
walilazimika kumpigia debe mgombea
urais wakati wa kampeni kwa lengo la
kutaka kulipwa fadhila ya kuteuliwa
kuwa waziri au naibu waziri
Alisema suala hilo pia linachochewa na
sheria inayokazi9misha waziri
ateuliwe kutoka miongoni mwa
wabunge.
Profesa huyo alisema kimsingi kazi ya
mawaziri ni kusimamia sera pamoja na
utendaji na si vinginevyo.
Kikwete, ambaye aliunda baraza la
mawaziri 60 alipoingia Ikulu jkwa
mara ya kwanza mwaka 2006, aliteua
mawaziri watatu zaidi ya wale
waliokuwemo kwenye baraza
lililomaliza muda wake ambalo
aliliteua mwaka 2008 baada ya Edward
Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu.
Baraza hilo pia linaponekana
kuzingatia uwakilishi wa kanda na
mikoa na linajumuisha mabadiliko
kadhaa ambayo mkuu huyo wa nchi
aliyaelezea kuwa yamefanywa ili
kuongeza ufanisi, ikiwa ni pamoja na
kuhamisha baadhi ya idara kutoka
wizara moja hadi nyingine na kuigawa
Wizara ya Miundombinu kuwa katika
wizara mbili.
Prof Shivji alisema kufanya mabadiliko
ya muundo wa Baraza la Mawaziri bila
kubadilisha mfumo ni sawa na kufanya
bure.
Lakini alimshauri Rais Kikwete kuwa
makini katika uteuzi wa makatibu
wakuu wa wizara pamoja na manaibu
wao, akimtaka azingatie uwezo katika
utendaji.
“ Katibu mkuu ndiye mtendaji wa
shughuli za kila siku za wizara. Kazi ya
waziri ni kusimamia sera na utendaji
tu," alisema Prof Shivji.
“ Rais Kikwete anatakiwa kufanya kazi
ya ziada katika kuteua makatibu
wakuu... muhimu ni lazima wawe
wasomi wazuri, wenye uwezo na
watakaokuwa wepesi wa kuelewa
wanachoshauriwa na wataalamu, ’’
alisema Profesa Shivji
Profesa huyo alisema kulingana na hali
ya uchumi ilivyo nchini, serikali ya
Kikwete inakabiliwa na changamoto
nyingi hasa ya kuhakikisha nchi
inazalisha zaidi kuliko ilivyo sasa.
Alisema pamoja na kwamba asilimia
80 ya Watanzania ni wakulima, sekta
hiyo inachangia katika pato la taifa
kwa asilimia 26, akifafanua kuwa
kiwango hicho kinamaanisha kuwa
Watanzania wanazalisha kwa asilimia
26.
Mhadhiri huyo ambaye ni
mwanaharakati wa ardhi alisema
katika miaka ya 50, kilimo nchini
kilifanya vizuri na nchi ilikuwa
ikizalisha kwa wastani wa zaidi ya
asilimia 50, lakini kiwango hicho
kimekuwa kikishuka kila mwaka.
“ Ukiniuliza sababu ya hili, nitakueleza
tu kuwa tumeua kwa makusudi
viwanda vyetu pamoja na kilimo,’’
alisema
Alifafanua kwamba ili nchi yoyote
iweze kuendelea, ni lazima uzalishaji
wake uwe mkubwa na hasa kutoka
kwa wazalishaji wadogo wa vijijini na
kwamba uchumi unayumba kutokana
na wazalishaji wadogo
kutothaminiwa.
Alisema ili nchi ipige hatua ya
kimaendeleo ni lazima kilimo cha
umwagiliaji kipewe nafasi kubwa
pamoja na kuwepo kwa zana za kisasa
za kilimo, ikiwa ni pamoja na
wakulima kukopeshwa fedha kutoka
katika benki.
“ Wanasema Tanzania ni maskini lakini
cha ajabu ina benki nyingi tena za
kimataifa ambazo haziko tayari
kuwakopesha wakulima, ’’ alisema.
“Serikali ndio ilipaswa kuwa dhamana
kwa wakulima kukopa lakini haiko
tayari katika hilo. ’’
Gwiji huyo wa sheria na aliyebobea
katika masuala ya katiba alikwenda
mbali na kusema pamoja na mambo
mengine suluhisho la matatizo mengi
nchini ni kuundwa kwa katiba mpya
itakayotokana na utashi wa wananchi.
Profesa Shivji alisema kinachopaswa
kuzingatiwa kwa sasa ni ni jinsi katiba
hiyo itakavyoundwa ili iweze kupata
uhalali wa wananchi wote.
“ Hapa napenda wananachi waelewe
kuwa unapozungumzia katiba mpya,
huzungumzii muundo wake bali jinsi
inavyotungwa ili iweze kupata uhalali
wa wananachi wote na si tu yale
yatakayokuwemo ndani yake, ’’ alisema
Alifafanua kwamba katiba ya sasa
ambayo ni ya mwaka 1977, ilitokana
na mfumo wa kisiasa wa chama kimoja
pamoja na hivyo kushirikisha watu
wachache.
Alisema hali hiyo inaifanya katiba iwe
haikidhi utashi wa Watanzania walio
wengi kutokana na kwamba haiendani
na mazingira ya kisiasa, kiuchumi na
kiutamaduni yalivyo sasa.
Alitoa mfano wa katiba mpya ya nchini
Kenya ambako alisema ilitokana na
wananchi na kwamba pamoja na
mambo mengine imepunguza
madaraka ya rais, ikiwa ni pamoja na
ukubwa wa Baraza la Mawaziri
kutokana na kueleza bayana kuwa
lisiwe na chini ya watu 14 na lisizidi
watu 24.
“ Wamekwenda mbali zaidi na sheria
kutaka wanaoteuliwa kuwa mawaziri
wasiwe wabunge, bali wathibitishwe
na Bunge, ’’ alisema .
 
Back
Top Bottom