Prof. Safari awajibu wanazuoni wa kiislamu kuhusu DC

Wewe Prof. Abdallah Safari unaimbishiwa wimbo ambao hujui umeanzia wapi?

Utatumika na hao jamaa kama mwavuli kudhalilisha dini yako ukiiisha wanakutupa!

Ukitaka ku-proove gombea uongozi wa juu uone mziki wake

Hutakuwa Prof. wa ukweli tena utakuwa profesa njaa..pole sana

watch out ..we are watch the movie..jitambue

Mi nadhani Prof. Safari amefanya jambo zuri tu kuonyesha msimamo wa chama.
Chama lazima kionyeshe nini kinaamini na sio kuendeshwa na watu wanaojiita viongozi wa dini.

Hii nchi kwa ukweli sio rahisi kupiga hatua mana dini zimeingia sana jamii na watu wanakuwa influenced na statement za watu wachache wanaojiita viongozi wa dini.
Angalau kusikiliza viongozi wa siasa ambao wanachaguliwa na wananchi kuliko hawa wanaojiita viongozi wa dini ambao wengu huwa wanajipa madaraka kama vile wana mawasiliano na Mungu.

Mimi kwa kweli nachukia sana, japo naamini Mungu, lakini viongozi wa dini hasa tanzania mana ndio wanaongeza wananchi kuwa wajinga na waoga kutetea haki zao...na matunda yake ni umasikini.
Embu fikiria watu kama hawa wanaojiita viongozi wa waisilamu, wao wanajali HIJABU kuliko uovu ambao mamilioni ya watu wanafanyiwa na hao viongozi wadhalimu na wengine wanavaa Hijabu au kanzu au misalaba kuficha maovu yao. Huyu DC ni muhalifu kama wahalifu wengine, huwezi kutetea HIJABU na kusahau ukweli kuwa alitaka kuiba haki hata ya waisilamu ambao kweli wanataka mabadiliko.....
kama nchi yetu inasema haina dini mi nashauri ipige marufuku haya matamko yanayotolewa kiholela.....Huyu DC hakuhukumiwa kama Muislamu bali kama mhalifu.....kwani mhalifu wa kiislamu akipelekwa Gerezani wanavaa Hijabu? Ni kwa vile nchi haina dini so....tusiruhusu watu wachache wenye interests zao kupoteza malengo ya watu wanaotaka maendeleo....wao waendelee na imani zao na kuacha sheria isiyokuwa na dini ifanye kazi!
 
ccm wanaposhindwa kwenye medani ya siasa hujaribu kutumia medani ya udini wakifikiri kuwa itawaokoa ili wapate huruma ya wapiga kura.

All in all ccm wanawatumia viongozi wa dini na baadhi ya waandishi as a political GIMMICK
 
Siasa bhana!!! Nashindwa kutambua nini maana ya majibizano "nijuavyo ili kuzuia majibizano ni mmoja akisema mwingine hunyamaza".Sasa hii ya Safari na press conference nadhani inamushkeli kidogo.Kwa kuwa amejibu nadhani yaweza kuwa mwanzo mpya wa majibizano na Wana wa Zuoni.Kwanza kwa nini Tamko hilo litolewe na Prof. Safari? maake yeye si msemaji wa Chama.Je! ni kwa sababu yeye ndiye Muislam aliyebora ndani ya Chadema na anaweza kukabiliana na Waislam wenzie?

Kuna kosa gani kusema Prof. Safari anatumiwa kuwahujumu waislam wenzie.Hapa napata shida,Safari hata kama ni Mwanazuoni lakini hii si status yake,utambulisho wake ni Siasa na hivyo ni Mwanasiasa.Hakuwahi kuwa imamu,sheikh na pengine hata alhaji.

Tusitumie dini vibaya katika siasa na kuwatumia Waislam kuwa hujumu Waislam wenzao.Leo hii ikitokea ata Sister kavuliwa gauni lake lazima mengi yatasemwa pasipo kujali aliyemvua alikuwa Mkiristu ama Muislam.Mavazi ya dini yaheshimiwe kwani ndio utambulisho wa mtu na imani yake.Kitendo cha Wanaume kumshikashika Mwanamke asiye wake (mke) ni utovu wa maadili, ndio maana polisi wa kike na mtuhumiwa wa kike na hivyo kwa wanaume kwa wanaume.

Hivi CDM haikuwa na Wanawake wa kwenda kumtomasa huyo mama? pengine kesi hii ingekuwa tofauti.



sasa na wewe ndugu yangu umemkuta muhalifu usubiri upoteze ushahidi wakati unatafuta mwanamke wa kumkamata?

yaani sister umkute anafanya wizi eti kisa kavaa la kisister asikamatwe

ifike wakati sasa viongozi wa dini wakemee watu wanaodhalilisha dini kwa kufanya uharifu huku wamevaa mavazi yanayotambulisha dini husika bila kuacha kukemea kitendo chenyewe cha uharifu
 
Chadema ni wadini sana and ni chama cha kikristo,thats why hakikubaliki mikoa ya pwani and zenji! Chadema wanawadharau sana waislamu,sijui kwanini?? Waislamu msikubali,komaeni hadi hawa WANAFIKI CHADEMA UNAFIKI UWAISHE!! Me nawashauri mfanye maandamano nchi nzima ya kuipinga chadema! Hawa cdm hawana adabu kabisa
sawa mkuu ndo maana cuf wanakubalika sana pwani na zenj...waipinge nnhi nzima kwa lipi mtu kuvuliwa hijabu nongwa tena kwa ujinga wake mwenyewe...magdalena sakaya mbunge cuf aliwekwa rumande urambo pamoja na wanaume mwezi mzima hakuna aliyepiga kelele.....Josephine Mshumbusi alivuliwa suruali na kipigo juu akiwa mjazito na kila mtu alikishudia laivu kwene tv hakuna aliyepiga kelele au kwa sababu dc ni ccm...tunapojadili tujadili beyond ushabiki wa vyama
 
Uroho wa madaraka na njaa ya profesa Safari itawaponza Chadema.Huyu profesa uchwara CUF walimshtukia mapema na uroho wake.Kwa ndani waligundua anatumika kuuwa vyama vya upinzani ndipo akatimkia Chadema.
Fursa mliyopewa CHADEMA mnaipoteza.Kiburi chenu kitawaondoa kabisa katika uwanja wa siasa.
Hivi Chadema muko na ubavu kweli wa kupambana na waislamu wa Tanzania!.
Chadema Nendeni huko na ujinga wenu.
 
Please we need to prevent the incidence of discriminatory stereo types, we need to come together and get rid of this kind of hate speeches.

As you know Tribes were there before all this kind of religions... so we need to be very careful...

As you know religious identity is not as strong as tribal identity, so if we started regime of addressing a religion rights to the country which has a tribal identity more linear than religions.

This will lead to genocide, discrimination, prejudice, cleansing this has been increased all over the world

We have just enough religion to make us hate, but not enough to make us love one another.
Ignorance and intolerance are the major cause.
We all have equal access to all institutions in TZ why Muslims are causing this kind of discrimination?
We need to get rid of this polarizing politicians who caused immense problems they only mind and think about their elections
Hate Means of expressions and crying that Muslim are the one who have been oppressed for 50yrs there were no rights for Muslim the mind set.
Let us work hand in hand to promote harmony!!!
 
Magamba wameishiwa hoja sasa wameamua kutumia Udini kama silaha yao ya mwisho,yatakwisha mbona waTz wameamka sana kwa sasa kwani hata huu mpango wao wataupuuza tu,huu ulikua ni mpango wa ccm tu juu ya huyu Dc ili ionekane Cdm wakorofi kwa hyo hili halikubaliki hata kidogo alofanyiwa Dc yalikua sahihi tu
 
I think hata kutumia akili za kawaida kabisa Profesa Safari yuko sahii kabisa!! Haitaji kuwa umemaliza elimu ya chuo kikuu kuelewa mantiki ya wote wanaoshabikia kwamba chadema wamemkosea heshima na mambo mengine kama hayo....huyo mama amejikosea heshima mwenyewe kwa kitendo chake cha kufanya mambo yake ya hovyo adharani!!
 
Tbs hawa wapuuzi sana hasa mijitu kama Marini Hassani na mkurugenzi wake wanakera sana mwisho wao waja watalia na kusaga meno vitambi hivyo walivyo navyo vitawaisha sas watake wasitake CDM itakuwa moto kwao.
 
Yani Mungu akupe maisha marefu,magamba evry time udini..magamba yamewashinda mnaanza kutumia masaburi..wel done prof,,
 
Please we need to prevent the incidence of discriminatory stereo types, we need to come together and get rid of this kind of hate speeches.

As you know Tribes were there before all this kind of religions... so we need to be very careful...

As you know religious identity is not as strong as tribal identity, so if we started regime of addressing a religion rights to the country which has a tribal identity more linear than religions.

This will lead to genocide, discrimination, prejudice, cleansing this has been increased all over the world

We have just enough religion to make us hate, but not enough to make us love one another.
Ignorance and intolerance are the major cause.
We all have equal access to all institutions in TZ why Muslims are causing this kind of discrimination?
We need to get rid of this polarizing politicians who caused immense problems they only mind and think about their elections
Hate Means of expressions and crying that Muslim are the one who have been oppressed for 50yrs there were no rights for Muslim the mind set.
Let us work hand in hand to promote harmony!!!

Why blaming muslims (the affected) and not the one who causes

Blame chadema for insulting muslim identity and propagates hates based on religion
 
CdM,cUf, sAu nk hawapigi mziki sana ndo maana tunawawekea watz 'show' la nguvu kutoka ccM na ndio watz wengi wanapenda hasa show bure.
Mkipiga mziki tutawarusha hewani. Ila mkibaki na SEra tu, hatuna muda huo.....
 
namimi niungane nawengine kukupongeza prof! maanayake ule mjadala wa bakwata kunawatu wanaukomalia sana! safi kwakutoa elimu ya bure kwa bakwata! na wote wenye mawazo mgando kama hao!

mimi nashangaa eti unampongeza prof huyo anatafuta sifa za binadamu na kesho lazima ataulizwa kwa mungu shida ni kwamba prof ana jicho moja kama fundi saa (one eyed men) kafumbua macho kaona dunia ni bora kuliko maisha milele na dr slaa alimleta cdm kwaajili ya kupambana na uislam lakini hawezi yeye wala huyo mwanazuoni uchwara yeye hapo cdm nikama karai la kubebea zege kazi ikiisha linatupwa
 
Viongozi wa dini ya kiislamu kupitia taasisi mbili zilizotajwa hapo juu wameonyesha kukerwa na kitendo cha DC 'kuvuliwa sijui ni jalabibu ama ni mtandio katika kichwa cha mama wa kiislamu'. Hata mimi katika mazingira ya kawaida ningekerwa na tabia ya makamanda wale na naamini ingekuwa hivyo kwa kila mtu na viongozi wangu wa CDM ambao hujali sana mambo ya kijamii wangekuwa wa kwanza kuomba msamaha kwa niaba ya Chama.

Lakini katika hili naomba nitofautiane na viongozi wangu watukufu wa taasisi tajwa hapo juu. Kimsingi sasa hivi Igunga is political battle ground na mahala popote ambapo kuna mpambano waina yoyote sheria za kawaida huwa hazitawali bali kunakuwapo na sheria na taratibu ambazo zinaelekeza namna bora ya kutekeleza majukumu yetu.

Mkuu wa wilaya ya Igunga saa na wakati ule alikuwa ni mhalifu wa kijamii na alipaswa kushughulikiwa kwa namna ileile ya kiuhalifu. Bahati mbaya imetokea mama huyu aliyetakiwa kusimamia mpambano wa kisiasa wa vyama vya siasa, aliamua kuvaa daruga na kuingia uwanjani bila ya kibali na ruhusa ya refa na akaingilia upande wa goli la upinzani shughuli aliyopata anaijua mwenyewe na wapambe wake.

kujaribu kuingiza hoja ya uislamu kwa mama huyu ambaye alikuwa anavunja kanuni ya msingi ya kutoa haki haijarishi ni padri au sheik, au sista au mama wa kiislamu ni lazima ashughulikiwe kwa lugha ya kisiasa `ambayo ataielewa vizuri.

Kuvaa baibui, hijabu au kanzu, au nguo za usista na upadri ukaende kutenda ushetani utashughulikiwa kwa hasira za kishetani.Chadema walijitahidi kuzungumza lugha ambayo CCM na mama yule na mwajiri wake wangeielewa. Ni bahati mbaya kuwa tendo la muovu huyu limewafika vipofu wa maadili na sasa wamelivalia kanzu na kulibeba eti ni kukashifu uisilamu.

Ebu tumwogope Mungu, na tutende haki kwa kuzingatia imani zetu.CCM iliyopoteza dira inatupeleka pabaya inahubiri Tanzania isiyo na dini halafu inatugawa katika misingi ya imani zetu. Watanzania tumefika pahala pabaya ambapo mwizi anaulizwa dini yake kwanza na kama nikigundua ni mkrito mwenzangu nasema eti si mwizi, ukijua ni mwislamu unasema wanamuonea eti kwa sababu ya dini yake, jamani tunakwenda wapi? Jalabibu na uhalifu wa kisiasa vinahusiana nini? Uhalifu na imani vinahusiana namna gani?

Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padre aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusianao

...mkuu umenena yaliyo-ya-kweli,na ninaunga mkono hoja.Labda niongeze kidogo,naomba ndugu zangu ktk iman mniwie-radha kama haya ntakayo-uliza yatawakwaza.JE kuna haja gani basi ya kungangania usiku na mchana kutaka tuwe na mahakama ya kadhi wakati mtu akishavaa "hijabu" tu hawezi kufanya kosa?,kwa mantiki hiyo hamuona kama hiyo mahakama ya kadhi uenda ikakosa kazi kama waumin wote wataamua kuvaa "hijabu??"...tufundishen njia hiliyo sahihi ya kumwabudu Mwenyezi Mungu,achen hizo proganda mbaya na hatari za CCM nukta
 
Wewe Prof. Abdallah Safari unaimbishiwa wimbo ambao hujui umeanzia wapi?

Utatumika na hao jamaa kama mwavuli kudhalilisha dini yako ukiiisha wanakutupa!

Ukitaka ku-proove gombea uongozi wa juu uone mziki wake

Hutakuwa Prof. wa ukweli tena utakuwa profesa njaa..pole sana

watch out ..we are watch the movie..jitambue

Topical, correct english: we are watching the movie...

Mtu mzima mwenye hadhi ya uprof na mwanazuoni anapoongea anaelewa impact na magnitude ya maneno yake

Just let him be! Haya mambo ya kuviziana kwenye dini yatatupeleka pabaya sana ndugu zangu
 
ulitegemea aongee tofauti na hicho, angekula wapi na hiyo njaa yake!?
leo anaonekana msomi wa kweli baada ya kwenda kinyume na bakwata na wanazuoni, lol

Kwa hiyo unataka kumvua uanazuoni na uprofesa wake kwa ajili ya kimtandio cha yule DC? Nyie mbona mnashindwa kufikilia kwa umakini jama
 
CCM wanataka kutumia upenyo wa dini kuwin CDM
Mimi nilidhani ni kuangalia why alivuliwa hijab kama ni kweli
You mean ata mtu akishikwa katika purukushani za ugoni nayo mtalalamika why amevuliwa au imevuka!
Kwanza hamkutakiwa ata kucomment on the Hijab thing ni kujishushia hadhi hasa maakama kama itaprove kuwa yuko guilt ingawa kwa mahakama za CCM ni ngumu kidogo
 
Back
Top Bottom