Prof. Safari ajiunga CHADEMA; akabidhiwa kadi rasmi leo

Amtake nani huyo mchovu, mnafiki na mpenda madaraka.

Amechooooka sanaaa kimaisha hana jipya zaidi ya kuwa yes yes apate ugali wake.

Kama nchi hii mtu mwenye hadhi ya Uprofesa anachoka, basi hakuna haja ya kusomesha watoto wetu.
 
Wanasema ktk makongamano yao eti chama cha kanisa katoliki. sasa labda chadema walitumia kujaribu kupunguza hasira hizo

"Makongamano yao" akina nani? Ningewaomba tusichanganye mambo mpaka tukachanganyana wenyewe. Issue iliyopo hapa inaweza kuhusu vyama vya siasa viwili au na mtu mmoja. Inakihusu chama cha CUF ambacho Profesa alikuwa mwanachama wake awali. Chama cha Chadema ambako ndiko alikohamia na mwisho ni Profesa mwenyewe ambae ndio mhusika. Sijua hayo makongamano yao unakusudia wao akina nani wanaosema chama gani ni cha wakatoliki.

Mbona suala la Profesa Safari kuhamia Chadema tunalikuza namna hii. After all, Profesa Safari hakuwa na wadhifa wowote mkubwa katika chama chake cha mwanzo CUF kiasia cha wachangiaji kumganda namna hiyo. Pia sio mtu wa kwanza kuhama CUF kwenda vyama vingine wala mtu wa kwanza kuhamia Chadema toka chama kingine. CUF waliwahi kuwapoteza watu maalufu na wenye nafasi kubwa katika chama chao kama Tambwe Hiza, kuna mmoja alikuwa mbunge machachali Zanzibar jina lake limenitoka, kuna mama Jidawi, kutaja baadhi yao. Hawa walikuwa ni mihimili katika CUF. Wapo pia watu wazito katika siasa waliopata kuhamia Chadema kutoka vyama vingine bila kuwasahau Mabere Marando, Shibuda nk. Wapo pia wazito waliowahi kuhama CHADEMA bila kumsahau DR WARID KABOUR aliyekuwa mmoja kati ya viongozi waandamizi wa Chadema. Yupo mkongwe Mrema aliyehama CCM akiwa katika nafasi ya Uwaziri, akahama NCCR Mageuzi na kuhamia TLP hali akiwa ameshashika nafasi ya Uenyekiti. Sasa kuna muujiza gani Prof Safari kuhamia Chadema.
 
nyinyi mnakula jasho letu, lkn wagumu mali hiyo hiyo kuliwa na downs. ndio maana mimi sipingi kulipwa downs. kwani hata nyinyi mnakula kwa mlango wa nyuma
Mhadhiri kama kweli una nia ya kutetea waislam na sio CCM, hebu kuwa siriaz kidogo. Taja kwa mifano hai na sio ya kusadikika, namna ambavyo muisalmu yeyote anakandamizwa na mkristo...
Nitaomba utaje kwa kifupi na kwa kueleweka vizuri (precise and claer), maana binafsi naona tu wimbo waislamu wanabaguliwa ndiyo maana Nyerere alifanya hivi, alifanya vile. Ndo maana mauaji ya mwembe chai.. Ok, naomba unitajie leo hii, haki au raslimali anayopewa mkristo, na ananyimwa muislamu kwa sababu ya dini yake.
 
Kaka mimi ni muislam na sikubali nipelekeshe kijinga kama baadhi ya waislamu wenzangu, Mfano Sheikh wetu Simba sijui anaongoza waislamu au anatetea ufisadi. Kwangu mimi namuona kama Mnafiki tu huyo Sheikh Simba kuwakingia vifua wakina Kikwete kuzitafuna rasilimali zetu kwa huku wakitumbandikizia mbegu za chuki ya udini ili sisi Watanzania tuchukiane na wao wakifaidi matunda ya hii nchi bila ya sisi kuyafaidi. Kaka inaelekea wewe umenizidi uislam, msimamo wako ni mbaya, nyie ndio mnaoshabikia wakian Omasa Bin Laden. Mungu amesema tuipiganie dini yake lakini sio kwa kupigania kiunafiki kama wewe na Sheikh Simba wanavyopigania, nyi msimamo wenu ni mkali na siko tayari kujiunga na Mujaheedina. Suala la kuwabagua Watanzania wezangu ambao natofautiana dini sikubaliani nalo kabisaaa inaelekea Fisadi Kikwete anakutumieni kuiharibu Dini ya Uislam hapa Tanzania na ndio maana tunaonekana waislamu wote wajinga kutokana na nyie wachache mnaotumiwa na Mafisadi kupandikiza mbegu za udini kwa wasilamu ili tuwachukie Watanzania wenzetu (Wakristo)

Bila kujali kama wewe ni muislamu au dini gani, ningekushauri ujiepushe na kutoa hukumu kama hizo kwa viongozi wetu wa dini bila kujali kama ni viongozi wa dini ya kiislamu wala kikristo. Kama hayo unayoyahukumu juu ya kiongozi wa waislamu ni sahihi mahali sahihi pa kuyasemea sio katika forum hii bali kwenye forum za dini husika. Prosesa Safari hakuingia Chadema kwa kuwa kiongozi wa dini yake ni mnafiki au anamuunga mkono Kikwete kama ulivyosema bali ameingia kwa sababu za kisiasa.

Tusitafute kuwagawa wana forum kwa misingi ya kidini bila sababu.
 
Anakaribishwa, ila tpe kama za akina Shibuda hatuzhitaji, Mungu ibariki chadema na viongozi wake wape hekima na utaishia wa kuwaongoza watanzania.

Unamaanisha nini unaposema "types za akina Shibuda?". Uwingi katika tungo yako "hutuzitaki" unamuwakilisha nani ukiondoa wewe mwenyewe? Sidhani kama utakuwa unamaanisha wanachadema au viongozi wa Chadema ambao ndio wana uwezo wa kumtaka au kutomtaka Shibuda katika chama. Maana, kama wasingemtaka wasingempokea na kumpa nafasi ya kukombea na hatimaye kushinda kiti cha ubunge katika jimbo kongwe na lenye heshima kama MASWA. Itakumbukwa kwamba kuingia kwa SHIBUDA katika CHADEMA kumechanguia kwa asilimia zaidi ya sabini kwa chadema kuzoa viti vitatu katika Mkoa mpya wa Shimiyu. Bila shaka ni kwa kuzingatia hilo ndio maana CHADEMA hivi karibuni imemteuwa kuwa mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga. Mimi ningeshauri tujiepushe kutaja majina ya watu kwa tuhuma tusizokuwa na takwimu nazo bila sababu. Tutakuwa hatuwatendei haki ikizingatiwa kwamba hatuna uhakika kama nao ni wanachama wa Jamii Forum au la.
 
Back
Top Bottom