Prof. Ndalichako: Kiama kinakuja wanaotumia vyeti feki makazini

Ni vema ila ajiandae kwa yote yatakayomkuta. Ametangaza vita kubwa ndani ya nchi. Ni tofauti sana na suala la watumishi hewa. Kwani hili linawahusu mpaka watekelezaji wa zoezi lenyewe.
 
Hawa sampuli za kina Ndalichako ndiyo walioiuwa elimu ya Tanzania mpaka imefikia watu wana foji hovyo vyeti kwa kuwa kwa sasa hakuna tofauti ya msomi mwenye pHd ya halali na asiye msomi mwenye pHd feki.

Wote sawa tu.

Tazama Rais wetu Magufuli, ana phd lakini kutamka Kiswahili cha ufasaha shida, Kingereza ndiyo usiseme.

Haki ya Mungu, nilipewa kazi ya ku assess applicants kwenye shirika fulani basi watu wana Masters Degree walishindwa kujibu barua simple za kibiashara mpaka nilishangaa.

Wafumue mfumo wote wa elimu na waturudishie mfumo tuliokuwa nao kabla ya azimio la Arusha. Ndiyo suluhisho pekee la kuwa na wasomi makini miaka 20 ijayo. Bila hivyo tutaendelea kuwa vihiyo kwa miaka mingi ijayo na wafanyakazi wa kutoka hata nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki zinazotuzunguka wataendelea kuonekana bora zaidi yetu.

Wawawache waliokuwepo mpaka watakapofanya madudu watakuwa wamejitumbuwa weenyewe na wadhibiti wote wapya wasiwepo hao feki la sivyo watatumbuliwa zaidi ya nusu hususan serikalini.
 
HILI suala la VYETI FEKI llnahusu vyeti vipi? vya primary,sekondari(f4 na f6)au vya chuo/chuo kikuu?.Ni uchunguzi gani utatumika kubaini kama cheti ni halali lakini mmiliki si mwenyewe?Sasa kama kweli hili zoezi likifanyika katika sekta zote ni sawa na kufunua misukule iliyotulia huko ilipo kuja duniani kusumbua watu.Maana hili zoezi litaishangaza dunia kuliko la wafanyakazi hewa,Kama hakuna namna ya kuficha aibu lifanyike tu haraka muda huu wa kutumbua majipu,Hapo patakuwa na shughuli pevu kama hapatakuwa na watu wa kuziba nafasi zitakazoachwa wazi na hao watakaotumbuliwa kwa vyeti feki.
Kama hizo nafasi watataka zizibwe kiundugu sawa!! Ila kama bi kwa haku mbona wenye vyeti halali wapo wengi mtaani
 
Hawa sampuli za kina Ndalichako ndiyo walioiuwa elimu ya Tanzania mpaka imefikia watu wana foji hovyo vyeti kwa kuwa kwa sasa hakuna tofauti ya msomi mwenye pHd ya halali na asiye msomi mwenye pHd feki.

Wote sawa tu.

Tazama Rais wetu Magufuli, ana phd lakini kutamka Kiswahili cha ufasaha shida, Kingereza ndiyo usiseme.

Haki ya Mungu, nilipewa kazi ya ku assess applicants kwenye shirika fulani basi watu wana Masters Degree walishindwa kujibu barua simple za kibiashara mpaka nilishangaa.

Wafumue mfumo wote wa elimu na waturudishie mfumo tuliokuwa nao kabla ya azimio la Arusha. Ndiyo suluhisho pekee la kuwa na wasomi makini miaka 20 ijayo. Bila hivyo tutaendelea kuwa vihiyo kwa miaka mingi ijayo na wafanyakazi wa kutoka hata nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki zinazotuzunguka wataendelea kuonekana bora zaidi yetu.

Wawawache waliokuwepo mpaka watakapofanya madudu watakuwa wamejitumbuwa weenyewe na wadhibiti wote wapya wasiwepo hao feki la sivyo watatumbuliwa zaidi ya nusu hususan serikalini.
Hivi ile broken ya hatari aliyoimwaga mkwere wakati wa ujio wa obama umeisahau ? Lakini nasikia jamaa ni professor
 
Safi sana manyumbu yaondoke ofisini..

Unakuta jitu linajiita msomi alafu eti linatoa maoni kuwa Magufuli hatakiwi kuwa rais anatakiwa awe chini ya MTU!!!!

Haya ndio yenye vyeti feki
 
Hili zoezi lianzie na vyeti vya primary kujiridhisha,waje kwenye hivyo vya sekondari hapo ndiyo kwenye kitovu hasa,pia waende kwenye shule kupekua adm reg na huko NECTA kuona kama kuna kumbukumbu.
 
Loth inaonekana wewe ni mtoto wa juzi,unafahamu vyeti vya primary vimeanza tolewa lini?
Fanya tafiti kabla ya kuja hapa.
 
Kelele nyingi ni juu ya vyeti feki serikalini lakini naomba nikumbushe pia kuna hili swala la watu kufoji vyeti vya kuzaliwa kwa lengo la kukwepa kustaafu mapema.Yaani wanataka waendelee kuwepo kwenye utumishi wa umma hata baada ya kufikisha miaka 60.

Wengi wanafanya hivi kwasababu mbalimbali kama vile tamaa,kuajiriwa huku umri ukiwa umeenda,kupenda madaraka n.k.Hivyo serikali ifuatilie swala hili ili kuwabaini watu hawa.

Taratibu za kusajili vizazi nazo zitazamwe upya maana huenda kuna mianya ya watu kudanya umri na wakabaki salama.
 
ni wazo zuri tatizo ni nani anauthubutu huo? Anaetakiwa kukagua mwenyewe unawezakuta alifoji umri. MCHIMBA SHIMO ANAWEZA DUMBUKIA MWENYEWE. ACHA NIISHIE HAPA CYBER ACT ISIJENIZOA
 
Hili zoezi ni gumu linaweza kuvuruga mambo.Ni bora kuimarisha stadi za maarifa na ujuzi wa watu walio nao kuliko kupekua mambo yaliyotulia.Kazi zinafanywa na watu.Dunia itashangaa mambo yakifunuliwa bila kutumia hekima na busara.Nini kilisababisha kukawa na ufoji wa vyeti?,hapo ndiyo pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom