Prof. Ndalichako: Kiama kinakuja wanaotumia vyeti feki makazini

ZOEZI LA KIHISTORIA HILI NDIO KIPIMO CHA SEREKALI YETU WATUMBULIWE TU.
Tupo pamoja sn maana wanaostahili kuwepo kazini kwa taaluma waliyonayo wapo mitaani na wenye vyeti vya taaluma feki wapo kazini wanakula mishahara isiyowahusu.
 
Wote hao mtakwenda, huwezi kuchakachua form 4 ukaenda 6 then chuo ukadhani utasalimika hakuna mpaka vyeti vyoote viwe sahihi
 
Hana jipya huyu, si alikuwa hapo hapo wanapotoa vyeti feki akatowa matokeo feki.

Hatujasahau.
Una akili sana we Bi mkubwa vyeti fake vingi ni form four na form six na alikua mtendaji mkuu wa baraza alishindwa vipi kuvizuia kipindi chake?
 
Hii ni safi sana.Big up Dr.Tulipigia kelele sana jambo hili lakini hatukusikilizwa.Baada ya zoezi hili au hata sambamba kama tuko serious kuboresha elimu, turudishe mitaala yote ya before UPE.Ukweli ni kwamba elimu ilianza kuharibika with UPE(Universal Primary Education).It's common sense kwamba haiwezekani darasa la saba akamfundisha darasa la saba mwenzie au Form Four failure akafundisha mtu akafaulu wakati yeye mwenyewe kafeli.

Ni ukweli ulio wazi kwamba waalimu wengi ni duni sana.
Akihitimisha leo bajeti yake ya wizara ya Elimu,sayansi,teknolojia na ufundi.Waziri huyo anayeonekana ana nia ya dhati kufufua sekta ya Elimu ambayo ilikua mahututi,amewaasa wale wote waliopo makazini kwamba,"kwa kulinda heshima zao wao wenyewe wajiweke pembeni kwani atahakikisha anawasaka popote pale".

Pia amegusia pia kwamba kuna hadi wabunge wenye vyeti feki ambapo amewatahadharisha nao kwamba hawatasalimika kwani wao ndio wanatakiwa kuwa mfano.
 
Kama cha form four ni fake lkn six na degree ni halali hapo inakuwaje?
Hapo sasa! Lakini dada Joy ni mwana Hisabati. Anaweza sema sema kuwa kosa moja linafanya mengine kuwa feki pia. Kinachoangaliwa ni "uharamu" wa mwanzo (cheti cha kidato cha Nne). LUKU vi..Naa Gu(a) kazi kwao....
 
Mkuu kama siasa haitaingizwa kwenye elimu mana ndio iliyotufikisha hapa,huyu mama anaweza akawa mwarobaini wa elimu yetu.Inaonekana si mwanasiasa, labda wamfundishe.Hii sekta ilikua yatima muda mrefu lakini dawa yake pengine inaweza ikawa imepatikana.Hebu tuweke akiba ya maneno.
Ningependa akisome kwa makini kitabu cha Msemakweli. Kuna kaorodha fulani humo. Mh. Waziri aanziage hapo....
 
Back
Top Bottom