Prof. Muhongo anafaa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania!

Ndugu zangu hawa wanasiasa huwa hawatabiriki.
Watu walikuwa na imani sana na 'mtoto wa mkulima' Pinda lakini mwisho wa siku amekuwa hopeless.

Siwezi kataa kama kulikuwa na watu waliokuwa na imani na mwana wa mkulima. Mimi si mmoja wao kama wapo. Kama unakumbuka vyema huyu bwana kwenye hotuba yake ya kwanza kabisa kati ya maneno yaliyonishtua ni kukiri kuwa hakuwa na imani kama viatu vya mtangulizi wake yaani EL vingemtosha kwani vilikuwa vikubwa mno. Hapo tayari alishakiri kuwa hawezi. Alikiri pia ndani ya muda mfupi uliofuatia kuwa mafisadi wana nguvu sana na hawawezekani. Those were weaknesses ambazo zilikuwa zinaonekana wazi. Huyu huyu pia aliwahi kukemea matumizi ya mashangingi na bado yakawapo na yeye akiwa kiranja mkuu. Hajawahi kufanya kitu chochote cha kukumbukwa kama shujaa. Hana ishu wala hajawahi kuwa nayo.
 
Back
Top Bottom