Prof. Muhongo anafaa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania!

ngoja aingizwe kwenye circles za bakshihi utasahau kabisa kama ndiye huyu....
 
Tatizo letu watz tunakuwa wepesi sana wa kuamini mtu kwa kajitu kamoja tu alikofanya, tumpe mda tuone kama tatizo la umeme litaisha, kumbukeni hawezi kuwa msafi ndani ya wachafu so let us see how things goes
 
What a good CV...but kasi aliyonayo atafika nayo? pengine mkomboz wa hii nchi haiko chin ya viongoz saiz....tunatakiwa wanachi tuamue uozo huu ili tubadri mfumo mzma
 
Cku moja tu unamteua m2 kua PM? ulimuona lakn be Kiroboto alivyokua akimwangali? najua baada ya kikao alimuita na kumuuonya..."hatuendu hivyo punguza ukali na ucweke mambo nje kiasi hicho" unajua kwa nn kamtetea Maswi..katibu wa wizara kuhusu PUMA aka BP?
 
Katiba yetu inataka ili mtu ateuliwe kuwa waziri katikia Serikali ni lazima awe mbunge, aidha Katiba hiyo inampa Rais madaraka makubwa ya kuteua watu kuwa wenyeviti wa bodi mbali mbali za mashirika ya umma, na mawaziri kuteua wajumbe wa bodi hizo. Wakati anahitimisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Waziri wa Wizara hiyo aliyeteuliwa hivi karibuni kufuatia Raisi kul;azimika kuvunja Baraza la Mawaziri Mhe Prof Sospeter Muhongo alitamka kuwa japokuwa Katiba inampatia madaraka ya kuteua wajumbe wa bodi ya Tanesco; utaratibu atakaoutumia katika kuteua wajumbe wapya wa bodi ya Tanesco ni kwa kutangaza nafasi katiika vyombo vya habari ili wale wanaofikiri wana sifa wajitokeze kuomba kushindanishwa. Alisema kuwa alifanya hivyo hivyo kwa Bodi ya TPDC, na ndio utaratibu atakaoutumia katika siku za usoni.

Kikubwa aliuponda utaratibu ambao umezoeleka hapa nchini wa "mawaziri kujifungia chumbani na kuteua marafiki zao kuwa wajumbe wa bodi za mashirika mbali mbali ya umma". Wakati akitamka maneno haya Prof hakuuma maneno wala kusita na hakujali kuwa mpaka sasa mawaziri ambao wamekuwa wakiwateua wajumbe wa bodi za mashirika ya umma tokea nchi hii ipate uhuru ni kutoka TANU na CCM, na hivi sasa hata yeye pia anatumika Serikali ya CCM. Ujasiri huu wa kusimamia ukweli unatokana na kuwa Yeye hajawahi kuomba nafasi yoyote ya kisiasa hivyo anatumiaka nafasai aliyonayo kitaalamu ila mfumo wa nchi yetu yaani Katiba ndio ina mapungufu ya kuigeuz anafasi ya uwaziri ya kisiasa

Ujasiri aliuonyesha Prof S Muhongo ni uthibitisho kuwa harakati za upinzani kuwarejeshea watanzania uhuru wao kamili uliokuwa umehodhiwa na wajanjja wachache ndani ya CCM zinafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa wataalamu kuanza kuteuliwa kuongoza Serikali badala ya uteuzi huo kuzingatia ukereketwa wao kwa CCM. Kazi tuliyonayo watanzania ni kuhakikisha katika Katiba Mpya Mawaziri wasilazimike kuwa wabunge ili Bunge na Serikali ziweze kuwa ni asasi mbili tofauti kiutendaji tofauti na hali ilivyo sasa ambapo kuna mwingiliano mkubwa unaofifisha utendaji na utaratibu wa wazi zaidi utumika katika kuwapata wajumbe wa bodi mbali mbali
za mashirika ya umma.
 
Kwa maoni yangu bado ni mapema mno kuweza kufikia hitimisho la kipi tulichojifunza katika ujasiri wa huyu Prof. S. Muhongo, labda miezi sita ijayo tutakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kufanya hivyo.
 
Pinda hana kitu ambacho kalifanyia Taifa. liwalo na liwe umapwaya sana... waziri miezi3 anakuzidi?
 
So far, ameonyesha mwanga mzuri. Binafsi amenivutia sana, akiendelea hivyo hakika atakuwa mtu ambaye namfurahia katika duru ya uongozi. Lakini kwa kipindi hiki kifupi nimefurahishwa sana na kupungua kwa gharama za kuunganishiwa umeme pamoja na kupungua kwa bei ya nguzo na utapeli mwingi ambao ulikuwa unafanywa na kumwumiza mlalahoi.
 
zamani watu wa Mara kama Wakurya walikuwa watu wa misimamo sana piga ua- wakisema no ni no! Maana wana pride sana na utu wao. Nimemsikiliza huyu Prof. nikagundua kuwa yuko proud in a positive way na anajiamini sana. Swali ni je atapata ushirikiano wa mapambano yake dhidi ya wezi?

Pili si formula kuwa wasomi wote si viongozi wazuri kama vile ambavyo pia si formula kuwa wasiosoma sana lazima wawe viongozi wazuri. Hata sasa tunaweza kuona utofauti wake na Maprof. wengine.
 
1. Unaweza kukataa ufisadi na ukapambana nao no matter what?

2. Si kweli kwamba wasomi wote ni wabovu katika uongozi. Wanaweza kuwa wabovu katika siasa!

3. Hakuna haja ya kulialia ukipewa madaraka na Rais unaweza kumsaidia kusafisha uovu na kuwakumbuka wananchi ambao ndio wenye mamlaka
 
Hapana. kuongelea nafasi za kisiasa sidhani sana kama huyu yuko ki-hivyo.

Isipokuwa kitu kimoja ambacho tumeambiwa ni kuwa hata huko alikotoka Mara (sijui sehemu) alilelewa katika misingi ya kukaba hadi golini inapokuja suala la kudai haki.

Wana-Saikolojia wamegundua kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya makuzi ya mtu na maisha yake. Huyu Msomi ni strict usiambiwe yaani hata kwa watoto wake. Halafu hata pale Geology dept UD alijulikana pia kuwa ni mtu wa kutotaka mambo ya kiswahili-swahili au blabla katika mitihani na kufundisha na hili Manaibu zake nao wamelisema leo kuwa ni mtu wa speed na kutaka vitu vya uhakika. Swali je mifumo wa nchi utamsaidia kuendeleza hayo mapambano???????
 
Wakati umefika wa kuwa wazi katika maamuzi magumu ikiwezekana yawe ya kidikteta ili ule udhaifu unaosemwasemwa ukomeshwe mara moja.KIUKWELI MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAWEZEKANA TU PALE MAMLAKA NA TAASISI ZILIZOPO KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO PASIPO KUOGOPA NANI WALA NINI NA HAPO NDIPO HATA SISI WANANCHI HUKU TUTAIGA MFANO ULIO BORA NASI KUTIMIZA WAJIBU WETU WA KUJENGA TAIFA.MAMLAKA/SEKTA HIZI ZISIPOFANYA/KUWA WAZI NI DHAILI KABISA TUTAYUMBAMYUMBA NA KURUDIARUDIA YALE YALE YASIO NA TIJA KWA TAIFA NA BADALA YAKE ZITAONEKANA KAMA WASALITI WAKUBWA KWA WANANCHI.HONGERA PROF. KWA UJASIRI HUO NA UENDELEE NAO IPO SIKU MWENYEZI MUNGU ATAKULIPIA HAKI YAKO YA UTUMISHI WA UKWELI,ILA HII ISIWE NI CHANGA LA MACHO/SPEED TU YA KUFIKA KILELENI ALAFU UNATUPUNGIA MKONO NA KUZAMA KATIKA MMOMONYOKO WA MAADILI YA UONGOZI KAMA YA WALE WALIOKUTANGULIA,TUNZA HESHIMA YAKO YA U-PROF. ILI MAPROF.WENZAKO WAOGA WAIGE MFANO HUO,ASANTE.
 
Wakati umefika wa kuwa wazi katika maamuzi magumu ikiwezekana yawe ya kidikteta ili ule udhaifu unaosemwasemwa ukomeshwe mara moja.KIUKWELI MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAWEZEKANA TU PALE MAMLAKA NA TAASISI ZILIZOPO KUTIMIZA WAJIBU WAO IPASAVYO PASIPO KUOGOPA NANI WALA NINI NA HAPO NDIPO HATA SISI WANANCHI HUKU TUTAIGA MFANO ULIO BORA NASI KUTIMIZA WAJIBU WETU WA KUJENGA TAIFA.MAMLAKA/SEKTA HIZI ZISIPOFANYA/KUWA WAZI NI DHAILI KABISA TUTAYUMBAMYUMBA NA KURUDIARUDIA YALE YALE YASIO NA TIJA KWA TAIFA NA BADALA YAKE ZITAONEKANA KAMA WASALITI WAKUBWA KWA WANANCHI.HONGERA PROF. KWA UJASIRI HUO NA UENDELEE NAO IPO SIKU MWENYEZI MUNGU ATAKULIPIA HAKI YAKO YA UTUMISHI WA UKWELI,ILA HII ISIWE NI CHANGA LA MACHO/SPEED TU YA KUFIKA KILELENI ALAFU UNATUPUNGIA MKONO NA KUZAMA KATIKA MMOMONYOKO WA MAADILI YA UONGOZI KAMA YA WALE WALIOKUTANGULIA,TUNZA HESHIMA YAKO YA U-PROF. ILI MAPROF.WENZAKO WAOGA WAIGE MFANO HUO,ASANTE.
 
CV na utendaji ni vitu viwili tofauti anyway tumpe muda tutaona... cv ya Omary Nundu unaijua? performence yake vipi?
 
Back
Top Bottom