Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,879
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Mhongo amesema kamwe hatafuata ushauri unaohusu gas kwa watu ambao wamehudhuria mafunzo ya wiki moja ya gas na kupata cheti cha mahudhurio 'certificate of attendance' na amekemea tabia ya watu hao kujifanya wanajua sana masuala ya gas kuliko wataalam wenyewe.
Binafsi hili nimeona kama ni dongo kwa ZZK ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akikosoa utendaji kazi wa Prof Mhongo hasa kuhusiana na sector hii ya gas.
Zitto amewahi kujinasibu kwamba yeye si mtaalam wa madini na gas lakini akasema, namnukuu,
Nimuombe Mheshimiwa waziri si kila ushauri unaotolewa na mtu ambaye si mtaalam wa sector husika basi si mzuri, namuomba aache kurusha madongo kwa watu wanaomkosoa, kiongozi asiyetaka kukosolewa hafai kuwa kiongozi.
Naomba ofisi ya wizara ya nishati na madini isikufanye ujisahau sasa, chukua kukosolewa kama ni challenges za wewe kufanya vizuri. Kama huelewani na ZZK kama mtu lakini chukua ushauri wake.
Sidhani kama Prof. Muhongo alikuwa ananipiga madongo mimi maana mimi sina certificate yeyote ya Oil and Gas. Atakuwa anawasema watu wa CSOs.
Nikiwa Mbunge kazi yangu ni kuisimamia serikali. Sitoi ushauri kwa waziri yeyote yule. Ninatoa hoja kwa mwono mbadala. Waziri ana hiari ya kuchukua hoja zetu kama upinzani au hapana maana sisi tukishika dola tutazitekeleza sera zetu.
Waziri aendelee na juhudi zake za kuhakikisha hakuna mgawo wa umeme nchini na kwamba wananchi wengi zaidi vijijini wanapata umeme kutoka 14%
Ya sasa mpaka 30% waliyoahidi kwenye ilani ya chama chao.
Ikumbukwe tu kwamba huyu ni Waziri wa CCM na tutamhukumu kama mwana CCM mwingine yeyote yule.
Nikiwa Waziri kivuli wa Fedha na uchumi na kwa kutumia taaluma yangu ya Uchumi, Uchumi Biashara (international trade) na Uchumi Madini (mineral economics) nitaendelea kusimamia sera za chama changu cha CHADEMA kwamba rasilimali za nchi lazima zifaidishe wananchi.
Tulisimamia suala la mikataba ya madini wakati wataalamu wa miamba wakiwa kimya na wengine wakiwa ma consultant wa hayo makampuni ya madini na tukafanikiwa kutunga sheria mpya ya madini.
Tumesimamia suala la kuandikwa kwa sera ya gesi kabla Prof. Muhongo hajawa Waziri na tutaendelea kusimamia mpaka tupate sera nzuri itakayojali maslahi ya nchi yetu.
Tutaendelea kukataa uchimbaji wa Uranium mpaka hapo tutakapojiridhisha kwamba usalama wa wananchi wetu umezingatiwa na makampuni ya utafutaji na uchimbaji yanalipa kodi inavyostahili.