Prof. Muhongo ammaliza rasmi Mhando; Mama Rwakatare naye alipuliwa!

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Sijawahi ona ktk kumbukumbu zangu za viongozi wa CCM mtu BOLD na muwazi kama huyu.

Kunaonekana nuru kuhusu suala la Umeme TZ amesema muhando na mkewe na watoto wake wawili walikuwa na kampuni iliyoanza kwa Tshs 10mil. the after 8 months ikapewa tenda ya Tshs mil 850.

Amesema waliagiza spea ila sanduku lililokuja likawa la Misumari. Hv hii nchi inakwenda wapi?

Mama Rwakatare naye atajwa wizi wa umeme wa zaidi ya mil 10
Amesema kuwa St Mary Secondary Schools za Mheshimiwa Rev Rwakatare ni mojawapo wa wezi wa umeme wa Tanesco, wameiba jumla ya Tshs millioni 10 plus.

Shame on you Mheshimiwa Rev Rwakatare.
 
St.marys in,ternational school milion 10.5
acsses bank.. Million 13
sharif co. Million 25.. Amesema wezi hao wamefikishwa kizimbani kujibu mashtaka na tusubiri maamuzi ya mahakama
 
Wakuu,

Waziri wa nishati na madini amewataja wezi wa umeme na miongoni mwao ni St MARRY'S na ACCESS Bank ya Tabata. Duh wahujumu uchumi wako wengi kumbe.
 
Chifu waweza fafanua zaidi kwa sisi tulio mbali na televisheni...asante
 
Inakuwaje shule inayomilikiwa na Mchungaji wanaiba umeme..labda wafanyakazi wameiba umeme bila mmiliki kujua..Ngoja tumsubiri Rwakatare atuambie..maana kwenye mahubiri anakemea wizi sasa inakuwaje ofisi yake inaiba umeme..
 
Sijawahi ona ktk kumbukumbu zangu za viongozi wa CCM mtu BOLD na muwazi kama huyu.

Kunaonekana nuru kuhusu suala la Umeme TZ amesema muhando na mkewe na watoto wake wawili walikuwa na kampuni iliyoanza kwa Tshs 10mil. the after 8 months ikapewa tenda ya Tshs mil 850.

Amesema waliagiza spea ila sanduku lililokuja likawa la Misumari. Hv hii nchi inakwenda wapi?

Mama Rwakatare naye atajwa wizi wa umeme wa mil 10

....................................
Jamani huyu mama si ndo yule Mchungaji wa kanisa kubwa hapa Dar es Salaam..!!??
....................................
 
Waziri wa Nishati na Madini ameitaja shule za st mary's zinazomilikiwa na mchungaji dr mhe. Rwakatare (mbunge), ni miongoni mwa wezi wa umeme wetu. Nimeshangazwa sana na taarifa hii. Kiongozi wa kiroho anadhiriki wizi, tena wa mali ya umma? Isijekuwa hata kanisani kwake tunatumia umeme wa wizi kusifu na kumwabudu Mungu. Nina watoto watatu katika shule hizi, kuanzia leo ninawahamisha. Watanzania, hivi tunakwenda wapi na nchi hii katika hali kama ilivyo sasa? I am so dissapointed! ! ! ! ! !
 
Back
Top Bottom