- Thread starter
- #21
Profesa Mbele: Wengi waanza kutambua ubora wa JK
Binafsi, niliona dalili za ubora wa uongozi wa JK tangu mwanzo, na sijaficha maoni yangu, pamoja na kushambuliwa na wengi, wengine wakidai kuwa nawania cheo katika serikali ya JK. Sijawahi kusikia mambo ya kipuuzi kama hayo, kwani mimi naamini kuwa kazi yangu ya ualimu nilipewa na Muumba, tangu nilipokuwa mtoto mdogo. Sijatetereka na sitatetereka; nina nadhiri ya ualimu.
Kuona mazuri ya JK kama kiongozi, kwa upande wangu, si sawa na kuipigia debe CCM. Tangu CCM ianze, nimekuwa nikiishutumu kwa namna mbali mbali, tena kimaandishi, ili kila mtu asome. Nimechapisha hata kitabu, wiki chache zilizopita, ambamo nimeendelea kuishutumu CCM.
Tatizo la waTanzania wengi ni ufinyu wa mawazo. Kwa vile wamezama mno katika siasa za vyama, wanayachukulia masuala kwa mtazamo wa kichama.
Ukisema hivi, wanaangalia unaunga mkono chama gani. Ukisema vile, wanaangalia kwa mtazamo wa chama fulani. Ukweli ni kuwa mimi si mwanachama wa chama chochote. Nina uhuru wa kusema chochote ninachofikiri, hata kama kinawaudhi watu wa chama fulani. Shauri lao na siasa zao za ufinyu na ukandamizaji wa fikra kwa maslahi ya chama.
Katika makala yangu mojawapo, kuhusu safari za JK nchi za nje, nilisema kuwa JK anafanya juhudi kubwa kama kiongozi wa nchi kuitangaza nchi na kutuwekea mazingira muafaka duniani. Lakini nililalamika pia kuwa waTanzania tunaoishi nje tunamwangusha JK kwa kutofuatilia yale anayoyaanzisha. Nilijenga hoja yangu kwa kutumia mfano wa waTanzania tuliko Marekani.
Ningependa kusisitiza jambo hilo. Wakati huu, wa-Tanzania wanaoishi nje wanapigania sheria ibadilike ili iruhusu uraia wa nchi mbili. Hoja moja ya msingi inayotolewa ni kuwa sheria hiyo ikibadilika, basi wa-Tanzania hao wataleta mitaji sana nchini.
Ninaposikia hoja hiyo, najiuliza masuali kadhaa. Kwanza, narudi kwenye usemi wangu wa namna waTanzania tunaoishi nje tunavyoshindwa kuendeleza yale ambayo JK anaanzisha katika ziara zake. Mianya ya kuwekeza nchini, mianya ya kushirikiana na wawekezaji anaokutana nao huku nje, sisi hatuifuatilii. Je, ni kweli kuwa tuna lengo la kuwekeza sana nchini?
Je, ni kweli kuwa bila uraia wa nchi mbili, inakuwa vigumu kuwekeza nchini? Kama ni hivi, mbona watu baki, wa mataifa mbali mbali, wanazichangamkia fursa zilizopo za uwekezaji nchini? Sheria za Tanzania za sasa zinaturuhusu sisi, na watu hao baki kuwekeza, nao wanachangamkia fursa hizo.
Iwapo kweli wa-Tanzania wanaoishi nje wana mitaji, kwa nini wasichangamkie fursa hizo kama hao wageni? Ni mwekezaji gani ambaye hachangamkii fursa zinapojitokeza? Nina mashaka sana hapo, kuhusiana na kinachosemwa na wa-Tanzania wanaodai uraia wa nchi mbili kwa hoja ya uwekezaji. Huenda kuna haja za kubadili sheria za uraia, lakini inatakiwa wanaopigania suala hilo watoe hoja zenye mantiki zaidi.
Watanzania wanaoishi nje wangekuwa wameonyesha ari ya kuwekeza tangu pale nchi ilipofungua milango, ningeielewa hoja hii vizuri. Hao wa-Tanzania wana ndugu zao nchini, na kwa hivi wangekuwa mstari wa mbele katika kuwekeza. Lakini iweje wanaweka pingamizi, kwamba bila uraia wa nchi mbili, wanashindwa kuleta hiyo mitaji yao? Suali linakuja: je, hao wana mitaji kweli? Je, kuna utafiti upi na takwimu zipi zinazothibitisha kuwepo kwa mitaji hiyo, au ni hadithi ya Abunuwasi?
Nafurahi kuwa kadiri siku zinavyopita, wengi wanaanza kutambua ubora wa JK kama kiongozi. Naamini kuwa kwa mahitaji ya nchi yetu, katika hali tuliyo nayo, tunamhitaji kiongozi wa aina yake, ambaye habagui waTanzania kwa msingi wa vyama, wala hajakatishwa tamaa na wale wanaofanya kila juhudi kutotambua juhudi zake za kuipeleka Tanzania mbele.
Nafahamu kuwa nimechanganya masuala hapo juu, lakini nimefanya hivyo kwa kuona kuwa yana uhusiano fulani muhimu.