Prof. Majimarefu, Nundu wapigwa mweleka

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Omari Nundu, amebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC). Katika uchaguzi huo, Nundu aliambulia kura 127 kati ya kura 1,175 zilizopigwa.

Nundu ameangushwa na mpinzani wake mkubwa wa siasa, ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Tanga, Salim Kassim Kisauji, aliyeshinda kwa kupata kura 514. Kura hizo, zilipigwa mara mbili, baada ya awamu ya kwanza kukaribiana kwa karibu na Saumu Bendera, aliyepigiwa kura 446.


KOROGWE VIJIJINI

Habari kutoka Korogwe Vijijini, zinasema, Mbunge wa jimbo hilo, Stephen Ngonyani maarufu (Profesa Majimarefu), ameangukia pua, baada ya kushindwa na mpinzani wake, mchumi Dk. Edmund Mndolwa.
 
Washindi watakuwa wa kambi gani mkuu? Maana kambi ya Lowassa inasikika ndiyo yenye nyota ya ushindi!
 
Profesa wa uchawi kwishney!! Profesa wa CCM ni standard 7! Uchawi haujamsaidia?? Teh teh teh
 
Kama walienda kwa mwendo wa Hanang kwa Nagu (Tsh 100,000 kwa kila mjumbe) sasa washindi wajiandae kulipa madeni si kuwatumikia wananchi kwa sababu ushindi wao ulitegemea pesa na siyo sera na utumishi. 100,000/= @ wajumbe 1000 = 100,000,000. Bado hujaweka gharama nyingine za kampeni.
 
Korogwe vijijini wamepiga hatua, ni aibu kwa mtu aliyefeli darasa la 7 kuwa professor
 
Sasa ndo maana siaminigi waganga
huyu si ni mganga au amestaafu uganga?
Inaelekea ugonjwa wake hauna tibu za kijadi loo
 
mheshimiwa nundu cjui yuko katika hal gan sasa, coz nakumbuka alivyokuwa akijibu hoja kutetea kununua ndege chakavu povu lilimtoka kwel, xaxa kupigwa chin kwenye nec yao cpat picha povu lake
 
Back
Top Bottom