Elections 2010 'Prof. Maji Marefu' ashinda kura za maoni huko Korogwe - Sipati picha huko Bungeni!

Yule mtabiri wa Magomeni hajawania kwa tiketi ya CCM? au ataendelea na cheo chake cha "AFISA HABARI ZA KINAJIMU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI"
 
Shadow:

Haya matokeo yote ya kura za maoni za CCM ni "mapendekezo" - Tusubiri August 14 ndipo tutafahamu nani alishinda! (right?)
nani atathubutu kumuengua prof. au yeye hajipendi hiyo ndiyo imetoka.
 
Hadija Kopa naye anagombea ili akawape mipasho huko bungeni; vipi alifikia wapi huyo malkia wamipasho?
 
hadi mipasho nayo iingie Bungeni,ama kweli CCM wametuona sisi watanzania ni wendawazimu!
Na mwaka huu hawatausahau milele!
 
matokeo haya yanaonyesha watz hawababaiki na vyeti......dr nje kwa maji marefu....mwambulukutu nje kwa idd azan....mr 2 naye ndani.....
 
Sasa matambiko bungeni kama kawa....mzee wa vijesenti ukija na unga wako kwenye vifuko Profesa 'longi wota' anakuja na gunia zima halafu screen ya bunge inazima kabisa mpaka Profesa amalize kunyunyiza.
 
Ahaaahaaa! Profesa longi wota? Na huyo jamaa ni Simba s.c bladi, yaani yebo yebo mtakoma.
 
Amechoka kuwa ngazi ya kuingia mjengoni, kaamua ajipande kwenda huko! CCM eeeh, CCM nambari wani! Hiii ni ishara tosha utawala wa JK ndumba ni muhimu sana!
 
oooh my mjengoni sasa kutakuwa na mauza uza :bored::bored::bored:
Kila kukicha kuna jipya
 
Hapo awali niliandika siasa za TZ ni sawa muziki wa mduara,kenge,mijusi madodoki ,n.k kila mtu yuko huru kucheza,pia siasa zinaonyesha watu wa madaraja ya juu kama DR Mndolwa hawako karibu na wananchi wa kawaida au wachini,kazi yao kujifungia kweney mahekalu yao na kusogoa huko sijui Kempsiki,wanaonekana walikozaliwa wakati wa kuomba kura tu,si ajabu Dr Mndolwa akapotea tena hadi 2015.Dar Es Salaam ina sumaku bana wakubwa hawataki kukaa vijijini
 
CCM ina watu wa kila AINA. Aliyenishangaza mimi ni yule bwana aliyesababisha CCM ikaanguka kule Tarime, Kisyeri Werema Chambiri. Kaibukia BAbati na kumbwaga Mwalimu wangu Omar Kwaang'!
 
Kwa kweli huyu bana ana msaada mkubwa sana kwanza napenda kuwaambia sisiemu wamechelewa kumukubali kuingia mjengoni..inahuzunisha wakubwa wengi sana wabunge na wengine mawaziri wamekuwa wakiingia mjengoni kupitia huyu bana\nahisi safari hii amechoka kufwata ama ameona asome nyakati kwa sababu akliwa bungeni 1)Litamrahasishia watu wake badala ya kwenda mpaka TANGA2)Wana Dododma watanufaika sana na huduma yake aliokuwa akiwapa watu wa TANGA3)Atakuwa akiwakilisha moja ya Proffesion talented ambayo mpaka leo hii serikali wanakaataa kuiamini pamoja na ukweli halisi unaonekana 4)Atasaidia kwa kiasi fulani kupunguza mgawanyiko wa wabunge kama walivyokuwa hapo mwanzi nikiamaanisha akutakuwa na makundi ya watu wa bagamamoyo-Tanga-Zanzibara mchamba wima...na kuwa kundi moja la DomKila la kheri Prof

Huko mjengoni - assuming anapita, kutatisha si kawaida!
Constituency yake ni pana haina mipaka, hata kama anatoka jimbo gani!
 
CCM kwa uchawi na uwanga, hivi mumerithi toka kwa nani?

CCM wamerithi mikoba ya uchawi toka TANU na Afro Shiraz. Mwalimu wakati anang'atuka katika moja ya hotuba zake alikili kuwa alikuwa anakwenda Bagamoyo kwa maremu sheikh Ramiya!! Unafikiri alikuwa anakwenda kunywa kahawa?Bila uchawi ccm hupati kura wote hao unawaona humo mjengoni wanatembea na ndumba viunoni au mifukoni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom