Elections 2010 'Prof. Maji Marefu' ashinda kura za maoni huko Korogwe - Sipati picha huko Bungeni!

Huyo hakuwa na haja ya kwenda Bagamoyo kuutafuta ushindi wake...
 
Duh ama kweli siasa ya mwaka huu yangu macho. Juzi nilikuwa nasikiliza majina ya watu mbalimbali yakiwemo wanamuziki wa kizazi kipya, watangazaji wa Radio na watu mashuhuri katika nyanja za kijamii (si kisiasa) wanataka kuingia mjengoni kutuwakilisha kisiasa nikabakia mdomo wazi! Sijui ni katika kuonyesha kuchoshwa na uongozi wa vibopa au tu sasa siasa imegeuka mchezo wa kuigiza.

Haya Professor Maji Marefu kila la kheri
 
Ni habari njema tunaongeza idadi ya maprofesa bungeni, ila tu hapatakalika huko ole wake atakayepinga hoja yake atakiona anaweza kulala Dodoma na kuamukia ufukweni Pemba.
 
Jina gani tuupe uchaguzi huu? fumua fumua? mkanganyiko? anyway tuvute subira na kufanya post moterm analysis hapo Octobe 31,2010
 
JK anaweza kumteua kuwa waziri wa Afya akamrithi prof. mwenzake Mwandosya au akawa waziri wa utawala bora maana hakuna mtu atakaye hoji maamuzi yake.
 
Jina gani tuupe uchaguzi huu? fumua fumua? mkanganyiko? anyway tuvute subira na kufanya post moterm analysis hapo Octobe 31,2010

Shadow:

Haya matokeo yote ya kura za maoni za CCM ni "mapendekezo" - Tusubiri August 14 ndipo tutafahamu nani alishinda! (right?)
 
Anaitwa Steven Ngonyani jina la kisanii ni : PROFESA MAJI MAREFU.
hongera kwa kuchaguliwa kugombea ubunge kupitia CCM ukutane na wa CHADEMA chama dume.
 
Natumai jamaa akiweza kuingia mjengoni itakuwa balaa maana watakaoingia na ndumba zao atakuwa anawaona
 
Kwa kweli huyu bana ana msaada mkubwa sana kwanza napenda kuwaambia sisiemu wamechelewa kumukubali kuingia mjengoni..inahuzunisha wakubwa wengi sana wabunge na wengine mawaziri wamekuwa wakiingia mjengoni kupitia huyu bana\nahisi safari hii amechoka kufwata ama ameona asome nyakati kwa sababu akliwa bungeni 1)Litamrahasishia watu wake badala ya kwenda mpaka TANGA2)Wana Dododma watanufaika sana na huduma yake aliokuwa akiwapa watu wa TANGA3)Atakuwa akiwakilisha moja ya Proffesion talented ambayo mpaka leo hii serikali wanakaataa kuiamini pamoja na ukweli halisi unaonekana 4)Atasaidia kwa kiasi fulani kupunguza mgawanyiko wa wabunge kama walivyokuwa hapo mwanzi nikiamaanisha akutakuwa na makundi ya watu wa bagamamoyo-Tanga-Zanzibara mchamba wima...na kuwa kundi moja la DomKila la kheri Prof
 
Dah.. sijui "taaluma" ilitumika manake hilo gap kubwa aisee......
 
JK anaweza kumteua kuwa waziri wa Afya akamrithi prof. mwenzake Mwandosya au akawa waziri wa utawala bora maana hakuna mtu atakaye hoji maamuzi yake.

Hivi kumbe profesa ni profesa tu bila kujali Uprofesa wenyewe!!
 
Yangu Macho!! '' Sasa namuita Mheshiwa Profesa Maji Marefu".... Mheshimiwa spika, nashangaa mnalalamikia hii Wizara ya Miundombinu wakati tuna usafiri wa kutosha wa angani.
Kama wachawi wetu watawezershwa, hata wabunge wetu hawatahitaji VX , uanalala DOM ukiamka unajikuta MASAKI''

Acha tusubiri hoja za bunge lijalao :nono:
 
Shadow:

Haya matokeo yote ya kura za maoni za CCM ni "mapendekezo" - Tusubiri August 14 ndipo tutafahamu nani alishinda! (right?)

Maji marefu anaweza kupiga 'mkwara' kwa wajumbe wanaotakiwa wabariki matokeo teh teh
 
Back
Top Bottom