Elections 2010 Prof. Lipumba: Tanzania kwanza vyama baadaye

Nadhani uchaguzi wa mwaka huu umethibitisha wazi - CUF wanawaandama sana CHADEMA kuliko wanavyowaaandama CCM.
Usipoacha kusema uwongo wako, heshima yako itaendelea kushuka kidogo kidogo kama kifo cha CCM. Uchaguzi wa mwaka huu ni Oktoba 31, kinachoendelea ni mchakato wake. Thibitisha vipi CUF wanawaandama chadema katika uchaguzi wa mwaka huu?
Kwani ni CUF waliomkashifu na kumchafua mgombea wenu?
Ni CUF waliowarubuni wagombea wenu wa ubunge kujitoa?
Ni CUF waliokushitakini kwa Nec?
Mkuu msitafute visingizio vya kushindwa, watanzania wana akili zao, mtaaibika bure!
 
Hili lilikuwa ni swali rahisi tu kwako? Soma maandishi ya wanaojiita wanaCUF hapa jamvini uone kwa macho yako mwenyewe kuwa Target yao ni nani!

BTW - mbona unakwepa sana swala la CHADEMA kuiunga CUF mwaka 2000? Ulidanganya uliposema kuwa miaka yote CHADEMA wanataka CUF wawafuate?
 
Vipi kuhusu mwaka huu?
BTW - mbona CUF wanapondea sana CHADEMA kuliko CCM? au ndio moja ya makubaliano ya viongozi wa juu wa vyama hivi (Kikwete na Lipumba)?
Bado unashikilia vitu vya kubuni kwa akili yako...Mkuu hakuna makubaliano ya Prof. Lipumba na Kikwete.

Hili lilikuwa ni swali rahisi tu kwako? Soma maandishi ya wanaojiita wanaCUF hapa jamvini uone kwa macho yako mwenyewe kuwa Target yao ni nani!

BTW - mbona unakwepa sana swala la CHADEMA kuiunga CUF mwaka 2000? Ulidanganya uliposema kuwa miaka yote CHADEMA wanataka CUF wawafuate?
Ahaaaa! sasa nimekuelewa ulikuwa unanishughulisha sana, kumbe unaongea mambo ya JF? Mkuu, humu jukwaani kila mtu ana namna ya kukereketwa kwake, haina maana ukereketwa wa mtu na ushabiki wake humu JF ndiyo ukaufanya kuwa msimamo wa chama.

Mimi binafsi nakerwa na viongozi wabovu wanaoharibu harakati za vyama vya upinzani (Mfano Mrema na Mbowe) hii haina maana kuwa ndiyo msimamo wa chama changu. Kama washabiki wa CUF ndani ya JF wanaiponda chadema huo ni ushabiki wa kivyama na siyo msimamo wa chama cha CUF.
Mkuu nina hakika kuwa tangu CUF iingie katika ushindani wa kisiasa imekuwa ikijipanga vizuri na haikuhitaji msaada wa chama chochote kusimama kwanye uchaguzi. Kama chama chochote kingine kikisema kuwa kinaunga mkono CUF, haitakuwa na maana kuwa tumekubaliana hivyo kama makubaliano hayo hayapo.

Nitakupa mfano, mwaka huu chadema wamesema wanaunga mkono CUF kwa kiti cha urais wa Zanzibar, wala hakuna makubaliano hayo! kwamaana hata kama wasingesema CUF inaweza kusimama bila ya kuungwa mkono na chama chochote.

Hivyo hata mwaka huu tusingekuwa na haja ya kusubiri chadema tujuwe wana mgombea au hawana ndiyo tukubaliane kuungana mkono wakati mchakato huo haukuandaliwa tokea hapo. CUF haiwezi kufanya mambo kwa kukurupuka ndiyo maana imeweza kupiga hatua kubwa kuidhibiti CCM kila kona.
 
Mkuu Junius,

Asante kwa maelezo yako. Kwa vile tumechelewa sana kuunganisha nguvu zetu katika ngazi ya uraisi mwaka huu, natumaini bado tunaweza kuelekeza mapambano yetu katika kumng'oa adui wetu mkuu - chama cha mafisadi (CCM).

CHADEMA iliwahi kufanya nafasi yake kuunga vyama vingine kwenye chaguzi kuu. Mwaka 1995 waliunga mkono NCCR kama sikosei, na mwaka 2000 wakaunga mkono CUF (officially) kwenye uraisi wa JMT.

Kadri muda unavyokwenda, inayonesha kuwa vyama vingine haviko tayari kurudisha fadhila kwa CHADEMA katika chaguzi kubwa. Natumaini kuwa siku zijazo mambo yatabadilika.

Bado naamini kuwa vyama vya upinzani vyaweza kukitoa madarakani chama cha mafisadi hata pasipo kuungana. Vyama vya upinzani hata vyenye kupingana sera vyaweza kukitoa chama kilichopo madarakani (Conservative na LDP walifanikiwa hili UK).

Tuelekeze mbinu na hasira zetu kwa adui yetu mkuu, adui aliyefilisi nchi, adui anayedumaza nchi, adui anayeuwa wanawake na watoto wetu kila siku - chama cha mafisadi (CCM).
 
Mwafrika,
Nikubaliane na wewe kwa maneno ya Mh.Zitto Kabwe kuwa "...tukiwa tayari kwa dhati hili linawezekana". Na mimi nakubalina naye kuwa hili linawezekana tukijipanga vizuri tu....kwa kuwa watanzania sasa wanaanza kuzinduka kidogo kidogo. Mimi ni miongoni ninaomini kuwa kuiondoa CCM madarakani kunahitaji kitu zaidi ya umaarufu wa mgombea au chama chochote cha upinzani.
 
Pamoja tutaweza mkuu,
CUF waelekeze mapambano yao dhidi ya chama cha mafisadi, na chadema wakifanya hivyo pale walipo na nguvu, ccm itabaki bila pa kushika.

Wakija kwenye mambo ya uchumi - Prof yupo anawapiga mawe na kuwaambia nini kifanyike.
Wakija kwenye mambo ya nini kisifanyike, Dr Slaa anawafunua namna wanavyoliibia taifa hili.

CCM watakosa pa kushika, watakuwa wanapigwa from both sides. Hilo linafanyika na linaweza kukamilika mwaka huu.

Nice discussion so far.
 
Mkuu Junius,

CHADEMA iliwahi kufanya nafasi yake kuunga vyama vingine kwenye chaguzi kuu. Mwaka 1995 waliunga mkono NCCR kama sikosei, na mwaka 2000 wakaunga mkono CUF (officially) kwenye uraisi wa JMT.

Mbona umeng'ang'ania mwaka 2000 na unauruka uchaguzi wa mwaka 2005? Mwaka 2005 CUF haikuungwa mkono na Chadema na ilishika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha urais. Tena 2005 Lipumba alipata kura nyingi zaidi ya zile za 2000 alipokuwa anaungwa mkono na Chadema. Sasa badala ya kung'ang'ania kuwa uchaguzi 2000 Chadema iliunga mkono CUF, bora uzungumzie 2005 ilikuwaje.
 
Inamaana wewe ulitaka CUF (pekee) iwe inaungwa mkono kila mwaka?

CHADEMA wameunga mkono vyama vingine 1995, 2000. Chadema kama chama cha siasa, chenye malengo ya kushika dola, nacho kina kila sababu ya kuwa na mgombea wake.

Wewe unaonaje?
 
Nilimesoma hii Lipumba kaongea vema ila tatizo utekelezaji wake utakuwa mgumu kwa kuwa hana kura za kutosha kumpatia ushindi sopia hutuna historia yake ya utekelezaji mambo zaidi ya kuwa mshauri wa mwinyi.
So ni vema akawambia washabiki wake kuwa waache ushabiki wampe Slaa kura.
Lipumba anafaa kuwa waziri wa uchumi na fedha .

Na huyo Slaa ndiyo ana historia ya "utekelezaji" ipi zaidi ya kubwabwaja kwenye bunge la Tanzania? Samahani, nimesahau, Silaa ana historia ya kufanikisha safari ya Papa Tanzania. Alikuwa katibu wa TEC na alifanikisha ajenda nyingi za makanisa.
 
Crap,
Haishangazi hata hivyo, ni wale wale September--eeeee:

Join Date Fri Sep 2010 Posts 18
 
Inamaana wewe ulitaka CUF (pekee) iwe inaungwa mkono kila mwaka?

CHADEMA wameunga mkono vyama vingine 1995, 2000. Chadema kama chama cha siasa, chenye malengo ya kushika dola, nacho kina kila sababu ya kuwa na mgombea wake.

Wewe unaonaje?

Nachosema ni kuwa hakuna makubaliano ya aina yoyote yanayosema sisi tutawaunga mkono uchaguzi wa mwaka 2000 na nyie mtuunge mkono uchaguzi wa 2010 huku uchaguzi wa mwaka 2005 hauko kwenye mjadala. Chadema ilipoamua kumuunga mkono mgombea wa CUF ilifanya hivyo kwa hiyari yake na hata mwaka huu ilipoamua kumuunga mkono mgombea wa CUF kule Zanzibar nayo pia imefanya hivyo kwa uamuzi wake. CUF haikushirikishwa kwenye maamuzi hayo ya Chadema. Sasa leo kuja na hoja kuwa Chadema iliunga mkono CUF mwaka 2000 basi ni shurti CUF iwaunge mkono Chadema kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, kama siyo uwendawazimu basi ni kuishiwa na hoja.
 
Adui mkubwa wa Vyama pinzani na WaTanzania kwa ujumla ni Katiba mbovu katiba ambayo iliundwa kutumikia waTz katika utawala wa Chama kimoja ,leo hii kuna msururu wa vyama ,iweje bado inatumika katiba ya Chama kimoja ,naona kwanaza ni mabadiliko ya Katiba na halafu ndio kuna wezekana kabisa kuiondoa kasumba ya CCM na mizizi yake.

Ila kwa wakati huu mtapigishana makelele kwa sana lakini bado CCM ataibuka mshindi ,hivi mnajua hakuna kuhoji baada ya kutangazwa mshindi ?
 
ni kweli kabisa hili jukwaa lilitawaliwa na wenye mawazo ya mrengo wa dr.slaa tu na hawataki hoja zingine kuhusu mtu mwingine imefikia mpaka kutukanana ukitoa maoni tofauti,hi si sahihi imenitisha sana mie na wenzangu waoga.

ni vyema tuheshimu mawazo ya kila mwanaforum,
siku ya kura ikifika basi tuweke mapenzi yetu hapo ila hapa tuheshimiane.
Lipumba anafaa sana, na hana njaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom