Prof Lipumba ni Rasilimali ya Tanzania

Mwendawazimu si lazima aokote makopo! hata wewe kwa upuuzi huu uliouweka hapa ni uwandazimu tosha.
Yaani mtu kagombea urais mara 4 tofauti alafu eti unadai yeye ni rasilimali ya Tanzania!!? my foot!
Nakuhakikishia haitakuja kutokea Lipumba kuwa Rais wa nchi hii....yaani sahau hicho kitu kabisa! Ni rahisi mtoto wa Lipumba siku moja anaweza kuja kuwa Rais lakini si Lipumba mwenyewe....RIP CUF

Hakuna kazi ngumu na mbaya hapa duniani kama kuukataa ukweli....na kuufanya uongo ndiyo ukweli:Tafakari!
 
Josephine,

Mie mara nyingi when it comes to comparison between our president huwa sipendi kulijadili kwa kuwa nawaheshimu ila nimeona nikujibu kwani hujui unalolisema. Kwanza katika marais waliokuwa poor katika kiuchumi Nyerere was a failed president. He was given a country with an immense amount of wealth but left within a brink of bankruptcy kama hujui jiuliza kwanini tulilazimika kukubali ERP 1 and 2 za World Bank and IMF. Economic Reform Policy 1 and 2 Rais Mwinyi alibidi azikubali kwani nchi ilikuwa haina kitu. Kama ungelikuwa na umri kidogo basi ungelikuwa unakumbuka enzi za unga wa dona (rangi ya njano) na foleni za sukari guru miaka 70. Kwakuwa nchi ilikuwa imefilisika data zipo nakushauri ukazisome usiwe unaropoka.

Rais Mwinyi alipoikuta ile hali na kwa kumuheshimu Nyerere ndipo alipokubali masharti ya nyanja ya uchumi kulegezwa. Leo hii hatuvai tena mashati ya mchele mchele, tunaweza kukosoana na tunakuwa kiuchumi ni matokeo ya policy formula za Rais Mwinyi na Lipumba ndio alikuwa mshauri wake.

Hivyo nakushauri look carefully around you what you have including these forums is as result of macro economic policy relaxation ambazo ziliasisiwa na Mwinyi na chini ya ushauri wa Lipumba je hilo si la kujivunia? Kama hukumbuki muulize mchumba wako enzi za Nyerere tulikuwa hata kuzungumzia seirkali katika vijiwe vya mtaani tulikuwa tunaogopa leo hii tunaikosoa wazi mbele ya jamii sio mafanikio hayo? Ukuaji wa sekta mbali mbali mfano sekta ya benki sio mafanikio? Kama ulikuwa hujui zamani ulikuwa ukilipwa cheque na serikali inachukua siku 28-14 kulipwa leo hii inachukua siku 4 tu je hayo si mafanikio.

Kuna mwanafalsafa mmoja alisema kuwa kama huna jambo zuri la kusema dhidi ya mtu ni bora ukae kimya otherwise utajiabisha especially kwa mtu kama wewe unayeheshimiwa na jamii.

Mkuu hayo hayawezi kuonekana as long as huyo jamaa na kina dada Josephine wanatofautiana kiitikadi kesho akihamia CDM kama Prof Safari hizo sifa atakazopewa humu JF itakuwa funika bovu. Tabia hii haina tofauti na tabia ya marehemu kafa eti watu ndio wanasikitishwa na kumchangia ( refer mzee kipara RIP ) alikpokuwa hai na akiumwa watu walimpotezea.

Mimi kuna watu na waheshimu kwa sababu ya elimu yao naamini kuwa wanastahili heshima mmoja wapo akiwemo Lipumba, Issa Shivji, Dr Bilali, Dr Lwatama na wengineo wengi.

Tatizo la Lipumba na kwanini amefeli kwenye vinyang'anyiro vya uraisi mara nne.

Sisi watanzania tunapenda porojo kwenye siasa! tunataka tuambiwe fulani kaiba kiasi fulani mheshimiwa nanihii kafumaniwa na mke wa mtu na aina kwa aina za uzandiki na majungu yaliyojaa choyo! Lipumba hakuwa hivyo yeye alikuwa anakuja na takwimu kwenye mikutano yake hakujua kama wananchi hawataki takwimu za kiuchumi wanataka udaku!

Ukitaka kujua jinsi gani watu wanapenda udaku fuatilia siku za ijumaa kila mtu ana gazeti la kiu na ijumaa! anzisha thread ya kiudaku uone itakavyochangiwa! Hili ndio taifa tulilo nalo na huo ndio umekuwa ustaarabu wetu tukipata na vazi la taifa tutakuwa tumeshakamilisha.

Labda kwa kuongezea tu Lipumba amesaidia sehemu zifuatazo kwa ufupi.

Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).


Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).


Kutoa taarifa katika Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya uchumi na maendeleo (ECOSOC) kuhusu mgogoro wa kimataifa wa fedha katika nchi za Asia, NewYork (1998).


Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Windhoek, Namibia (1998).


Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Mbabane, Swaziland (1998).


Kutathmini maendeleo ya ‘The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa', (MEFMI) ili kuwasaidia wahisani kufanya maamuzi juu ya kuendelea kuisaidia taasisi hiyo,1998.


Nadhani watu wanajua kazi zake na ndio maana huwa wanampa kazi waswahili wanasema mtume huwa hakubaliwi kwao sisi wasambaa tunasema kui njako dashi njako. (tikiti baya.................) penye miti hapana wajenzi.
 
Mohamed Shossi said:
Nadhani watu wanajua kazi zake na ndio maana huwa wanampa kazi waswahili wanasema mtume huwa hakubaliwi kwao sisi wasambaa tunasema kui njako dashi njako. (tikiti baya.................) penye miti hapana wajenzi.

Mohamed,

..nakubaliana na wewe kwamba Prof.Nguyuru Ibrahim Lipumba ni mchumi aliyebobea.

..tatizo wanakosea CUF kufikiri kwamba maadam Prof amefanikiwa sana ktk taaluma ya uchumi, basi ataweza kuwavusha ktk harakati zao za kisiasa.

..Prof siyo mwanasiasa hilo tukubaliane. He doesnt have the instincts ambazo wanasiasa wanazo. Mfano mdogo ni jinsi alivyoendelea kukaa Washington D.C wakati chama chake kinapita ktk mgogoro na msukosuko. Prof angekuwa ni mwanasiasa basi ungemuona yupo akijishughulisha kutatua mgogoro uliokuwa ukikisumbua chama chake.

NB:

..hata msimamo wake kuhusu muungano haueleweki.

..wafuasi na viongozi wa chama chake walioko ZNZ wanafurumusha matusi na ubaguzi kwa wa-Tanganyika na yeye yuko kimya "anatafiti uchumi wa dunia."




 


Mohamed,

..nakubaliana na wewe kwamba Prof.Nguyuru Ibrahim Lipumba ni mchumi aliyebobea.

..
tatizo wanakosea CUF kufikiri kwamba maadam Prof amefanikiwa sana ktk taaluma ya uchumi, basi ataweza kuwavusha ktk harakati zao za kisiasa.

..Prof siyo mwanasiasa hilo tukubaliane. He doesnt have the instincts ambazo wanasiasa wanazo. Mfano mdogo ni jinsi alivyoendelea kukaa Washington D.C wakati chama chake kinapita ktk mgogoro na msukosuko. Prof angekuwa ni mwanasiasa basi ungemuona yupo akijishughulisha kutatua mgogoro uliokuwa ukikisumbua chama chake.

NB:

..hata msimamo wake kuhusu muungano haueleweki.

..wafuasi na viongozi wa chama chake walioko ZNZ wanafurumusha matusi na ubaguzi kwa wa-Tanganyika na yeye yuko kimya "anatafiti uchumi wa dunia."





Aisee hapo kwenye red mkuu nitatofautiana na wewe especial kwa mazingira ya hapa TZ na sio kwa Lipumba tu ila tumeshuhudia wanataaluma wengi wakiingia kwenye siasa na kuacha taaluma zao. Nadhani huo ni moja ya ufisadi ikiwa nchi inakabiliwa na uhaba wa madaktari na ratio ni 1:30,000 lakini tunawaona kina Prof Mtulia, Prof Sarungi na madr wengineo wakiacha kutibu wagonjwa na kukimbilia kwenye siasa!

Kwa pointi yako kama prof lipumba alitakiwa ajikite kwenye maswala ya uchumi/taaluma yake basi hata vyama vingine ukiangalia wengi ni watu walioibukia ukubwani na kuwa wanasiasa hawakusomea siasa kama taaluma ni wachache sana waliosoma mambo ya siasa wengi ni kama they were born to be politicians.

Ila mkuu mie sipendi kuwa mwanasiasa unajua kwanini? nitakuwa mwongo lol. Kitu ambacho mwanasiasa anasema ukweli ni jina lake tu yanayobakia yote ni porojo si huyo lipumba wala nanihii.
 
huu ni ukweli usiopingika ukibisha utaonekana una matatizo katika chako, huyu jamaa kweli ni prof wa ukweli mungu amempa akili na uwezo mkubwa, leo kuwa ni mtu mweusi pekee kutoka afrika aliyeshughulikia mtikisiko wa uchumi duniani akiwa ni mwenyekiti wao, akiongea kuhusu tanzania anasema yupo tayari kufanya tafiti juu ya tanzania ila tu wakubaliane kutekeleza utafiti huo na uchumi wa tanzania utapanda haraka na watanzania tutakuwa kwenye neema, ni professor pekee mwenye uchungu wa nchi yake, watanzania wameitupa almasi wazungu wameiokota. tusubiri 2015 labda watanzania wanaweza kuiona almasi.

Hana lolote ni mzee wa Pumba tu huyo, kwangu mimi ni mgombea uraisi wa kudumu kutoka kile chama cha Kizanzibar kisicho na sura ya muungano na kinachokufa.
 
Back
Top Bottom