Prof Lipumba kwenda SPAIN -Barcelona 28.3.2012

woyowoyo

Senior Member
Jul 24, 2011
173
12
amealikwa katika mkutano utakaojadili, "machafuko yanayoendelea ktk nchi za kiarabu na athari zake katika nchi nyingine" bado anaendelea na hasa anaelezea hali ya uchumi wa Tanzania umaskini unao wakabili waTanzania. nitaendelea kuwajuvya kinachoendelea, watu ni wengi mno.
 
..haya machafuko yanayoendelea ndani ya CUF amemwachia nani kuyashughulikia?

..mimi nadhani hali ndani ya chama cha CUF inahitaji usimamizi wa karibu sana wa Mwenyekiti Prof.Nguyuru Ibrahim Lipumba.

..kitendo cha mwenyekiti kuendelea na Fellowship yake Washington D.C wakati chama kinapita ktk misukosuko kinaashiria kwamba chama hakina umuhimu kwa Prof.Lipumba.
 
Nenda Prof Lipumba

kama wao wanakuona hufai kuna nchi wanakuona unafaa

Eng.Mtolera,

..Lipumba alipaswa kuwa nchini ku-coordinate ushiriki wa CUF ktk majadiliano ya mswada wa Katiba mpya, badala yake alikuwa USA kufanya utafiti wa masuala ya demokrasia.

..Prof amekaa USA kwa miezi mitano, lakini sijawahi kusikia akitumia muda kama huo kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kukijenga chama.
 
Ha ha ha.. sie tuta-google hapa tujue kama hii ni kweli au ndo kama lile changa la Marekani.. Mwenyekiti wa Maprofesa 500 duniani.. Wa kurekebisha Uchumi Duniani..
 
Bila Shaka hataacha kuwaambia jinsi ambavyo chama chake kinavyozidi kuimarika.

..haya machafuko yanayoendelea ndani ya CUF amemwachia nani kuyashughulikia?

..mimi nadhani hali ndani ya chama cha CUF inahitaji usimamizi wa karibu sana wa Mwenyekiti Prof.Nguyuru Ibrahim Lipumba.

..kitendo cha mwenyekiti kuendelea na Fellowship yake Washington D.C wakati chama kinapita ktk misukosuko kinaashiria kwamba chama hakina umuhimu kwa Prof.Lipumba.

Siongezi!
 
Kuna kiongozi mmoja alienda Spain akaishia kuwaalika kina Ronaldo wamtembelee Ikulu... acha wafu wazikane wenyewe
 
kwa kweli hotuba ya leo aliyotoa Prof Lipumba imenigusa sana, hasa hili suala la raslimali za Taifa zigawiwe kwa wanainchi wote na litamkwe na katiba tunayokwenda kuiunda na hili linafanyika brazil, mexico imesaidia sana kupunguza umasikini nchini mwao, lakini hapa TZ itakuwa utata mafisadi hawatakubali.
 
Mimi ni mmoja wao nilienda kumpokea pale air port baada ya ku danganywa kwenye masjid moja pale buguruni kuwa ni mwenyekiti wa maproff 500 lakini jf ikanifungua macho sitaki hata kumsikia tena Pambaf
 
Asije enda jidai kuwa yeye ni mlima kilimanjaro, na sifa za yule mwanamziki aliimba kibongofleva!
 
Eng.Mtolera,

..Lipumba alipaswa kuwa nchini ku-coordinate ushiriki wa CUF ktk majadiliano ya mswada wa Katiba mpya, badala yake alikuwa USA kufanya utafiti wa masuala ya demokrasia.

..Prof amekaa USA kwa miezi mitano, lakini sijawahi kusikia akitumia muda kama huo kuzunguka maeneo mbalimbali ya Tanzania kukijenga chama.

mkuu
naomba nikupe siri ya binadamu kama ulikuwa huifahamu

ni kwamba hata siku moja ktk dunia hii huwezi kumridhisha binadamu mwenzako

Prof:- akizunguka tanzania nzima kukiweka chama sawa WATASEMA,akienda spain WATASEMA,akikaa kimya WATASEMA cha muhimu hapa nikufanya kile unacho ona kina manufaa zaidi pasi kumwangalia nani kasema nini.go to spain Prof
 
Ofcourse hata mimi nilikuwa nina mpango wa kutoa taarifa juu ya mualiko wangu japo hauna maslahi kwa taifa na wala haitapunguza shida ya maji inayolikabili jiji kwa sasa, nimealikwa kuhudhuri birthday party ya mtoto wa rafiki yangu jumamosi hii atakuwa anatimiza miaka miwili. Asanteni sana
 
Lipumba ni kibaraka wa Seif Sharrif Hamad. Siku akimchoka atamtema kama alivyotemwa HR.
 
sasa trip za Prof. Mapumba zinatuhusu nini? kila mwanasiasa angekuwa anatangaza safari zake za makongamano ingekuwaje humu ndani? Tukianza na za Kikwete?
 
sasa trip za Prof. Mapumba zinatuhusu nini? kila mwanasiasa angekuwa anatangaza safari zake za makongamano ingekuwaje humu ndani? Tukianza na za Kikwete?

huyu ndio dira ya uchumi hivi sasa Duniani bila huyu Dunia inateketea kwa njaa haraka sana, ni juzi tu amerudi kurebisha mtikisiko wa uchumi Duniani, najua haya yanakuuma lakini mungu ndiye aliyempa uwezo, kama hutaki unanyukwa.
 
mkuu
naomba nikupe siri ya binadamu kama ulikuwa huifahamu

ni kwamba hata siku moja ktk dunia hii huwezi kumridhisha binadamu mwenzako
prof:- akizunguka tanzania nzima kukiweka chama sawa watasema,akienda spain watasema,akikaa kimya watasema cha muhimu hapa nikufanya kile unacho ona kina manufaa zaidi pasi kumwangalia nani kasema nini.go to spain prof

wafuasi wa cdm hapa jf wote ni vipofu kwa mazuri nje ya cdm lakini watashabikia zuri na hata baya la slaa. Prof go..
 
Back
Top Bottom