Prof Lipumba kila Mtanzania alipwe 450,000 kwa mwaka.

woyowoyo

Senior Member
Jul 24, 2011
173
12
M/kiti wa CUF Prof ibrahim Lipumba amesema inawezekana kila Mtanzania kulipwa sh 450000 kwa mwaka kutokana na raslimali zilizopo nchini. Prof Lipumba aliyasema hayo Dar es salaam jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mwembeyanga na kusisitiza kuwa fedha hizo zinaweza kulipwa kama watanzania wataamua kuweka kipengele hicho kwenye katiba Mpya. "Tanzania ina raslimali nyingi za asili kama bahari, gesi, madini ya dhahabu, tanzanite, mbuga za wanyama na nyingine nyingi ambazo zinaweza kuingizia Tanzania sh. bilioni 2 kwa mwaka ambazo zinatosha watanzania milioni 40 kugawana sh. 450,000 kwa mwaka.
 
du! Kumbe tunaweza kulipana hadi mshahara wa kuwa raia wa tanzania na nchi ikaendelea bila matatizo..basi ccm inatunyonya zaidi ya tujuavyo.
 
Sasa hapo sindio tutakuwa maskini zaidi maana 450,000 kwa mwaka ni sawa na bure kabisa.
 
M/kiti wa CUF Prof ibrahim Lipumba amesema inawezekana kila Mtanzania kulipwa sh 450000 kwa mwaka kutokana na raslimali zilizopo nchini. Prof Lipumba aliyasema hayo Dar es salaam jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mwembeyanga na kusisitiza kuwa fedha hizo zinaweza kulipwa kama watanzania wataamua kuweka kipengele hicho kwenye katiba Mpya. "Tanzania ina raslimali nyingi za asili kama bahari, gesi, madini ya dhahabu, tanzanite, mbuga za wanyama na nyingine nyingi ambazo zinaweza kuingizia Tanzania sh. bilioni 2 kwa mwaka ambazo zinatosha watanzania milioni 40 kugawana sh. 450,000 kwa mwaka.

Hizo hesabu zako ni Lipumba hazina mshiko unless umemquote vibaya au ni USD. Hata hivyo bado hizo hesabu zina utata!! Kwa kiasi hicho; 450,000 x 40,000,000 = 18,000,000,000,000 (18 Tillion). Pesa hizo ni zaidi ya bajeti yetu kwa mwaka. Kama anasema kwa utajiri tulionao hatukupaswa kuwa na bajeti tegemezi then nitamuelewa. Otherwise, hukumwelewa.
 
unambishia proff mkuu! aliyetoka UN juzi tuu tuliyempokea kwa mbwembwe!
 
Hizo hesabu zako ni Lipumba hazina mshiko unless umemquote vibaya au ni USD. Hata hivyo bado hizo hesabu zina utata!! Kwa kiasi hicho; 450,000 x 40,000,000 = 18,000,000,000,000 (18 Tillion). Pesa hizo ni zaidi ya bajeti yetu kwa mwaka. Kama anasema kwa utajiri tulionao hatukupaswa kuwa na bajeti tegemezi then nitamuelewa. Otherwise, hukumwelewa.
Something is wrong. Yaani Prof wa uchumi akurupuke kihivyo?
 
naamini hawajumisha wazanzibar kwenye paylist....mana kuwalipa itakuwa si haki
BTW-naona anazungumza ndoto tu
 
Hizo hesabu zako ni Lipumba hazina mshiko unless umemquote vibaya au ni USD. Hata hivyo bado hizo hesabu zina utata!! Kwa kiasi hicho; 450,000 x 40,000,000 = 18,000,000,000,000 (18 Tillion). Pesa hizo ni zaidi ya bajeti yetu kwa mwaka. Kama anasema kwa utajiri tulionao hatukupaswa kuwa na bajeti tegemezi then nitamuelewa. Otherwise, hukumwelewa.

Aisee huyu mzee anajitaftia umaarufu tena... kwanini asiseme kuwa hatupaswi kuwa na bajeti tegemezi?? yeye anarukia kuwa tunaweza KULIPANA.. haha haaaaaaaa acha nicheke.. ameshtukia wanaomsikiliza wananjaa na wakitajiwa ela lazima wamuunge mkono..!
 
Mimi navyoona,kwa rasilimali tulizonazo,zikisimamiwa vizuri,zitatosheleza kabisa budget ya Tanzania,na kubaki!!
Hicho kitakachobaki,kila Mtanzania ataweza kupata roughly hiyo 450,000/= !!It's possible kabisa ukiangalia hii issue kwa jicho la ziada!!!
 
watanzania ni walalamikaji wazuri sana,tunalalamika flani ameiba mabilioni wakati wenyewe kwenye nafasi zetu tunakula rushwa za sh elfu kumi(tukisingizia maisha ni magumu),na pia ni wazembe,tunachelewa kazini nk.unadhani taifa litajengwa hivi!?Taifa hujengwa na kila mtu anapoamua kukaa katika nafasi yake na kufanya kitu kwa manufaa yake,kama unasema mwenzako aliyeiba bilioni wakati na wewe umeiba elfu 50,huna tofauti nae,wote ni sehemu ya wahujumu uchumi wa Taifa letu,Watanzania tuache unafiki.
 
Aisee huyu mzee anajitaftia umaarufu tena... kwanini asiseme kuwa hatupaswi kuwa na bajeti tegemezi?? yeye anarukia kuwa tunaweza KULIPANA.. haha haaaaaaaa acha nicheke.. ameshtukia wanaomsikiliza wananjaa na wakitajiwa ela lazima wamuunge mkono..!

Halafu ni mapema sana kuzungumiza kulipana wakati shule zetu za sekondari hazina maabara,zahanati hazina vifaa vyaa kutosha na dawa,barabara mbovu,ndo ujue unafiki wa wanasiasa.
 
watanzania ni walalamikaji wazuri sana,tunalalamika flani ameiba mabilioni wakati wenyewe kwenye nafasi zetu tunakula rushwa za sh elfu kumi(tukisingizia maisha ni magumu),na pia ni wazembe,tunachelewa kazini nk.unadhani taifa litajengwa hivi!?Taifa hujengwa na kila mtu anapoamua kukaa katika nafasi yake na kufanya kitu kwa manufaa yake,kama unasema mwenzako aliyeiba bilioni wakati na wewe umeiba elfu 50,huna tofauti nae,wote ni sehemu ya wahujumu uchumi wa Taifa letu,Watanzania tuache unafiki.

Kweli kabisa, wavivu wa kutupwa, kila siku maziko, leo mjomba kesho mama mkubwa, kesho kutwa jirani. Kuumwa ndio usiseme, mtu akiamka na hangover, huyo kazini hawamuoni.

Ni wavivu na tunachekeleana sana. Inabidi tubadilike wenyewe na si kudangayana kuwa tunaweza kupeana pesa za bure.

Huyu Lipumba nae, kachanganyikiwa, umpe laki nne na nusu kwa mwaka Mtanzania, na miradi?
 
Hizo hesabu zako ni Lipumba hazina mshiko unless umemquote vibaya au ni USD. Hata hivyo bado hizo hesabu zina utata!! Kwa kiasi hicho; 450,000 x 40,000,000 = 18,000,000,000,000 (18 Tillion). Pesa hizo ni zaidi ya bajeti yetu kwa mwaka. Kama anasema kwa utajiri tulionao hatukupaswa kuwa na bajeti tegemezi then nitamuelewa. Otherwise, hukumwelewa.

jamani wana js,someni maandiko na muyaelewe,mala nyimgi tumekuwa tunabadirisha kilicho semwa ama kuandikwa
 
M/kiti wa CUF Prof ibrahim Lipumba amesema inawezekana kila Mtanzania kulipwa sh 450000 kwa mwaka kutokana na raslimali zilizopo nchini. Prof Lipumba aliyasema hayo Dar es salaam jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mwembeyanga na kusisitiza kuwa fedha hizo zinaweza kulipwa kama watanzania wataamua kuweka kipengele hicho kwenye katiba Mpya. "Tanzania ina raslimali nyingi za asili kama bahari, gesi, madini ya dhahabu, tanzanite, mbuga za wanyama na nyingine nyingi ambazo zinaweza kuingizia Tanzania sh. bilioni 2 kwa mwaka ambazo zinatosha watanzania milioni 40 kugawana sh. 450,000 kwa mwaka.
Billion 2 uzigawe kwa watz mil 40 kila mmoja apate laki 4.5. Labda mimi ndo sijui hesabu. By the way anaishi kwa kuongea jukwaani.
 
Nadhani hoja yake ni kutaka watanzania waelewe kuwa pato la taifa ni lao. Kwa sasa hivi pato la taifa ni la serikali na watu wanakuwa hawawajibishi wanaofuja mali ya serikali.
 
hii idea ya Lipumba ni superb. Jaribuni kumuelewa anachomaanisha.
Kwanza under 18 hawatajumuishwa kwenye malipo.
Pili wale wote wenye formal employment hawatajumuishwa.
Tatu pesa hizi hazitolewi ili watu wakanunue khanga, pombe au anasa fulani. Hizi ni pesa ambazo asilimia kubwa itakatwa kuwa invested kwenye shughuli za maendeleo ambayo watu hawa wanaishi. Sasa kitakachotokea ni kwamba watu watakuwa na hasira na maendeleo. Wakiona kisima hakijachimbwa na pesa yao imekatwa watakuwa wakali kwa wasimamizi. Hivi sasa pesa za TASAF zikiibiwa no body feels kwamba ameibiwa, ila angeambiwa kuwa katika ile 450,000 yako umekatwa 120,000 kwa ajili ya kisima halafu kisima hakioni - you can imagine reaction yake kwenye kikao cha kijiji.
Huu mpango ni mzuri na unatekelezeka.
 
Back
Top Bottom