kutoka mwananchi
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amesema malumbano ya wafanyabiashara yanayoendelea kushika kasi nchini kuhusiana na ufisadi, hayana tija kwa taifa badala yake yanalitoa katika harakati zake ya kukabiliana na changamoto za maendeleo.
Profesa Lipumba alisema hayo jana katika mahojiano na gazeti hili kuhusiana na kauli ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz aliyemtuhumu Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kuwa ni nyangumi wa ufisadi.
Alisema malumbano hayo yanawafanya Watanzania wengi kuacha kujadili mambo muhimu ya kimaendeleo na kubaki kwenye fitina zinazosambazwa na wafanyabiashara hao.
Aliitaka serikali ya Rais Jakaya Kikwete kukomesha tabia ya wafanyabiashara kukamiana kupitia vyombo vya habari, kwa lengo la kuwashirikisha wananchi kwenye chuki zao ambazo zinaotesha mbegu za rangi na ukabila, hivyo kutishia amani ya nchi.
Tanzania ni nchi maskini ingawa tuna rasilimali nyingi. Tumekuwa na tatizo kubwa la kushindwa kujipanga vizuri katika kuzitumia. Kwa jinsi suala hili la ufisadi linavyokwenda, linazidi kutuvuruga, alisema Lipumba na kufafanua: Mijadala (malumbano) hii inazidi kututoa kwenye mstari.
Hata hivyo, alisema katika maelezo ya Rostam, ambaye pia ni Mbunge wa Igunga, kuna hoja nzito alizozitoa na ambazo zimewafumbua macho Watanzania, hivyo Rais Kikwete hana budi kuzishughulikia kikamilifu.
Alitaja miongoni mambo hayo kuwa ni tuhuma kuwa Mengi alikopa mabilioni Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kabla haijabinafsishwa na hakurejesha na vile vile alichukua mabilioni mengine kwenye mfuko unaochangiwa na wahisani; Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (CIS) ambazo pia hakuzirudisha serikalini kama ilivyo utaratibu wa mfuko huo.
Aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuutangazia umma wote waliokopa NBC na CIS na kuwaamuru walipe na kwamba, wachukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa mafisadi wengine waliochota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Profesa Lipumba, alisema kama nyaraka zinazohusu fedha za CIS zitakosekana Hazina, serikali iwasiliane na nchi wahisani wa mfuko huo, kwa sababu wana kumbukumbu za kampuni zote zilizokopa.
Alimtaka Rais Kikwete kuonyesha dhahiri nia yake ya kupambana na ufisadi kwa kutowaonea huruma wafanyabiashara wote wawili ambao kila mmoja anaonekana yuko karibu naye (rais).
Profesa Lipumba alisema anamtambua Rostam kuwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mengi ni mwanachama wa CCM ambaye amekuwa akijinadi kuwa anamsaidia Rais Kikwete kwenye vita dhidi ya mafisadi; hivyo akasisitiza wote wako karibu na Rais Kikwete.
Alisema fedha za Mfuko wa CIS hutolewa na wahisani ili kuwasaidia wafanyabiashara kuagiza bidhaa nje na hutakiwa kurejeshwa serikalini kwa shughuli nyingine za maendeleo, hivyo kama hazikurudishwa, huo utakuwa ni wizi wa mali ya Watanzania.
Kuhusu EPA, Profesa Lipumba aliendelea kusisitiza kuwa ripoti ya awali ya ukaguzi ilionyesha kampuni ya Kagoda ilighushi nyaraka ili kuzichota hizo fedha, hivyo haoni sababu ya serikali kutowapeleka mahakamani wahusika au wamiliki wake ambao mpaka sasa wanafichwa.
lipumba unataka kikwete amshughulikie mengi je marafiki zako RA, manji(nssf). tanil, jetu et al vipi.
Mengi ameshamaliza hizo kesi zote mahakamani!
Kweli RA payroll yake ni kubwa mpaka Lipumba....![/QUO
Lipumba nina wasiwasi ajenda yake ina ashiria udini.