PatriotMzalendo
Member
- Jan 17, 2011
- 28
- 6
Kama hana tamaa ya madaraka na ni mtu aliyebobea kwenye taaluma ya Uchumi,kwenye siasa anafanya nini? Mchumi asiye na tamaa ya madaraka kwa nini asiishi kwa taaluma yake badala ya kujidhalilisha kwa kupambana na madongo ya kisiasa ambayo katika kuyakabili wakati mwingine anafanya usomi wake uwe questionable?Lipumba ni moja kati ya watu makini! Hana tamaa ya madaraka kama ilivyo kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa hapa nchini. Vilevile anaheshimika si Africa tu bali Duniani kwa ujumla! Taaluma ya uchumi aliyonayo imetumika kuimarisha hali za kiuchumi katika baadhi ya Mataifa duniani.
Tatizo letu sisi watanzania ni ushabiki/unazi,hatuwezi kabisa kupima uwezo wa mtu na kumpa heshima anayostahili. Na ushabiki/unazi huu utatufanya tuendelee kuwa duni hadi kiama!