Prof Lipumba alia rafu Nec

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
lipumba%20nec.jpg

Prof Ibrahim Lipumba

Exuper Kachenje na Hawa Mathias


CHAMA cha Wananchi (CUF), ambacho kimekuwa kikidai kuchezewa rafu katika kuhesabu kura, hasa visiwani Zanzibar, kimeibua tena wasiwasi wake baada ya kuihoji Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuhusu uchapishaji wa karatasi za kupigia kura.Chama hicho, ambacho kimekuwa kikishika nafasi ya pili katika chaguzi mbili zilizopita, pia kimeitaka Nec kuweka hadharani mapema daftari la wapigakura ili lifanyiwe uhakiki na kuepuka kuwanyima baadhi ya wananchi haki ya kupiga kura.

Nec ilishakaririwa ikisema kuwa karatasi hizo zitachapishwa nchini Uingereza na kwamba vifaa vyote kwa ajili ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Oktoba 31, tayari vimeshatayarishwa huku ikiahidi kuwa wote waliojiandikisha kupiga kura watatumia haki yao kutokana na kuandaa mfumo bora.


Lakini mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alionyesha wasiwasi wake kuhusu karatasi za kupigia kura wakati alipoongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu muhtasari wa awamu ya kwanza ya kampeni zake katika mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara, Songea na Mbeya.


“Bado tuna matatizo na Nec... hawashughulikii mambo mengi; hatujui ballot papers (karatasi za kupigia kura) zitakuwaje, zitachapwa nchini au nje,” alisema Prof Lipumba ambaye anagombea urais kwa tiketi ya CUF kwa mara ya nne sasa.


Alifafanua kuwa hadi sasa wakati zimebakia siku zisizozidi hamsini kabla ya tarehe ya kupiga kura, Nec imekaa kimya kuhusu karatasi za kupigia kura na ushiriki wa vyama vya siasa katika kuziandaa, jambo alilosema linawatia wasiwasi.


“Nina wasi wasi na utaratibu wa Nec, ballot paper zitakuwaje wala hatujui ushiriki wetu katika kuziandaa utakuwaje,” alilalamika Lipumba.


Lipumba ambaye pia ni mweyekiti wa CUF alisema kuwa chama chake tayari kimeiandikia Nec barua mbili kikitaka kujua suala hilo, lakini hadi sasa hawajapata majibu kutoka tume hiyo ambayo alisema imeendelea kukaa kimya.


Alisema mapendekezo ya chama chake ni kwamba karatasi hizo za kupigia kura zingefuata mfumo wa mwaka 2005 huku akifafanua kwamba itakuwa bora wagombea wakapangwa kwa kufuata alfabeti.

Huku akiilaumu Nec, mgombea huyo wa urais alisema tatizo kubwa la msingi ni tume hiyo kutotenda haki kwa wapigakura na vyama.

Kuhusu daftari la wapigiakura, Lipumba alisema kuwa Nec inapaswa kulitoa mapema Bara na Zanzibar ili lihakikiwe kwa kuwa chama chake kimegundua kuwa wapo wananchi wengi wenye vitambulisho vya kupigia kura, lakini majina yao hayamo katika daftari hilo, hivyo kujenga hofu ya kukosa haki yao ya kupiga kura.


“Tunahitaji hili daftari ili lihakikiwe... sote tuone. Ni muhimu kulipata mapema ili tuweze kuwaelimisha vema mawakala wetu wajue taratibu, sheria na haki zao,” alisema.


Kuhusu kampeni za uchaguzi mkuu Lipumba alisema wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanazuia njia zote alizoziita za ‘kichina na za kuchakachua’ matokeo, huku akilisifu Jeshi la Polisi kwa kumpa ulinzi wa saa 24 na pia kuwapongeza wakuu wa wilaya kwa ustaarabu na ushirikiano mwema katika kampeni zake.


Kuhusu wagombea waliopita bila ya kupingwa, Prof Lipumba alisema ushindi wao utatia shaka na kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi, akidai kuwa kuna ushahidi kuwa baadhi ya wagombea walinunuliwa.


Alieleza kuwa ishara ya rushwa kuwa wazi ameiona hata katika kampeni zake akitoa mfano wa mtu aliyemuita ‘mmachinga mwenye asili ya kimasai" ambaye baada ya kusikiliza kampeni zake alimuomba fedha akisema: "Mzee unaniachaje?”


Lipumba alisema baada ya ombi hilo alimwuliza mmachinga huyo kama haogopi Takukuru naye alimjibu kwa kumwomba watoke pembeni ya eneo hilo ili Takukuru wasimuone.

Hata hivyo, alionyesha hofu kuhusu hali hiyo akieleza kuwa kubadilika kwa mambo hayo tofauti na ilivyokuwa mwaka 2005 kusiwe chambo na baadaye kugeuziwa kibao.

Alisema kutokana na kulitambua hilo, CUF inafanya kampeni zake Bara na Zanzibar kwa tahadhari kubwa kuhofia kugeuziwa kibao.


Alipotakiwa kueleza mtazamo wake iwapo kura zingepigwa leo, Lipumba anayegombea urais kwa mara ya nne mwaka huu, alisema: “Nina hakina uchaguzi ungefanika leo, tutapa kura za urais zaidi ya asilimia 50."


Prof Lipumba alisema CUF itashinda ubunge kwenye majimbo ya Kilwa, Rufiji, Kibiti, Lindi Mjini, Lindi Vijijini, Liwale, Newala, Tandahimba, Tunduru Kusini na Kaskazini pamoja na Mbeya Mjini.

Chanzo: Mwananchihttp://www.mwananchi.co.tz/componen...news-story/4871-prof-lipumba-alia-na-nec.html
 
Asante profesa wewe nakuamini ni mtu makini kabisa wala si mbabaishaji kama hawa viongozi wengine wapenda madaraka na wenye kudandia na kutaka urais wa ghafla baada ya kuona ubunge haulipi! Profesa nahakika kabisa ushindi ni wenu cuf mwaka huu hasa visiwani ushindi uko wazi na huku bara kampeni ulizopiga huko ktk mikoa ya kusini na ukija kuunganisha na mikoa ya tanga, dar-es-salaam, tabora, kigoma, mwanza, kagera na kumalizia mara naamini kama hakutakuwa na mizengwe ktk kuhesabu kura basi ushindi uko wazi kwa cuf na mikoa iliyobakia ya kilimanjaro, arusha, singida, shinyanga,na dodoma waachieni ccm na chadema wagawane!

Profesa lipumba nakuamini kwa ahadi zako wewe ni msomi uliebobea ktk uchumi na hasa uchumi unaoangalia zaidi maslahi ya walalahoi(micro-economy) na ndiyo hasa uliyosomea na cuf inawasomi wa aina zote yaani wamo wanauchumi, wanasheria, wenye kujua kutangaza sera, nk.

kura kwa lipumba na cuf!!!!!
[size=+0]haki sawa kwa wote[/size]!!!
 
Back
Top Bottom