Prof. Lipumba akana kumtetea Pinda, akiri kupigiwa simu kuhusu uwaziri

Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. (Mambo ya Walawi 11:07-08)
 
WAKATI macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete aliyeahidi kufanya mabadiliko makubwa kwenye baraza lake la mawaziri, jina la Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwapo kwenye baraza hilo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Aliahidi wapi?

Na Tanzania Daima nalo ni gazeti la kuaminika? si la Mwenyekiti wa Chadema hili? au sio?
 
akiwemo huyo then tutajua kua ccm na cuf sasa wameungana...huwezi jua labda ccm wanaona hawawezi kushinda wenyewe so wanawachukua na wana cuf..mbona kule zenji cuf na ccm ziko pamoja zinasaidiana...??!!
 
Hahahaha CCM wana hila nyie wala msijidanganye wachanganye na wapinzani! na hivi jahazi linazama ndo kabsaaa!
 
Hayo ni mambo ya chabo hayo. Siamini gazeti la mtanzania daima linaweza kuandika utombo namna hii, linakoelekea sio kuzuri linayafuata wakina habarileo mzalendo na uhuru, ambayo kwa sasa hayana mvuto kabisaa.
 
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Msiile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu. (Mambo ya Walawi 11:07-08)
Good quote GC

tatizo huwa tunachagua cha kufuata....

Pia alisema tusisengenye, tusiabudu uchawi, tusiue, tusilawiti, tusidhulumu.... nk

Hayo yote hatufuati, bali hili la nguruwe, ni rahisi kufuata kwani kuna sungura, ngombe, ngamia, samaki, mbuzi nk.

SASA ASIFA HABARI NKASI WATAMPA UBUNGE WA KUTEULIWA??
 
Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu kutoka nje kinachoweza kumtia mtu najisi. Lakini kimtokacho moyoni ndo chamtia najisi.Kwa maana hakimwingii moyoni ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni. Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi.mawazo mabaya, uasherati,wizi,uuaji,uzinzi,uchoyo,uovu,udanganyifu,ufisadi,wivu,kashfa,kiburi na upumbavu. Hayo ndo yamtia mtu unajisi. Marco 7:14-23. Mungu amehalalisha vyakula vyote.Ndugu kitimoto halali yako.
.
 
WAKATI macho na masikio ya Watanzania yakielekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete aliyeahidi kufanya mabadiliko makubwa kwenye baraza lake la mawaziri, jina la Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwapo kwenye baraza hilo, Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Profesa Lipumba ambaye si miongoni mwa wabunge, anatajwa kuwa mmoja wa mawaziri watakaoteuliwa kutoka nje ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Rais Kikwete ambaye tayari ameshapata baraka za Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya mabadiliko, anatarajia kutangaza mawaziri wapya wakati wowote kutoka sasa baada ya mawaziri wake wanane kukumbwa na kashfa ya ufisadi iliyoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM na CUF, zinaeleza kuwa Rais Kikwete anatarajia kumwingiza Profesa Lipumba kwenye baraza lake na kwamba anaweza kumpa wizara ya Fedha na Uchumi.

“Kuna taarifa kwamba Profesa Lipumba anaweza kuwa miongoni mwa sura mpya za mawaziri. Anachoweza kufanya Rais ni kumteua kuwa mbunge, kisha kumpa uwaziri.

“Na kwa vile Bunge linatarajiwa kukutana Juni 12 mjini Dodoma, kama kuna watu kutoka nje ya Bunge ambao Rais anataka wawemo kwenye baraza lake, anaweza kuwateua kuwa wabunge na mawaziri wateule hadi hapo watakapoapishwa bungeni, ndipo ataweza sasa kuwaapisha kuwa mawaziri,” kilisema chanzo chetu cha habari.

Alipoulizwa na gazeti hili kwa njia ya simu, Profesa Lipumba alisema kuwa hawezi kuzungumzia uvumi huo kwani hata yeye ameusikia kutoka kwa watu mbalimbali.

“Siwezi kuzungumzia nafasi yangu kuhusu taarifa hiyo, lakini ukweli ni kwamba hadi sasa sijaitwa na Rais kwa ajili ya mashauriano yoyote kuhusu jambo hilo na kimsingi najua kama ana mpango huo, angeniita, lakini sijaitwa na sina taarifa,” alisema Profesa Lipumba.

Mwenyekiti huyo wa CUF ambaye ni mchumi, alisema kuwa amepigiwa simu na vyombo vya habari kadhaa pamoja na watu wengine kumuulizia jambo hilo ambalo alisisitiza ni uvumi usio na ukweli wowote.

Kumbe ni uvumi,sasa uvumi unauweka vipi hapa?
 
good quote gc

tatizo huwa tunachagua cha kufuata....

Pia alisema tusisengenye, tusiabudu uchawi, tusiue, tusilawiti, tusidhulumu.... Nk

hayo yote hatufuati, bali hili la nguruwe, ni rahisi kufuata kwani kuna sungura, ngombe, ngamia, samaki, mbuzi nk.

Sasa asifa habari nkasi watampa ubunge wa kuteuliwa??

wacheni haya mambo jamani. Mahali pengine anasema, nguruwe kula wakati huna jinsi kwa kuokoa nafsi. Kumbe kuokoa nafsi kunabatilisha ukweli? Si afadhali uifie imani ya kwanza?
 
Hata kama Lipumba anaota uwaziri,haiwezekani kwani yeye si mbunge,itabidi Jk amteue kwanza then uwaziri,hii ni ndito ya saa sita mchana kwa magamba government
 
...Yes, Prof Lipumba anafaa sana kwenye hiyo nafasi, nitamuunga mkono JK kama atafanya hivyo...
 
Tht possble throw uteuz wa ubunge wa rais coz idadi ya wabunge 10 haijatimia..mfano mzur ni shamsi nahotha hakua mbunge bt nw ni waziri wa mambo ya ndani...Thr4 mcpinge kila mlisikialo..
 
Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu kutoka nje kinachoweza kumtia mtu najisi. Lakini kimtokacho moyoni ndo chamtia najisi.Kwa maana hakimwingii moyoni ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni. Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia najisi.mawazo mabaya, uasherati,wizi,uuaji,uzinzi,uchoyo,uovu,udanganyifu,ufisadi,wivu,kashfa,kiburi na upumbavu. Hayo ndo yamtia mtu unajisi. Marco 7:14-23. Mungu amehalalisha vyakula vyote.Ndugu kitimoto halali yako.
.
kwahiyo kula nguruwe sio issue eh??

safi sana, ngoja niagize kilo

kwenye uasherati ni kipi chaingia na kipi kinatoka??

ndio maana biblia imetumia neno busar mara nyingi zaidi kuliko wokovu kwani inajua kwamba without wisdom sisi si mali kitu

ila ndugu yangu dotto kama kawa, kakurupuka
 
Jamani Raisi JK anaweza kufanya hivyo kutokana na kuwa na akiba ya viti 7 vya kuteua wabunge wa viti maalum kati ya 10 alivyonavyo kikatiba, alitumia nafasi 3 tu mwaka 2010 alipokuwa anaanza ngwe yake ya pili ya Urais wake kwa kumteua Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni waziri wa mambo ya ndani wa sasa, Prof Makame Mbarawa pamoja na Mama Zakia Meghji tu ndiyo walioteuliwa na Rais mwaka 2010, kwakuwa katiba inamruhusu kuteua watu 10 kuwa wabunge kwa kupitia viti maalum nafikiri kwa sasa ataweza kutumia akiba yake ya nafasi 7 zilizosalia kwa kuwateua hao waweze kuingia katika baraza lake jipya la mawaziri kwa kuwa hana watakatifu wengine pale bungeni ambao siyo wachafu kisiasa, kila aliyebaki ana kashfa yake inayomuandama, tusubiri tutaona.
 
Wana jf nimesikia leo katika vyombo mbali mbali vya habari kuwa,Mkuu wa Kaya yetu anatarajiwa kusuka baraza lake la kuongoza kaya yetu upya.
Safari hii ni kwa staili mpya kabisa, inasemekana ule upepo wa Zenji utafika na bara "ndoa ya cuf &ccm"
Mvumilivu hula mbivu, Mh. Lipumba aweza kuingia tena Mjengoni safari hii akiwa na TITLE kubwa, Waziri sio 'kivuli' wa ukweli kabisa.
Swali ni kama itakuwa kweli atakwenda kuwa Prof. wa mawaziri wote "mkuu wa mawaziri" au kuwa mchumi?.
Na je ni inaonyesha kuwa ni kweli wasafi ni adimu ndani ya ccm?.
 
Back
Top Bottom