Prof. Lameck Mabelya of MUHAS is no more!

Alikuwa anaumwa ? Duu kila nafsi itaonja mauti......, inna lilah waina ilaih raj'uun, namkumbuka sana prof. Kipindi kile akiwa head, Department of Community and preventive Dentistry, alitufundisha health economics.......So Sad
 
Nusu saa iliyopita kuna mtu ameniletea sms akieleza kwamba Prof Mabelya hayuko nasi tena. Akasisitiza kwa kusema "Amefariki dunia". Nilivyopigwa na butwaa sikuweza tena kuuliza zaidi. Sijawahi kumsikia hapa karibuni kwamba alikuwa anaumwa, lakini kumbe ni mara ya mwisho nilimwona akipita mbele ya jengo lao na PRADO lake akiwa anaenda zake nyumbani. Tulizoea kupungiana mkono tukitiana machoni lakini this time nadhani alikuwa amefocus njia asisababishe ajali nadhani hakuniona. He was a man of the people, mpole asiye na maneno mengi. Sijapita mikononi mwake kama mwalimu, kwa sababu nilipoingia hapo yeye alikuwa Denmark kusoma, aliporudi nami nilikuwa nimemaliza tukabaki kufahamiana kwa maingiliano ya kitaalam zaidi na kwa kuwa alikuwa Dean of Faculty ilikuwa ni lazima ukutane naye kiutawala pia.

SoD imepoteza mtu muhimu sana. Amefundisha wanafunzi wengi sana hasa Community Dentistry na kusimamia postgraduates wengi pia. Kipenzi cha watu wengi hata hatuwezi kusema yote. Mungu tu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amen. ndugu na jamaa na marafiki zake kwa kweli Mungu awatie nguvu sana. Tulimpenda, lakini Mungu amempenda zaidi. Mara nyingi migulubaja hudumu zaidi ili siku moja ifunguke na kutubu kuunganika na Mungu kiroho, lakini wapole na wacha Mungu hutoweka haraka ili wasichafuliwe wakakosa ahera waliyoandaliwa milele. Tujifunze tu, kwamba kuna kifo mbele yetu, tuache mabaya na kutubu. Kusali ni muhimu kabla hatujaswaliwa.

Tutabaki na historia yake mzee wetu Mabelya, Mungu atujalie tuyaendeleze yale mema yote aliyofanya. Sijamsikia kuwa na maadui, lakini binadamu hukosea ili kuonyesha kwamba ni binadamu, tusameheane ili aende kwa amani, nasi Mungu aturehemu kama tulikwazana naye mahali fulani. Ndio utu bora.

RIP Professele Mabellya.
 
Mleta habari mbona hueleweki?
Wewe umeleta news halafu uantaka details zipi?
kumbuka hili sio gazeti wala blog ya mtu ..hapa kila mtu ni mwandishi huyu hapa kaja na tetesi kama una details more weka hapa kama huan nyamaza wenye nazo wataleta na wengine ndio tunazitafuta habari kamili ..sio kulalama..hii ni forum
 
Kama ni kweli, basi tunaweza kusema mgomo wa madaktari umekula kwao. RIP Professor
 
R.I.P DR, JAMANI
Iknew proff Mabelya. alikuwa ananing`oa meno nikiwa mdogo

Ni kweli amefariki hasubuhi hii ghafla nyumbani kwake akiwa ametoka mazoezini.
 
kumbuka hili sio gazeti wala blog ya mtu ..hapa kila mtu ni mwandishi huyu hapa kaja na tetesi kama una details more weka hapa kama huan nyamaza wenye nazo wataleta na wengine ndio tunazitafuta habari kamili ..sio kulalama..hii ni forum

Habari nzito kama hizi mmmmh! Ni bora ukawa na details kidogo
 
Hii habari ni ya masikitiko sana. Ukiwa mmoja wa wana ndugu, naomba nifikishie pole kwa ndugu hapo Dar na Bariadi. Mungu ailaze mahala pema roho ya mpendwa wetu Mabelya!
 
RIP, Prof mabelya
namjua vizuri sana huyu mzee ni mtu mpole, mwenye imani, na mwenye kutoa kile alicho nacho
mara ya mwisho kuongea nae ilikua maeneo ya Mwenge alikuwa mwenyekiti wakati tunapokea mahari ya dada yetu,
ooh may your soul rest in peace...
 
Bebe Singili mhwala ahene?poleni sana na msiba uliowapata,Mungu awatie nguvu kipindi hiki kigumu.Namfahamu sana Prof Mabelya tangu akiwa Dr na baadae kuwa prof.Kwanza ingawa hakunifundisha maana nilisoma MUCHS lakini sio Dentistry,lakini tulifahamiana kama wana Bariadi na mara nyingi wakati wa likizo alikuwa akinituma pale Majahida kwa mzee Singili kwa ajili ya kufikisha salamu na mambo mengine.Pia mzee Singili namfahamu sana kwani mwaka 1997 nilikuwa nanunulia pamba kwenye ile nyumba yake.Poleni sana brother tuko pamoja.
 
Back
Top Bottom