Prof issa shivji kusaidiana na dr slaa wanafaa kuongoza tume ya katiba mpya

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
57
Kama jk anataka kweli kuondoa fitina na kulitakia mema taifa hili-basi watu hawa wawili wanafaa kabisa kwa vyovyote na kwa maslahi ya umma kuongoza tume ya katiba mpya.

1. Prof issa shivji amekuwa katika mchakato wa kudai katiba mpya kabla na baada ya mfumo wa vyama vingi. Sio mnafiki, hanunuliki kama wasomi wetu wengi -anayetaka ukweli asome raia mwema la wiki ya jana atapata ukweli huu kutoka katika makala yake. Hayumbishwi. Nampendekeza awe mwenyekiti wa tume hiyo

2. Dr w. P. Slaa ni mtanzania mwenye msimamo aliyesababisha chachu ya katiba mpya, kama ilivyo kwa shivji slaa(phd) hanunuliki na hayumbishwi. Ni mtanzania aliyekuwa anagombea urais agenda yake kubwa ya kwanza ikiwa ni kuanzisha mchakato wa katiba mpya. Ni mtanzania anayeona mbali na anayeitakia mema nchi hii, mwenye kuchukizwa na umaskini, ufisadi, ujinga, na maradhi ya nchi. Huyu anafaa kuwa katibu wa tume hii -aombwe ashiriki hatakama yeye mwenyewe hakubaliani na approach ya serikali ya jk. Lakini kwa jk kumuomba na kumtumia katika tume hii wote wawili watakuwa wameweka historia ya aina yake kwa maslahi ya umma.

Tunao watanzania wengine kama jaji kisanga,ulimwengu, ayoub lioba, amiri maneto, bomani -hawa wanaweza kutumika kama wajumbe pamoja na mama nkya, ila hoja kubwa ni kutaka watanzania wazalendo wa kweli -nilisikitishwa na tume ya bomani ya madini ambayo mpaka leo bado wizi wa madini unaendelea -ndio maana slaa(phd) hataki tume hizi kwa kuwa zinakuwa hazipo huru.

Haya ni maoni yangu na ninaamini wapo wana jf watakubaliana na mimi kwa kupitia reference ya tume zilizowahi kuundwa huko nyuma na matunda yake.
 
Siungi mkono uwepo wa mtu yeyote mwenye cheo cha kisiasa katika tume ya katiba, suala la katiba ni suala la Watanzania wote lisiolofungamana na itikadi ya mtu, kwa vyovyote vile vyama vya siasa ni wadau muhimu wa katiba na watahusika kwa namna zingine lakini katu isiwe kwenye uongozi wa tume hiyo..

Hivyo uwepo wa Dr. Slaa kama ilivyo kwa Yusufu Makamba na wenzake ni big NO.
 
Siungi mkono uwepo wa mtu yeyote mwenye cheo cha kisiasa katika tume ya katiba, suala la katiba ni suala la Watanzania wote lisiolofungamana na itikadi ya mtu, kwa vyovyote vile vyama vya siasa ni wadau muhimu wa katiba na watahusika kwa namna zingine lakini katu isiwe kwenye uongozi wa tume hiyo..

Hivyo uwepo wa Dr. Slaa kama ilivyo kwa Yusufu Makamba na wenzake ni big NO.[/QUO

Nakubaliana na wewe mkuu, wanasiasa hawatakiwi kuongoza tume hii, hili ni swala la linalohitaji watu ambao hawana upande
 
Tatizo au shida yangu kubwa ni hao wengine -very very few wanaweza kusimamia haki mbele ya pesa za mafisadi. Mi siamini kuwa slaa atavutia kwake wapi? Slaa ni sauti ya umma na akiwa kwenye jopo hili atakuwa amewakilisha umma siyo chadema. Hapa tunaangalia maslahi ya taifa na siyo ya chama. Tuna wasomi wengi wenye sifa za kisomi lakini ni mbwa mwitu na vigeu geu. Mimi bado naamini slaa as a person ni lulu ambayo haipaswi kuachwa pembeni.
 
Back
Top Bottom