Prof. Ibrahim Lipumba, anatupenda watanzania kipindi cha uchaguzi tu?

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Nimekua nikijiuliza kuhusu mwenyekiti wa chama cha wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba na tabia yake ya kuwakacha watanzania wakati wa matatizo kama haya tuliyonayo sasa na badala yake kujitokeza wakati wa uchaguzi mkuu tu; na kujifanya ana uchungu sana wa kuwakomboa watanzania kutokana na matatizo yanayowakabili.

Kila wakati uchaguzi unapokaribia tumekuwa tukishuhudia kujitokeza hadharani kwa Prof. huyu mahiri wa uchumi huku akiyasemea matatizo ya watanzani na kuahidi kuyatatua endapo angechaguliwa kuiongoza nchi. Lakini baada ya uchaguzi, huwa hatumsikii kiongozi huyu hadi uchaguzi mwingine unapokaribia.

Nilitarajia kumsikia na kumuona mwanasiasa huyu akiyasemea matatizo ya watanzania. Tunayo matatizo mengi sana ikiwa ni pamoja na kupanda kwa kasi kwa gharama za maisha na kuundwa kwa katiba mpya nchini.

Nilitarajia kumuona Prof. Lipumba kama mwanasiasa na mchumi mwandamizi akitoa mchango wake mkubwa katika maeneo hayo, lakini amekuwa kimya tangu uchaguzi mkuu ulipoisha.

Je ndio kusema kwamba Prof. Lipumba amewasusa watanzania kwa sababu nao walimtosa kwenye uchaguzi mkuu uliopita?
Au mchumi huyu ni mwanasiasa wa kipindi cha uchaguzi tu!?
 
''Enyi wanawake, watiini waume zenu nao watawapenda''

sio mimi, ni kitabu cha mnyazi Mungu!!
 
u will know a person by his action, hana jema na sisi lengo lao ni kugawa kura especially zile za kanda ya kusini.
 
Lipumba na cuf yake si ni Puppets wa magamba..unategemea nini hapo.
 
Jamani Lipumba yuko us alipata bahati kati ya maprofessor 360 duniani walio omba na kufanikiwa kuwa kati ya maprofessor 16 na yeye akishika nafasi ya 2, wapo shirika la uchumi la umoja wa mataifa wanashughulikia mtikisiko wa uchumi Duniani, usiwe na wasi wasi mwezi wa 2 atarejea baada ya kukamilisha kazi.
 
Lipumba yupo UN anapiga kazi za kimataifa, JK anaacha kumtumia kichwa prof. kama yule mpk UN wanamchukua, ama kweli Nabii hakubaliki kwao!
 
ila jamaa kichwa.. JK ilibidi ampe shavu hata la uwaziri wa uchumi., sema katiba hairuhusu ndo maana katiba mpya inahitajika ku utilize skills za wAtaalam kama hawa.
 
Lipumba yupo UN anapiga kazi za kimataifa, JK anaacha kumtumia kichwa prof. kama yule mpk UN wanamchukua, ama kweli Nabii hakubaliki kwao!

Kuwa nchi nyingine kunamzuia vipi mtu kujadili masuala ya nchi yake?
 
Hana mamlaka yeyote ya kiutendaji kwa hiyo aseme asiseme watanzania hawatafaidika kwa lolote.
 
Wanasubiria chadema watoe elimu ya uraia alafu wao waje waombe kura
hahahaa watapata moja au mbili tu
 
Back
Top Bottom