Prof. Ibrahim Haruna Lipumba for BoT governor

Wakuu hii nimeinyofoa Wikipedia sijaona sehemu wamelezea aliwahi kuwa mshauri wa uchumi Uganda.

Maisha ya Mwanzo na ElimuMh. Lipumba alizaliwa tar. 6 Juni Mwaka 1952, katika kiji cha Ilolangulu Wilaya ya Tabora Mkoani Tabora Tanzania. Ameanza elimu ya msingi 1959 - 1962 katika shule ya msingi ya Swedish Free Mission Primary School, Sikonge 1962 - 1966 : L.A Upper Primary School, Sikonge
baadae kuendelea masomo na Elimu ya Sekondari 1967 hadi1970 Tabora Boys Secondary School 1971 hadi 1972 Pugu Secondary School Kisha Elimu ya Chuo Kikuu 1973 hadi 1977 University of Dar es Salaam 1978 hadi 1983 Stanford University. Akapata Shahada BA (Hon.Economics) University of Dar es Salaam 1976 MA (Economics) University of Dar es Salaam 1977 MA (Economics) Stanford University 1979 Phd (Economics) Stanford University1983
[h=2][hariri] Uzoefu wa Uongozi[/h]Aliwahi kuwa mweka hazina wa Umoja wa Vijana Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970 pia akawahi kuwa Katibu mkuwa wa Kikundi cha Majadiliano cha Tabora Boys Secondary School toka mwaka 1969 hadi 1970, baadae akaja kuwa Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Vijana katika shule ya pugu Secondary School hiyo ilikuwa mwaka 1970 hadi 1971, baadae akaja kuwa tena Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam toka mwaka 1975 hadi 1976. na pia ndiye Mwanzilishi na Rais wa Kwanza wa Stanford African Students Association (SASA), Stanford University; Stanford, California USA hiyo ilikuwa mwaka 1978.
[h=2][hariri] Kazi[/h]
  • 1976 hadi 1977 Mkufunzi Msaidizi (T.A)
  • 1977 hadi 1983 Mhadhiri Msaidizi
  • 1983 hadi 1986 Mhadhiri
  • 1986 hadi 1989 Mhadhiri Mwandamizi
  • 1989 hadi 1993 Profesa Mshiriki
  • 1991 hadi 1993 Msaidizi wa Rais Mambo ya Uchumi
  • 1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professor, Williams College, Massachussets, United States of America
  • 1996 hadi 1998 Senior Research Fellow, United Nations University, World Institute of
Economic Research, Helsinki Finland.
[h=2][hariri] Heshima za Kitaaluma[/h]
  • 1993 hadi 1995 Fulbright Visiting Professorship
  • 1986 hadi 1989 Kellogg International Fellow in Food Systems
  • 1977 hadi 1983 Rockefeller Foundation Fellowship
  • 1976 Zawadi ya Mwanafunzi Bora, Best Student
Award, Faculty of Arts and Social Sciences,University of Dar es Salaam.
[h=2][hariri] Mshauri wa Uchumi[/h]
[h=2][hariri] Shughuli za Kimataifa[/h]
Lipumba akiwa kwenye shughuli za Kimataifa

Utafiti kuhusu kushiriki kwa nchi za kusini katika mfumo wa biashara wa kimataifa, Uruguay Round Multilateral trade negotiations kuanzia mwaka 1986 ha 1990. Utafiti kuhusu sera za kilimo za nchi zinazoendelea. Kuwasilisha maelezo (Testmony) kuhusu matatizo ya madeni ya Afrika kwenye kamati ya Bunge la Marekani - House Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - February, 1994.
Kuwasilisha, maelezo (Testmony) kuhusu shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na uhusiano wake na nchi masikini kwenye kamati ya Bunge la Marekani House - Sub Committee on International Development, Finance, Trade and Monetary Policy - April, 1994
Kutayarisha "Report of Group of Independent Advisers on Development Cooperation issues between Tanzania and Aid Donors". June , 1995
Kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya sera ya maendeleo (member of the United Nations Committee for Development Policy (1995 hadi 1999.)
Kutayarisha vigezo vya kuainisha nchi masikini sana duniani. (The list of Least Developed Countries (1997 na 2000)
Kutayarisha na kuratibu utafiti na kupendekeza sera za viwango vya kubadilishana sarafu (exchange rate policy) na sera za kulegeza masharti ya mfumo wa fedha (financial liberalization) Kampala, Uganda (1997).

Kutoa taarifa katika Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mambo ya uchumi na maendeleo (ECOSOC) kuhusu mgogoro wa kimataifa wa fedha katika nchi za Asia, NewYork (1998).
Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Windhoek, Namibia (1998).
Kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha muundo na sera za fedha, Wizara ya Fedha, Mbabane, Swaziland (1998).
Kutathmini maendeleo ya ‘The Macroeconomic And Financial Management Institute Of Eastern And Southern Africa', (MEFMI) ili kuwasaidia wahisani kufanya maamuzi juu ya kuendelea kuisaidia taasisi hiyo,1998.
[h=2][hariri] Shughuli za Kitaifa[/h]
  • Mjumbe - Kamati ya kurekebisha mashirika ya umma, 1992 - 1993
  • Mwenyekiti - Tume ya kuchunguza matatizo ya chama cha ushirika cha mkoa wa Shinyanga (SHIRECU), 1992
  • Mwenyekiti - Tume ya Waziri wa Fedha ya kuchunguza matatizo ya Shirika la Bima (NIC) 1993
[h=2][hariri] Baadhi ya Tafiti za Uchumi na Maandishi Muhimu[/h]
  • Stabilization Policies in Tanzania, University of Dar es Salaam, 1984
  • African Unity, Some Practical Guidelines, MAWAZO Vol. 1. No. 2, May 1983. Published by Stanford African Students Association.
  • Problems and Prospects of African Economic Integration , MAWAZO Vol. 1. No. 1, April 1982.
 
Issue sio Lipumba au serikali ya mseto, issue ni uongozi mbovu wa serikali ya magamba. Hapa ili kulete maendeleo ya nchi hii ni kuondoa magamba yote na kuwa na serikali inayojali uwajibikaji. Unadani kukiwa na serikali ya mseto halafu RAHISI ni Mkwele kipi kitabadilika? Ni kuondo mafisadi wote waje watendaji ambao sio wababaishaji
 
NJAA INAMSUMBUA HUYO ANATAFUTA ULAJI BOT,NDIO MAANA AKAAMUA KUUA UPINZANI ZANZIBAR KWA KUKUBALI CHAMA CHAKE KIOLEWE NA MAGAMBA

huyu ni njaaa kali hakuna lolote
 
nilivutiwa na uelewa wake jinsi alivyokuwa akijibu hoja nadhani ni mtu muhimu kumtumia kama Taifa kwa maendeleo yetu na mustakabali wetu!
 
Mtu yeyote makini anajua fika Prof Haruna Lipumba ni mchumi mahiri sana na wachumi wote sio tu wa huko Tz bali dunia nzima inamtambua.

lakin siku zote nabii huwa hathaminiki kwao.

IMF sasa wanamtumia kama alivyowasaidia waganda.
 
Jamani hivi vitu vya uchambuzi wa kutumia natharia (theory) mtu kama ni mzuri wa kujieleza anaweza akateka dunia nzima, ila linapokuja swala la ku-fuse theory and practice, hapo ndipo kazi ipo na hapo ndio watu hupewa credit za ukweli...Mfano kuna mwana jamii moja katukumbusha kuwa Prof. alikua Lipumba alikua mshauri wa Rais Mwinyi ila mambo nayo hayakua mazuri..nae (Lipumba) alijitokeza wazi akasema sasa unaposhauri mambo mazuri alafu hayafanyiwi kazi, unategemea nini kitokee?? Mh. Godon Brown alie kuwa waziri mkuu wa wingereza, wengi walikua wakimsifu kuwa ni kichwa na angeweza kuingoza Wingereza vizuri, ili kilichompata enzi za uongozi wake kila mtu anakijua...Kwa mfumu huu wa serikali yetu hata akija DSK hakuna kitakacho badilika, kwasababu wataalamu wanashauri vizuri ila wanasiasa wanafanya vingine ili kujitajirisha wao na wala sio nchi.

Kwa hiyo tukae hivihivi kwa vile wanasiasi wanafanya vingine. Hii inakuwa ni dalili mbaya ya kushindwa. Mi nahisi mabadiliko ni chachu ya maendeleo. Tunamuweka mtu akiharibu tunatoa
 
Hivi mathalani Prof Lipumba anakuwa Governor wa BoT wakati huo huo JK and his cronies wanaendelea
ku-loot pesa zetu kama EPA, majengo pacha ya BoT, Kagoda, Meremeta, Richmond etc. Wakati huo huo
dhahabu yetu inaendelea kusafirishwa nje with nothing badala ya kukuza uchumi wetu. Huyo Lipumba atasaidia nini?

Kwanini watanzania hamtaki kukubali UKWELI mchungu na badala yake mnaziba viraka kama KATIBA yetu.

The root causes of all of this is CCM, Without voting them out CCM we are doomed. Tumeona watu waadilifu
walipoingia kwenye system ya CCM wameishia kuwa manyang'au Mfano mzuri ni CAG Utoah wakati alipokuwa NBAA
au Marehemu Balali wakati yuko Washington DC, they miserably failured when they came to work under CCM government.

The best example ni huko Zanzibar hivi SUK imefanya nini cha maana. Tuondoe cancer (CCM) inayotafuna nchi yetu sio
kupiga piga mionzi!
 
My friend FJM,

Tofautisha kuwa mtendaji na kuwa mshauri. Unaweza kuwa mshauri mzuri lakini aliyeko kwenye nafasi ya utekelezaji akafanya kinyume cha kile ulichoshauri. Ndicho kilichotokea wakti wa Rais Mwinyi. Ushauri wa Prof. Lipumba haukuwa ukizingatiwa, Remember the same Prof. Lipumba wa hired by Yoweri Kaguta M7 to advice on Uganda's economy. Uganda economy propels with a supersonic speed when the Prof's ideas and advices were implemented accordingly.

IMF wanajua nini Prof. Lipumba alifanya kwa Tanzania na Uganda na ndiyo maana wamemchukua yuko IMF Headquarters anakula kuku maana wanajua ni kichwa siyo mkia.

Very good. sasa wewe unalala, unaamka, unarudi kulala, unaamka tena na bado umeendelea kuwa na imani
kwamba Kikwete anashaurika. kama mwinyi hakumsikiliza Lipumba Kikwete sio kwamba hatamsikiliza yeye
hatokuwapo kabisa wakati anaongea atakuwa zake tour USA.

Na naomba tusipotezeane focus. The focus ni kuiondoa CCM period. Chama hiki hata akirudi Mwenyenacho
(Mwalimu) hawezi kukikubali hata akiambiwa awe mwenyekiti wake milele.

Kimeshindwa kutengeneza serikali imara, sasa hakina hata watu imara, hiki ndio mchawi wetu.

Watanzania tuunganishe nguvu zetu kufanya kazi hii kwa uwezo wetu wote, kuindoa CCM ndio
Jambo pekee tunaloweza kujivunia wakati wa uzee wetu.
 
JUzi ya Kiswahili nilisoma mawazo kama haya unayoyatoa hapa Makoye2009

Cuf wataka serikali ya umoja wa kitaifa bara.

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Serikali yatamalizwa kwa kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. CUF imesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeelemewa na majukumu ya kuongoza na hivyo kuhitaji msaada kwa kuundwa serikali hiyo kama ilivyo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, visiwani.

“Baraza Kuu linaona njia pekee ya kulitoa taifa hapa tulipofikishwa ni kwa rais Jakaya Kikwete na CCM kukubali kusaidiwa dhamana ya kuongoza nchi kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Ali.

Aliongeza kuwa hatua hiyo pia itaisaidia nchi kuvuka salama katika mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo itasaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo. Ali alisema serikali ya CCM imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuongeza kuwa tatizo la nishati hiyo linachangiwa na kuingizwa siasa na si utaalamu au rasilimali fedha.

Cuf wataka serikali ya umoja wa kitaifa bara

CCM na Serikali yao wanapewa ushauri mwingi tu ambao utaipesha TZ kuingia katika umwagaji damu lakini hawaonekani kuwa wanaona hatari inayolikabili taifa hili. Kwa hali inavyoendelea ya "maisha bora kwa kila mtanzania" na ubabaishaji unaofanywa wa kuleta katiba mpya au katiba viraka au kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi kuna dalili mbaya kwa siku zijazo.

Nonda well said.

Sijui ni wangapi wanaokubaliana na mawazo haya linapokuja swala la uzalendo na mstakabali wa Taifa letu.
Mwana Halisi ya jana inasema Vyama vya Siasa havijapata Ruzuku ya kila mwezi toka Serikalini, na gazeti moja hivi juzi lilisema Wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM Dar hawajapata mishahara ya mwezi wa 10. Lakini alipoulizwa Nape akasema kwanza ndiyo anasikia habari hiyo!!!!Sasa akanushe na hili la Ruzuku. Hii inathibitisha kuwa madai ya wafanyakazi ni sahihi maana ruzuku haijatoka.

Lakini kwasababu tu ya UTASHI WA KISIASA WA CCM AMBAO NI WA KIPUMBAVU NA KIJINGA,Nape anakanusha siyo kweli. Sasa hii longolongo ya wanasiasa wa Magamba itapelekea hii nchi kulipuka. Nape ajue kuwa haohao wana-CCM kesho watamkuta akiwa amejificha kwenye Daraja la Sarander Bridge akikimbia mkono wa Peoples Power kama alivyofanya marehemu Babu yake Muammar Ghadafy.

Kwa kweli kauli ambazo huwa zinatolewa na viongozi vichaa wa CCM hata kwenye jambo la wazi na la msingi zinatiaga kichefuchefu. I hate all CCM leaders and thy members. They can go to HELL!!!
 
Hivi mathalani Prof Lipumba anakuwa Governor wa BoT wakati huo huo JK and his cronies wanaendelea
ku-loot pesa zetu kama EPA, majengo pacha ya BoT, Kagoda, Meremeta, Richmond etc. Wakati huo huo
dhahabu yetu inaendelea kusafirishwa nje with nothing badala ya kukuza uchumi wetu. Huyo Lipumba atasaidia nini?

Kwanini watanzania hamtaki kukubali UKWELI mchungu na badala yake mnaziba viraka kama KATIBA yetu.

The root causes of all of this is CCM, Without voting them out CCM we are doomed. Tumeona watu waadilifu
walipoingia kwenye system ya CCM wameishia kuwa manyang'au Mfano mzuri ni CAG Utoah wakati alipokuwa NBAA
au Marehemu Balali wakati yuko Washington DC, they miserably failured when they came to work under CCM government.

The best example ni huko Zanzibar hivi SUK imefanya nini cha maana. Tuondoe cancer (CCM) inayotafuna nchi yetu sio
kupiga piga mionzi!

Bobuk,

Mawazo yako ni msumari rafiki.

Kwa hali tuliyo nayo kwasasa rafiki is very critical economically to say! HAIHITAJI KUANZA KUFIKIRIA NAMNA YA KUING'OA CCM kwasababu is already too late! Leo tuna almost more than 20 years tangu upinzani uanze lakini BADO CCM WAMENG'ANG'ANIA KWENYE MADARAKA KWA NGUVU NA HAWATAKI KUACHIA! Kwa hiyo hiki tunachozungumzia kwasasa ni kutaka kujaribu kuokoa Uchumi wetu unaoporomoka kwa kasi ya ajabu sana! Gharama za maisha ziko juu,bei ya mahitaji muhimu km vyakula,umeme,mafuta n.k viko juu. Dollar kwa sasa inakimbilia kwenda kwenye Tshs 2,000/= kwa Dollar.

Ripoti ya UN inasema bei ya vyakula inaenda kuwa dabali(double) katika siku chache zijazo pale Dollar 1 itakapofikia Tshs.2,500/=! Maisha yatakuwa hayakamatiki hasa kwa Watanzania wenye kipato cha chini. Vigogo hawatahusika na hali hii kwasababu tumeamua kuwakabidhi kodi yetu waitumie wanavyotaka na hakuna wa kuwauliza. Si Kiwete wala si Mkullo wala Benno Ndulu wanaoweza kutuepusha na balaa hili kwasasa kwa vile kila kitu tayari kimeshaparaganyika.

Kiwete na CCM yake anapaswa kufikiria mara mbili ili aweze kunusuru Uchumi wa Nchi yetu vinginevyo anaenda kuadhirika na CCM yake. Na hali ikifikia huko si ajabu akalazimika kukubali USHOGA ili kunusuru hali mbaya ya kiuchumi.
 
Wakuu hii nimeinyofoa Wikipedia sijaona sehemu wamelezea aliwahi kuwa mshauri wa uchumi Uganda.

Source: Gazeti la MWANANCHI la Tarehe 26.Agosti,2010.
CUF yazindua ilani 'ya elimu, matibabu' Send to a friend
Thursday, 26 August 2010 23:36
0diggsdigg

Elias Msuya

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimezindua Ilani yake ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ikisema kuwaq iwapo itapewa ridhaa ya kuongoza nchi kitarejesha mpango wa kutoa bure huduma za elimu na matibabu kwa wananchi wote.

CUF, ambayo katika chaguzi mbili zilizopita ilikuwa ikishika nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa rais na kuwa na idadi kubwa ya wabunge, pia inazindua kampeni zake leo kwenye viwanja vya Kidonge Chekundu jijini Dar es salaam.

Akizindua ilani hiyo inayokwenda na kauli mbiu ya "Dira ya Mabadiliko", mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba alisema lengo la kurejesha mpango huo wa kutoa elimu na matibabu bure unalenga kuboresha kiwango cha elimu na pia kuimarisha afya wananchi.

Kwa sasa elimu inatolewa kwa kuchangia sehemu ya gharama na hali ni mbaya zaidi kwenye vyuo vya elimu ya juu ambako wanafunzi huchambuliwa uwezo wao kwa kutumia mfumo maalum kabla ya kuelezwa kiwango ambacho wanatakiwa kuchangia.

Awali, huduma za elimu na matibabu zilikuwa zikitolewa bure na serikali, lakini tangu katika ya miaka ya tisini, ilipitisha mpango huo wa kuchangia elimu ambao umekuwa ukiibua migogoro ya mara kwa mara.

Lipumba alisema kuwa katika kutekeleza ilani hiyo, atahakikisha huduma za elimu na matibabu zinatengewa asilimia 50 ya bajeti yote, akifafanua kuwa elimu itatengewa asilimia 25 hali kadhalika matibabu.

"Kila mwanafunzi atapata laptop (kompyuta ndogo) bure," alisema Prof Lipumba, ambaye aliwahi kuwa mshauri wa kiuchumi wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

"Tutaimarisha matumizi ya mtandao wa internet (mawasiliano ya kompyuta) na kila mwanafunzi atapata laptop yake. Haya yanawezekana na kuna kampuni moja ilishatangaza uwezekano wa kuunda kompyuta kwa gharama nafuu."

Kuhusu huduma za afya, Lipumba alisema serikali yake itahakikisha inaimarisha huduma ya afya ya msingi na kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Lipumba, ambaye anawania urais kwa mara ya nne baada ya kushindwa mwaka 1995, 2000 na 2005, alisema CUF pia imepania kuondoa utegemezi kutoka kwa nchi wahisani.

"Rais (Jakaya) Kikwete anajisifu kwa kuifanya nchi yetu kuwa matonya wa kimataifa... tumekuwa ombaomba. Nimemsikia kwenye kampeni zake huko Mwanza akijisifu eti yuko karibu na rais wa zamani wa Marekani, George) Bush na wa sasa, Barack) Obama," alisema.

"Nitaingia madarakani kupunguza tabia ya nchi kuomba misaada na mikopo kutoka kwa wahisani.

Mtaalamu huyo wa uchumi alisema nchi inakabiliwa na matatizo mengi na kunukuu ripoti ya serikali ya utafiti wa bajeti kwa kila kaya ambayo alisema inaonyesha kuongezeka kwa umaskini,

"Ripoti ya Household Budget Survey inaonyesha kuwa maskini wa kutupwa wameongezeka kutoka 11.4 milioni mwaka 2001 hadi kufikia 12.9 mwaka 2007. Hizi ni ripoti za serikali siyo za CUF," alisema.

Alitaja pia tatizo la ajira ambalo alisema kuwa licha ya kuwa na nguvu kazi ya watu 21 milioni, ni Watanzania 900,000 tu walioajiriwa viwandani huku watu wengi wanaodaiwa kupata ajira ni wale waliojiari kwenye kazi dhalilifu kama uokotaji wa chupa za plastiki.

Aliibeza kauli mbiu ya CCM ya mwaka 2005 ya "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" akisema kuwa badala ya kuwa na maisha bora yamekuwa maisha bomu.

"Mwaka 2005 bei ya sukari ilikuwa Sh600 sasa ni Sh1,600 hadi 1,700; sembe ilikuwa Sh250, sasa imepanda hadi Sh800; mafuta ya uto yalikuwa Sh700 kwa lita, sasa Sh2,000; mchele ulikuwa Sh350 kwa kilo sasa umefikia Sh1,200. Kwa hiyo gharama za maisha zimepanda mno. Ile kauli mbiu ya "Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi" inamaanisha 'Anguka'," alisema Lipumba.

Prof Lipumba pia alitaja tatizo la katiba kuwa linaifanya nchi ikose misingi ya kidemokrasia hasa baada ya majaji wa Mahakama ya Rufani kupora haki ya wananchi ya kuwa na mgombea huru.

Alizikosoa hata mahakama za mwanzo kwa kushindwa kuwapa haki wananchi badala yake wakinunua haki hizo na mara nyingine kubambikizwa kesi.
Profesa Lipumba alisema pia kwamba serikali itatoa huduma za elimu na afya bure kwa kuzipangia asilimia 25 kila moja kwenye bajeti ya serikali.

Lipuma pia alisema ataimarisha kilimo kwa kukiwekea asilimia 15 hadi 20 katika bajeti ya serikali yake wakati miundombinu itapata asilimia 15 hadi 20 na huduma nyinginezo asilimia 20 hadi 25.
Aidha Lipumba alionyesha kushangazwa na serikali kushindwa kutumia bahari inayozunguka nchi,

"Nchi yetu ina bahati ya kuwa na bahari zinazofanya biashara ya kimataifa kuwa nafuu kwetu. Tuna bandari za Zanzibar, Tanga, Mtwara na Zanzibar. Tumezungukwa na nchi sita zisizo na bandari, lakini kutokana na mfumo mbaya wa biashara, nchi hizo zinahamia bandari za nchi nyingine. Congo wanashushia mizigo yao Afrika Kusini. Rwanda wanashushia Mombasa," alisema.

Lipumba alisema kuwa serikali yake itahakikisha kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia nane hadi tisa kwa mwaka
 
Mkuu Makoye.

Haya magazeti ya Bongo yamejaa ukasuku au umesahau yaliwaaminisha waTanzania JK ni mwarobaini wa matatizo ya wananchi.Mara ngapi yamepotosha wasomaji wake.Nitajie mwaka Lipumba alikuwa Uganda ?.

Source: Gazeti la MWANANCHI la Tarehe 26.Agosti,2010.
CUF yazindua ilani 'ya elimu, matibabu'
Send to a friend

..Hata Prof.Ndulu naye alikuwa World Bank.

..Dr.Daudi Balali naye alifanya kazi IMF kwa miaka 20++ na amezishauri nchi nyingi za Kiafrika kuanzia Ghana,Ethiopia,etc etc.

..kilichomtokea Balali baada ya kurudi Tanzania na kuongoza Benki yetu wote tunakijua.

..ukifanya kazi na mafisadi wa CCM bila shaka na wewe utachafuka, na utakuwa na mwisho mbaya sana.
 
hana sifa za kuongoza-huoni kila siku CUF inazid kuporomoka
akipewa bot nayo ndani ya muda mchache kila kitu kitaharibika
 
Back
Top Bottom