Prof. I. Lipumba: Vyama Vya Upinzani Kuaandaa Maadamano Nchi Nzima Kumshinikiza JK Kuchukua Hatua.

wamemiss virungu na maji ya kuwasha...ila itapendeza kama kwenye hayo maandamano viongozi ndio watakuwa mbele.

Tahariri square style!hata risasi za moto ziwepo,tena ndio zitazidisha hasira kutoka kwenye kutaka uwajibishwaji wa wezi mpaka kuondoa anaekumbatia wezi!na tutafunga airport,bandari na road,hakuna kukimbia mtu mpaka tuwahukumu kwa dhambi walizofanya!
 
Kuna ubaya kama wakishiriki kwenye hili? Naamini hata wewe utakuwepo maandamano yakiiva.

kwa hiyo Ritz wewe ndio unawasemea C.d.m au ni uoga ndio umewajaa?mimi ni c.d.m damu lakini kwa ili kwa kua ni maslahi ya taifa,na cuf na cdm wameonyesha ushirikiano,mimi nasubiri tamko tu nishiriki
 
CUF hawana lolote siwameolewa na Magamba' CCM, wasituharibie CDM yetu hawa jamaa, wao wameunda serekali waliyoipa jina la umoja wa kitaifa na CCM sasa hayo ya maandamano wanayatoa wapi? Wanafiki tu hao CUF, wakadai talaka kwanza ndo warudi.
 
Na kwa hiyo yatakuwa maandamano ya vyama vyote maana CCM itawakilishwa na CUF.
Siasa kweli kazi, wataalamu wetu msitoke kwenye fani zenu kukimbilia siasa maana ni maigizo.
Mbona unaingilia mambo ya nchi nyingine ambayo ni Tanganyika na wakati wewe upo kwenye nchi yenu ya Zanzibar hatutaki ushauri wako kwenye taifa letu wakati nyie mna matatizo kibao!!!!!!
 
Maandamano sawa kabisa..........Nitasikitika sana nikimuona Jusa ndani..............Jusa sio tu hafai kuitwa Mtanzania bali hata Mzanzibari................
 
Akihojiwa na Ch.10 amesema ameshapokea mapendekezo kutoka kwa wananchi mbali mbali na kwa sasa wanafanya mpango wa maandamano ya nchi nzima yatakayoshirikisha vyama vyote vya upinzani ili kumshinikiza "the so called president" yaani "JK" kuwachukulia hatua mawaziri wabadhirifu wa mali za umma. Hili naliunga mkono kwa asilimia mia.


Source: Taarifa ya Habari Ch.10.

MV spice ilipozama sikumsikia lipumba akitaka kuwajibika kwa waziri husika ambaye ni wa CCM B aka Cuf. Lakini wakati wa mabomu ya Gongolamboto na Mbagala alimtaka waziri wa ulinzi (mwinyi wa CCM) ajiuzuru. Cuf hawana nia ya dhati ya kuikomboa nchi, ni wasanii kama alivyo huyo kiwete wa akili
 
Ya CUF huhitaji shahada ya siasa au utafiti kubaini kuwa kuna kitu Maalim SHERRIF alikitaka Zanzibar na kibinafsi-kama watu wa kizazi chake waliokuwa nyaye CCM,amekipata nacho ni CHEO.Hawa CUF wengine wanaoendelea kupambana wameshagundua waliuzwa long time kwa mazungumzo ta faragha kati ya Sherrif na Amani Karume,mwakumbuka?Sasa Mwenyekiti Fullbright Prof Ibrahim Lipumba kaachiwa boti inayoweza kuzama na ni juu yake kuona kuwa haizami.So hili ni somo lingine,lakini maandamano yoyote duniani yanahitaji uongozi madhubuti na mikakati madhubuti kama nguzo ya msaada.Nguzo ya kati ya maandamano ni maono, umoja,KUJIKANA na KUJITOA MHANGA kwa waandamanaji.Mnawakumbuka wanafunzi wa SOWETO mwaka 1976 kwenye historia?
 
wamemiss virungu na maji ya kuwasha...ila itapendeza kama kwenye hayo maandamano viongozi ndio watakuwa mbele.
Wakati virungu vitakapowageukia na wenzako ndipo utakapojua kuwa pombe si chai.. kaa mkao wa kula na siku yaja na haipo mbali.

Kwa kukukumbusha tu ni kwamba siku zote viongozi wamekuwa mbele kwenye maandamano.
 
Sababu kubwa Chadema wanasema CUF ni CCM B sasa kuna maandamano hapo kama yatakuwepo Chadema hawawezi kushiriki.

Haya ni masilahi ya Taifa sio masilahi ya Chama, njoo ushiriki hata kama wewe ni CCM, PPT Maendeleo au SAU
 
Prof. Lipumba amesema yatafanyika maandamano makubwa ya nchi nzima ya kuishinikiza serikali iwawajibishe mawaziri wake wanaotuhumiwa na ufisadi."
kama jambo hili litafikiwa je litaonesha taswira gani ya mwelekeo wa kisiasa hapa nchini.!!?

Tunashukuru Mh. Prof. Dr. Ibrahimu Lipumba kaja na moto mpya kama ataendelea hivyo basi CUF itarudisha integrity kwa waTZ.
 
Sababu kubwa Chadema wanasema CUF ni CCM B sasa kuna maandamano hapo kama yatakuwepo Chadema hawawezi kushiriki.

nilijua tu yaani mawazo yako kama ya nape,hujasikia kuwa kwenye swala la kutokuwa na imani na pm tumechukua hadi sahihi za wabunge wa ccm,ni hivi kwenye masilahi ya taifa cdm tunashirikiana na yeyote ili mradi aonyeshe dhamira ya kweli.msalimie nape
 
Rais Kikwete,

UFISADI wa mawaziri wako kwa kutukwapulia kodi kwa ma-bilioni kila mahali wala SI UPEPO WA KUPITA kwa jinsi unavyoonekana kudhania.

Hakika ukweli wa mambo ni kwamba huu UFISADI WA KUTISHA katika historia ya nchi hii ni UPEPO WENYE PEPO BAYA YA KUPITA NA MAFISADI WOTE kila mhali.

Hadi hivi sasa swala hili nyeti la kutakiwa Mawaziri MAFISADI 8 pamoja na Waziri Mkuu kujiuzulu ni mambo ambayo tayari CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na TLP tumeshazifikisha katika MAHAKAMA YA UMMA usiokua na hongo, hofu wala upendeleo.

CCM hivi sasa subirini hukumu yenu juu ya madhambi haya yote mnayoendelea kufunikiana kule bungeni na kote serikalini. Wananchi tuna hasira ile mbaya juu ya haya!!!


Prof. Lipumba amesema yatafanyika maandamano makubwa ya nchi nzima ya kuishinikiza serikali iwawajibishe mawaziri wake wanaotuhumiwa na ufisadi."
kama jambo hili litafikiwa je litaonesha taswira gani ya mwelekeo wa kisiasa hapa nchini.!!?
 
Back
Top Bottom