Prof. I. Lipumba: Vyama Vya Upinzani Kuaandaa Maadamano Nchi Nzima Kumshinikiza JK Kuchukua Hatua.

melxkb

JF-Expert Member
Sep 11, 2010
206
56
Akihojiwa na Ch.10 amesema ameshapokea mapendekezo kutoka kwa wananchi mbali mbali na kwa sasa wanafanya mpango wa maandamano ya nchi nzima yatakayoshirikisha vyama vyote vya upinzani ili kumshinikiza "the so called president" yaani "JK" kuwachukulia hatua mawaziri wabadhirifu wa mali za umma. Hili naliunga mkono kwa asilimia mia.


Source: Taarifa ya Habari Ch.10.
 
Prof. Lipumba amesema yatafanyika maandamano makubwa ya nchi nzima ya kuishinikiza serikali iwawajibishe mawaziri wake wanaotuhumiwa na ufisadi."
kama jambo hili litafikiwa je litaonesha taswira gani ya mwelekeo wa kisiasa hapa nchini.!!?
 
Hayo maandamano sidhani kama Chadema watakubali kushiriki...
 
Safi sana wadau tunataka jk awaadabishe hao wezi anaowafuga hakuna cha upepo hicho ni kimbunga lazima kiondoke na mtu kama hataki basi kitaondoka na waziri mkuu.
 
asante kwa taarifa, ila haitasaidia labda muondoe kubwa la maadui.
 
Natamani yawe ni maandamano ya kumwondoa JK madarakani. Chadema wakubali tu kushirikiana na vyama vyote vya siasa kumuondoa JK madarakani halafu akishaondoka waongoze nchi kwa style ya sharing of power. Wanakubaliana tu, kati ya Slaa au Lipumba, mmojawapo awe Rais na mwingine awe waziri mkuu. Ukiangalia uwezo wao wote wanaonekana wanafaa kwa nafasi yoyote. Tena vizuri.
 
wamemiss virungu na maji ya kuwasha...ila itapendeza kama kwenye hayo maandamano viongozi ndio watakuwa mbele.
 
wanatakaochaguliwa wapya watatoka chama gani vile?

Movie Director wa Tandale.
 
ni muda muafaka na ishara njema kwa vyama vya siasa kuunganisha nguvu na kuweka mbele maslahi ya taifa kwanza kabla ya vyama vyao na kujenga imani kwa watanzania walio wengi kuwa vyama ya upinzani viko makini katika kusimamia mabo ya msingi na kupingana na kila aina ya dhuluma na ufisadi ambao unapelekea wo kuishi maisha ya kubahatisha. kwa cdm ni turufu kwani usahiba wao unaweza kuwasaidia kuingoa ccm madaarakanikwa urahisi zaidi kwa pandee zote mbili za muungano. japokuwa kwa cuf naona kunaviongozi 2 tu kwa upande wa bara pro lipumba na julius mtatiro. kwa upande mwingine naona hii inaweza kuwaadvantage kwa cdm kupenya maeneo cuf yenye ushawishi mkubwa kwa mgongo wa opposition partinesrship, na hii ni kwa sababu cdm wana viongozi wengi wenye ushawishi mkubwa wa siasa za majukwaani kama G lema, sugu mnyika kabwe, nassari, mdee, kakunguru ben sanare etc. pia ni wakat mzuri kwa viongozi wa TLP nA nccr kujitambulisha kwa wananchi katika sehemu mbalimbali za nchi. pamoja na hayo naona ni wakati mzuri kwa vyama hivi kuendelea kuvuna wanachamana viongozi kutoka ccm na kujiongezea nguvu kama mataji kwa ajili ya chaguzi zijazo. washikane katika hoja hizi za kitaifa. Pamoja tutafika!
 
Sidhani kama CUF ni wapinzani kwa sababu wapo madarakani tayari

nakuunga mkono, kwani cuf watatumia hii opportunute ya CHADEMA popularity kujinufaisha kisiasa so ni vyema Viongozi wa CDM wakaliangalia hili swala kwani cuf sio wapinzani hata kidogo kwani wana sera za ubaguzi pia cuf wameshaona jinso chadema inavyoweza kumobilize watu wengi kuliko wao so ni vyema chadema ikawa makini kuhus hili swala.
"FORGIVE YOUR ENEMIES BUT DONT FORGET THEIR NAMES" by kennedy.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom