Prof. Haroub Othman Afariki Dunia

Mungu mwenye enzi amlaze pema peponi kamanda. My condolence to his family and to all Tanzanians.
 
Hi guys kutoka Helsinki

MSIBA WA KUSHUTUA SANA
Mimi kama member wa UDASA-nimezipata habari za kifo cha professor-kupitia UDASA mails kwa mshituko mkubwa sana. Professor Othman alinifundisha pia alikuwa ni mshauri wangu katika mambo ya academic hasa hasa masomo yangu ya PhD. Alikuwa ni mtu wa watu, hana majungu, hana fitina, hana majigambo hata kama alikuwa ni professor wa kimataifa, he was a very humble person, he was the wisest person, I have ever met, alikuwa hakuulizi kabila lako, wala dini yako hata umri wako, alipenda kuheshimu watu wote wakubwa na wadogo. Nilipenda sana kumtembelea ofisini kwake kuongea kuhusu mambo mbali mbali ya Africa na dunia, hakuwa mchoyo wala mtu wa kujidai-PENGO HALIZIBIKI MAANA NI VIGUMU KUPATA MTU MWENYE C.V kama hii-maana hata chuo kikuu cha DSM wanalijua hili- wakubwa wanataka kukaa juu na wadogo wakaa chini lakini professor Haroub alikuwa tofauti kabisa-mungu muweke mahali pema peponi

Rest in peace!
Rest in Peace!

Frateline Kashaga
PhD student
Department of social policy
University of Helsinki-Finland
 
Jamani tunaomba kama kuna anayeweza kupata access ya CV yake ikijumuisha na machapisho yake atuwekee hapa ili tuendelee kumuenzi kwa kumsoma zaidi!
 
wekeni STICKY hii thread

huyu prof aliwagusa members wengi sana humu na ni muhimu mkampa heshima yake

its not a bid deal is it?
 
RIP Professor.

Nakumbuka akifundisha DS pale mlimani....acha bwana hata watu wa FoE wakati ule kwa jinsi tulivyokuwa hatuipendi DS lakini huyu Prof alikuwa akiifanya inoge ukiingia kwenye lecture zake. Alikuwa very very brilliant. Ni pengo kubwa sana kwa taifa.
Poleni sana familia na jamaa wa Prof, mnapenda lakini Mungu kampenda zaidi. Amani yake Mungu mwenye rehema iwafunike.
 
I have just been informed that the funeral will take place tomorrow noon in Zanzibar. Some young intellectuals are organizing to travel tomorrow to Zanzibar to join the family and other friends who are already there. There also plans to meet in the evening at the University of Dar-es-Salaam for a vigil in remembrance of our beloved Professor. Will keep you posted as soon as I get more information on these plans.
-------------------------------------------------------------------------------------------
Taarifa nilizozipata ni kuwa maziko/mazishi ni kesho alasiri huko Zanzibar. Baadhi ya wanazuoni tunajipanga kusafiri kesho kwenda kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki ambao wameshafika huko. Pia kuna mpango wa kukutana leo jioni hapo Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam kwa ajili ya mkesha wa kumkumbuka mpendwa Profesa wetu. Nitawapasha habari zaidi punde nikipata taarifa kamili kuhusu mipango hii.
-------------------------------------------------------------------------------------------

UDADISI: Rethinking in Action: Sad and Shocking News: Professor Haroub Othman Has Moved On
 
Last edited:
Huyu Hakika atakumbukwa kwa Mengi na Msimamo yake Imara katika Kutetea Demokrasia na kusema Ukweli, Umeacha pengo kubwa sana katika Comments zako katika Vyombo vya habari Tanzania, Mungu akujalie na Akupe Amani, Tumebakiwa na Watu wachche sana makini, Prof, Baregu, Shivji, na wengine wengi walio tayari kusema ukweli
 
Burian Professor Haroub Othman. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mahali Pema Peponi.
Utakumbukwa kwa mengi ndani na nje ya Tanzania na Zanzibar.
Ulikuwa msomi mahiri kutoka Tanzania Visiwani, ukiwa na mbongo zinazochemka.
Uliasisi harakati mbali mbali za kimapinduzi, bila woga wala hiana.
Ulikuwa mwana-mapinduzi mfuasi wa falsafa za Karl Marx usiyebadili msimamo, ukiwaunga mkono kamaradi Fedel Castrol, Che Gwivara na wanamapinduzi wengine.
Uliasisi Zanzibar Legal Services Centre; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Zanzibar.
Ulifundisha watanzania wengi waliopitia Chuo Kiuu Cha Dar es salaam; utaendela kukumbukwa na wengi.
Ulikuwa nguzo, maktaba na hazina ya hekima ya Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo (IDS) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kwa heri Prof.
Kwa heri Haroub Othman
Kwa heri kipenzi cha wanamapinduzi wengi.
 
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi.Ameni. Alikuwa mtu muungwana asiyependa makuu na mkweli kwenye masuala mengi bila kujaribu kuumauma ili amfurahishe mtu.We will miss you and miss leturers wa aina yako.
 
Du kweli kila mtu ana siku yake!Tangulia mwalimu Prof Othman,ulinifundisha DS,ni masikitiko sana umetutoka!
 
Mbona hata hatukusikia kama alikuwa mgonjwa? Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape wafiwa nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu kwao~*AMEN*~. Ahsante sana kwa michango yako mbali mbali katika nyanja za elimu, uchumi na siasa.
 
Mbona hata hatukusikia kama alikuwa mgonjwa? ....

Kwani lazima usikie, ukisoma kwamba hadi jana midnight alikuwa na afya njema na kuhudhuria sehemu sehemu na kwamba amefariki usingizini haitoshi?

Ulitaka kwenda kumjulia hali mnazi mmoja hosp kwanza ndo usikie habari za kifo?

Saida mpweke.

 
Kwani lazima usikie, ukisoma kwamba hadi jana midnight alikuwa na afya njema na kuhudhuria sehemu sehemu na kwamba amefariki usingizini haitoshi?

Ulitaka kwenda kumjulia hali mnazi mmoja hosp kwanza ndo usikie habari za kifo?

Saida mpweke.


Hukuwa na haja ya kuandika hayo uliyoaandika. Kama unajua amefariki ghafla au usingizini basi ungenifahamisha hivyo badala ya kuandika uliyoyaandika. Umauti huwafika binadamu kwa njia mbali mbali na siyo mpaka wawe wagonjwa, niliuliza ili kutaka kujua tu nini kilichomsibu hadi kufariki.
 
Oh MY GOD -- AM LOST FOR WORDS.WHAT A GREAT LOSS.GOD REST YOUR SOUL IN PEACE -PROF.EVEN THOUGH YOU HAVE GIVEN US SO MUCH WE WERE NOT READY FOR YOU TO LEAVE US.
HIS UNTIMELY DEPATURE IS A WAKEUP CALL TO US ALL." NEVER TAKE THINGS FOR GRANTED"
 
Back
Top Bottom