Prof David Mwakyusa ampoza Bw. Richard Kasesela kwa kumpa ujumbe wa bodi

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
mchuano mkali ulionekana kwenye siasa za Jimbo la Rugwe Mashariki baina ya Prof DAVID Mwakyusa dhidi na Nd. Richard Kasesela, ambapo baada ya chakachua ya hapa na pale , Prof.Mwakyusa akaibuka na ushindi mwembamba ambapo nd.Kasesela hakuridhika na chakachua ile , akaamua kukata rufaa kwenye Kamati kuu ya CCM, ambapo hata hivyo Mwakyusa akapenya na kutangazwa mshindi.

katika hali inayoonyesha kumpooza adui yake (kisiasa) leo kupitia vyombo vya habari , amemteua ndugu Kasesela kuwa Mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya Taasisi ya Mifupa MUHIMBILI, MOI, KUANZIA tarehe 10 Agosti,2010.

uteuzi huo umefanyika chini ya sheria ya MOI ya mwaka 1996, kifungu cha 5.

Je kwa kupoozana huko Mwakyusa atakua amevunja mpasuko wa kisiasa jimboni kwake, ambako kwa ccm , Kasesela ananguvu zaidi.
 
apppphhhhhhhhhhhhhhhewwwwwwwwwwww!!!!!!!!!!!! Siasa hizi aaaaaaagggggggggggggggghhhh!!!
 
Hongera sana Prof Mwakyusa kwa kuishi na NENO, mpende adui yako.
Once again Prof amescore a first,siasa si uadui na kwa kufanya hivyo anaondoa roho ya uadui katika jamii.
 
hongera richard

hii familia wana bahati sana maana naona dada mtu alipata ujumbe wa bodi ya TACAIDS juzi tu hapa... Mama Nyoni, Dr. Mwakyusa...hongereni sana kwa kuona hawa watu
 
Hongera sana Prof Mwakyusa kwa kuishi na NENO, mpende adui yako.
Once again Prof amescore a first,siasa si uadui na kwa kufanya hivyo anaondoa roho ya uadui katika jamii.
JF tumeishiwa mawazo kiasi hiki????????????????????????????????
 
mchuano mkali ulionekana kwenye siasa za Jimbo la Rugwe Mashariki baina ya Prof DAVID Mwakyusa dhidi na Nd. Richard Kasesela, ambapo baada ya chakachua ya hapa na pale , Prof.Mwakyusa akaibuka na ushindi mwembamba ambapo nd.Kasesela hakuridhika na chakachua ile , akaamua kukata rufaa kwenye Kamati kuu ya CCM, ambapo hata hivyo Mwakyusa akapenya na kutangazwa mshindi.

katika hali inayoonyesha kumpooza adui yake (kisiasa) leo kupitia vyombo vya habari , amemteua ndugu Kasesela kuwa Mmoja kati ya wajumbe wa bodi ya Taasisi ya Mifupa MUHIMBILI, MOI, KUANZIA tarehe 10 Agosti,2010.

uteuzi huo umefanyika chini ya sheria ya MOI ya mwaka 1996, kifungu cha 5.

Je kwa kupoozana huko Mwakyusa atakua amevunja mpasuko wa kisiasa jimboni kwake, ambako kwa ccm , Kasesela ananguvu zaidi.

Nguvumali, Mwakyusa jimbo lake ni Rungwe Magharibi. Jimbo ulilolitaja la Mashariki ni la Mwandosya (Busokelo)
 
In short haja teuliwa kutokana na uwezo bali kwa kuogopwa kuwa kizingiti katika harakati za mtu mmoja kuwa mbunge? This is stupid.
 
In short haja teuliwa kutokana na uwezo bali kwa kuogopwa kuwa kizingiti katika harakati za mtu mmoja kuwa mbunge? This is stupid.

mimi pia najitahidi kuwaza , nahisi kuna msukumo zaidi ya uwezo, kuna msukumo wakumegeana kamuhogo, kumfuta machozi, na kumsogoza karibu.
naujua ukaribu wa Kasesela kwa Kikwete, mkuu wa mkoa wa Mbeya, ukaribu wa huyu jamaa na kina Lowassa.
alijiandaa kwa miaka 5, alikita kweli mizizi, isingekua chakachua ya wazee wa kule Rungwe , jamaa angeshinda tu.
 
JF tumeishiwa mawazo kiasi hiki????????????????????????????????
wewe ndio umeishiwa

ungejua yaliyo nyuma ya pazia usingesema tena

te unaweza connect dots za mama nyoni na richard>????
ukishamaliza unaweza pia za subilaga na tacaids??
baada ya hapo, unazijua za wote hao na mwakyusa??
je unajua za migombani na urusino??

eeeiiiishhhhh

ndo maana wewe ni macho mdiliko
 
haya ndio mambo ambayo shemeji zangu wananiangusha, sitaki kuamini eti ni coincidence...
 
Slaa au Kikwete lazima ampooze Kikwete au Slaa baada ya uchaguzi kwa kumpa ubunge wa viti maalum!
 
Hivi karibuni waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dr Mwakyusa amemteua bw Kasesela kuwa mjumbe wa bodi katika taasisi ya MOI ikiwa ni siku chache tu baada ya bw Kasesela kuangushwa kwa kura chache na Dr Mwakyusa.

Jambo jingine la ajabu ni kuwa kaka yake wa damu na waziri Wassira ni mjumbe wa bodi iliyochini ya wizara yake (bodi ya pamba) kwa kuteuliwa na mdogo wake..... je hapa hakuna mambo ya ajabu????
 
Back
Top Bottom