Prof. Abdallah Safari, uzalendo wako ni wa kupigiwa mfano ndani ya CHADEMA

Mnyonge Namba1

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
402
81
Katika hali ambayo vibaraka wa ccm hawataweza kuipotosha na CD zao za Udini na Ukabila, jana Prof aliudhihirishia umma wa Watanzania na dunia kuwa, kwenye harakati za ukombozi wa nchi kupitia M4C sisi sote ni ndugu, tatizo ni ccm peke yake kwa mustakabali wa taifa hili na watu wake.
Utayarishaji wa kesi ya kupinga Ushindi feki wa Dr. Kafumu Igunga, ufuatiliaji na usimamiaji wa hoja zote za kesi hii ulifanywa kizalendo sana na Prof Safari.

Bila shaka CCM watakuwa walijaribu kumshawishi Prof kwa sera zao za Ukabila na Udini au kumpa rushwa ili alegeze kamba lakini Prof aliamua kuupuuza ujinga wao, akafuata njia iliyosahihi na ya haki, kwa sababu anaipenda nchi yake na watu wake, lakini zaidi anakipenda chama chake cha CHADEMA. Ndiyo maana jana na leo tunasherehekea nchi nzima ushindi wa haki dhidi ya dhuluma jimbo la Igunga.

Wito wangu kwa Watanzania wote wanaopotoshwa na ccm kwa sera yao ya Ukabila na Udini au fedha, wapuuzeni hao ccm na muwe wazalendo wa kweli kama Prof. Safari ili sote kwa pamoja tuikomboe nchi yetu mapema iwezekanavyo.



!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO LETU SUGU NI CCM !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ccm wataisoma namba tu na mpaka kieleweke....mnadhani hizi ni zama za akina mrema 2005?
 
rufaa ya ubungo na arusha lazima mnyolewe bila wembe

Hayo majembe hata ukiyatoa bungeni yakiwa nje ni balaaaaaaaaaaaaaaaaaaa zaidi hasa nyika.Mkimtoa mnyika bungeni atapewa kazi ya kuzungukia nchi za ulaya na mashariki kuhamasisha watanzania kuunga mkono M4C
 
...tumeona mchango wa Godbless Lema (CHADEMA) aliyevuliwa ubunge wa Arusha. Vipi mchango wa Aeshy (CCM) aliyevuliwa ubunge Sumbawanga mjini? Karibu Kafumu usaidie kuiimarisha CCM yetu inayozidi kuporomoka kila kukicha
 
kweli usipoelewa ushabiki wa siasa utaishia kushangaa kila siku, ukishinda haki imetendeka, ukishindwa wamependelea, loh!
 
kweli usipoelewa ushabiki wa siasa utaishia kushangaa kila siku, ukishinda haki imetendeka, ukishindwa wamependelea, loh!
hakuna sehem ccm inashinda kihalali kwa hiyo upinzani ukishinda kesi haki imetendeka ukishindwa mahakimu wamepewa maelekezo na ccm wao..habari ndo hiyo
 
Huyo Profesa si analipwa lakini?

Hivi nyie huwa mnaanza na viroba kabla ya kuandika? Kwani mtu kuwa mzalendo maana yake ni kutolipwa?

Narudia kauli yangu ya awali "SERIKALI YA CCM PIGA MARUFUKU VIROBA AU WAAMURU WATENGENEZAJI WAPUNGUZE ALCOHOLIC CONTENT YAKE".
 
...tumeona mchango wa Godbless Lema (CHADEMA) aliyevuliwa ubunge wa Arusha. Vipi mchango wa Aeshy (CCM) aliyevuliwa ubunge Sumbawanga mjini? Karibu Kafumu usaidie kuiimarisha CCM yetu inayozidi kuporomoka kila kukicha

Kichekesho hiki. Hivi kafumu unaweza kumlinganisha na haiba ya Kamanda Lema?.
 
Ndo mjue kuwa cdm imejaa vichwa vya maana na wasomi wa ukweli na cyo wale wa kupewapewa ovyo!Heko Prof Safari!You did it.
 
Back
Top Bottom