Printer za mahakama zashindwa kutoa hukumu ya Lema

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Wanajamvi hebu nisaidieni hli swali kwa kuchagua jibu sahihi.

Hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyomvua ubunge Godbless Lema wiki mbili iliyopita hadi sasa nakala yake imeshindwa kutolewa, sababu hasa ni ipi?
a) Printer ni mbovu
b) Jaji amepata kigugumizi kwa dhambi aliyoifanya
c) Rushwa inahitajika ili kutoa nakala
d) Mahakama imechanganyikiwa kwa maombi ya kufunga ya Lema
e) (b) na (d) ni sahihi.
 
Lakini hiyo siyo brewking news mkuu. Utata wa nakala ya hukumu ya G. Lema nadhani unafika mwisho. Kwani mtu anaweza kukata rufaa kabla hajapewa nakala ya hukumu?
 
Mungu yupo kazini sasa,kwa ajili ya kuwatetea wajaa wake,kwani amekiskia kilio cha watu wake,niliwaambia siku nyingi kuwa tulieni Mungu atawatetea tuu!!
 
Wewe uliyepata ndondoo tulitegemea ukawa muwazi zaidi.

thread nyingine zinatoka machozi zinahitaji kufutwa na kitambaa.

Mods kitambaa cha kufutia thread za aina hii kiko wapi?
 
Wanajamvi hebu nisaidieni hli swali kwa kuchagua jibu sahihi.

Hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyomvua ubunge Godbless Lema wiki mbili iliyopita hadi sasa nakala yake imeshindwa kutolewa, sababu hasa ni ipi?
a) Printer ni mbovu
b) Jaji amepata kigugumizi kwa dhambi aliyoifanya
c) Rushwa inahitajika ili kutoa nakala
d) Mahakama imechanganyikiwa kwa maombi ya kufunga ya Lema
e) (b) na (d) ni sahihi.

Dhambi hii itawatafuna wote waliopindisha sheria,na wote waliosema uongo chini ya ardhi hii wanayoikanyaga huku ikiwasubiria pindi watakapoicha dunia hii
 
Wanajamvi hebu nisaidieni hli swali kwa kuchagua jibu sahihi.

Hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyomvua ubunge Godbless Lema wiki mbili iliyopita hadi sasa nakala yake imeshindwa kutolewa, sababu hasa ni ipi?
a) Printer ni mbovu
b) Jaji amepata kigugumizi kwa dhambi aliyoifanya
c) Rushwa inahitajika ili kutoa nakala
d) Mahakama imechanganyikiwa kwa maombi ya kufunga ya Lema
e) (b) na (d) ni sahihi.

Mimi nachagua C kwa sababu ndio kawaida yao. Kwao kila kitu lazima utoe kitu kidogo. Si unakumbuka ile ripoti ya nafikiri jaji Warioba kuhusu rushwa. Ilionyesha mahakama ni sehemu moja wapo inayodai sana kitu kidogo.
 
Ni kawaida ya serikali yetu, wamethubutu kwingi na wameweza, je hii itashindikana? Chadema haiwezi kwenda mahakamani bila copy ya hukumu, na siku wakiipata muda wa rufaa umekwisha, kumbuka June 2013 hakuna kesi itakayosikilizwa, kwa hiyo jimbo litabaki wazi na ndiyo dhamira ya ccm.
 
mpaka wale watatu waliofungua kesi mahakamani
kwa kumpinga lema ambaye alikuwa chaguo la Mungu watwaliwe.
ndipo majibu yatakapopatikana.
 
On the serious note, hiyo nakala ya hukumu inahitajika, kwani CDM si wameshakata rufaa? How did they do it without hiyo nakala?
 
Ni kawaida ya serikali yetu, wamethubutu kwingi na wameweza, je hii itashindikana? Chadema haiwezi kwenda mahakamani bila copy ya hukumu, na siku wakiipata muda wa rufaa umekwisha, kumbuka June 2013 hakuna kesi itakayosikilizwa, kwa hiyo jimbo litabaki wazi na ndiyo dhamira ya ccm.

Mkuu hiyo deadline ni ratiba ya mahakama au ni sheria!? Nifafanulie kidogo!
 
Ebu viongozi wetu wa CHADEMA watoe tarifa kama hiyo hukumu imetoka au bado na kama bado wameambiwa lini itatoka?Maana tunahitaji kuisoma na kuichambua
 
Hivi sheria za kesi za namna hii hazina kipengele kinachoilazimisha mahakama kutoa kopi ya hukumu? Ni lazima si si lazima? Kama ni wajibu wa mahakama kutoa kopi hiyo, ni muda gani?

Ikiwa si lazima na/au sheria haisemi chochote kuhusu hilo, basi hili ni bao la kisigino, CDM ijipange kulirejesha jimbo kupitia uchaguzi.

Ikiwa ni lazima na kuna muda uliowekwa kwa mahakama kutoa kopi hiyo, hapa kuna kesi ndani ya kesi. CDM ifungue kesi mpya kuishtaki mahakama.

Wazo binafsi linalowakilisha wengi - Nchi hii inaogozwa kijombajomba.
 
Back
Top Bottom