Printer Tshs 100,000

Nimetumia printer za aina nyingi na zimenifundisha kuwa wakati mwingi printer ni rahisi kuliko bei ya wino aka catridge. Chunguza pia bei za wino usijeikimbia printer.
 
Wakuu mnaoweka printers hapo juu (inkjet) nadhani majogajo anataka laser printer (tena anataka hp 1010 to be exact), sasa nyie mnamuonyesha inkjets..

Anyway mkuu kwa ufupi naomba uniambie unataka hii printer kufanyia nini biashara au kazi zako za nyumbani za kawaida.., kama biashara nashauri ununue laser (ingawa hii ni rangi moja, b/w kwahio utashindwa kuprint cards na kazi nyingine za rangi, ambavyo kwa inkjet ungeweza). Printer za rangi laser zipo (ila running cost ni kubwa sana) sababu zina catridge nne, na kila moja zaidi ya laki moja (hapo ni laki nne) yaani catridge zina bei kuliko printer (laser printer ya rangi ni kama laki mbili na nusu).

Kama ni kazi za nyumbani kutoa barua moja kwa siku kadhaa nakushauri nunua inkjet iwe 3 in 1 au hata ya kawaida tu (ambayo unaweza kupata kwa elfu 60) catridge za hizi inkjet zote mbili unaweza kuzipata kwa elfu 70 au 60 (na mara nyingi zinatoa page chache sana kama 200) kwahio utaona running cost ni juu (ila kuna way out badala ya kununu catridge mpya unaweza kurefill catridges kwa kutumia sindano zaidi ya mara tano kila wino ukiisha (hapa utapunguza matumizi kwa hali ya juu).

Pia kama unaona usumbufu kurefill kila mara unaweza kununua printer ambayo unaconnect CISS (continous ink system) ambayo catridge zinakuwa zipo connected kwenye mitungi wa wino kwahio wino ukiisha inavuta wino, wewe kazi yako ni kujaza mitungi tu (ingawa hii inashida moja kama printer haitumiki sana mara nyingi head zinakuwa zina shida ya kuziba)

Kwahio in short mkuu utaona kwamba kununua printer inategemea na yafuatayo

Budget yako: Inkjet ni bei rahisi kuliko laser ila running cost ni kubwa (ingawa ukiwa unarefill running cost inapungua, (kumbuka hata laser unaweza ukarefill pia)
Matumizi: Laser ni heavy duty kuliko inkjet ila kama unaprint rangi ni bora uchukue inkjet ambayo ni cheaper running cost na quality ya picha ni nzuri
mkuu inkjet ngap nzuri na wino wakurefill unapatikana wapi.?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom