Prince Muro lapata ajali

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
559
Basi la Prince Muro T485BQV limepata ajali eneo la Senjele-Tunduma na kuua abiria mmoja na kujeruhi kadhaa! Basi hilo lililokuwa likitokea Dar kwenda Tunduma lilikuwa likijaribu kulipita/Overtake Lori ndipo liliacha njia na kupinduka. Chanzo kinadaiwa ni mwendo kasi! IMG-20120320-WA002[1].jpg IMG-20120320-WA003[1].jpg IMG-20120320-WA006[1].jpg
 
lilikuwa likijaribu kulipita/Overtake Lori ndipo liliacha njia na kupinduka. Chanzo kinadaiwa ni mwendo kasi!

Inasikitisha! Halafu sababu za ajali huwa ni zilezile kila kukicha! Hatujifunzi?
 
Jamani jana si juzi tu nilisikia ajali nyingine ya basi la kampuni hii limepata ajali?
Nadhani mmiliki ni member wa FREE MASON. na ndo muda wa kutoa sadaka
 
hivi kweli kila ajali ni mwendo kasi? sijui, kama kweli sisi tunaokuwa tumo ndani ya magari hayo ni wapumbavu kwanini huwa hatukemei mwendo kasi?
 
ni princess muro na sio prince muro mkuu ni mabasi tokea muro investment

Tatizo hata sisi abiria huwa tunashabikia mwendo kasi wa magari badala ya kuwakemea inasadikika mabus yanayoenda tunduma kama mwendo wako ni lele mama hupati abiria eti bus lazima liwe na mwendo mdundo ndo unapata abiria hii inachangia madereva kukimbiza mabus ilimradi la nyuma yake lisimpite.tubadilike abiria tuyachukie mabus yanayokimbia hii itafanya mabus kuwa na mwendo wa kawaida
 
Nakumbuka siku moja nilisema kuhusu magari haya hapa JF kabla hata hayajapata ajali, waungwana wakanichana sana wakaniambia kuwa nisiwe napanda basi hilo nipande ndege na nk, lakini hawakujuwa kuwa nilitoa thread ile kwa ajili ya kuwaonya pia Watanzania wenzangu, ona sasa.... haya mabasi ni mabovu sijui kwanini yanaruhusiwa kuendelea kufanya shuguli hizo..... ngoja yasababishe vilio ili tupande bendera nusu mlingoti, ndiyo tulivyo watanzania, hapo ndipo tutakapolia na kusaga meno.
 
Back
Top Bottom