:::Preta & El-Toro:::

afrodenzi

Platinum Member
Nov 1, 2010
18,145
9,207
Hongera zikufikie, kimwali kumtwaa
Wambea msiwasikie, nyumba na mitaa
Karaha msizishike, msingenyo kukataa
Hongera zikufiee, kimwali kumtwaa...

Kwa mbali msikike, mkipeta na ku ng'aa
Pamoja mshikike, kwa dhiki na rahaa
Wawili muhangaike, kulea na kuzaa
Hongera zikufike, kimwali kumtwaa..

Kazi zisikuzidie, nyumbani ukakaa
Kwa wema umsikie, usiwe ka kichaa
Ndugu muhudhurie, mfikapo mkaa
hongera zikufikie, kimwali kumtwaa

Wana JF tunapaa, na la kheri tunawapa
Msiwe kama mkaa, kutumiwa na kuchakaa
Pamoja mnang'aa, na sifaa mwazitwaa
Hongeara zikufike, kimwali kumtwaa..

Afrodenzi unatisha, umenirusha roho juu na lako shairi, Nguli Shusha pumziii, oooh shabashii. Najua wanawali wataishi Arusha

Afrodenzi unatisha, umenirusha roho juu na lako shairi, Nguli Shusha pumziii, oooh shabashii. Najua wanawali wataishi Arusha

Nguli nakutafuta, naona wanikataa
Kona baa yatufa, unialikapo tuta kaa
Pamoja tutafaa, twa washa nama ta
Furaha tutatwa, tutakanyaga na mita..

Mmmmh!...bado sijaellewa,ngoja wajuvi wa kufumbua mashairi waje,..wakisha dadavua ntakua kwenye nafasi ya kusema chochote,.....i will be back

Imetulia ngoja niimbe kwa sauti ya 3

Niingilie naya kwanza au ya mnee..??
Hahaha lolz

Kuna waliofunga ndoa ee?

Hongera zao, Mungu muweza awajaze baraka tele na tele kila siku ya maisha yao pamoja

Mi ni mpya but ninfatiliaji sk nyingi, hongereni sana ndugu.

afrodenzi, mi sijui kuandika poems, nitakuandikia na ww waraka na mtakatifu. manake nataka unipeleke kwa mganga wako,limbwata lako lina cement it seems. nataka la kujengea ghorofa baharini,lol

embu chukua maamuzi magumu AD,tufafanulie kinagaubaga nini hasa kimetokea,kuna mtu kavuta mzigo jumla au?

afrodenzi, mi sijui kuandika poems, nitakuandikia na ww waraka na mtakatifu. manake nataka unipeleke kwa mganga wako,limbwata lako lina cement it seems. nataka la kujengea ghorofa baharini,lol

Hamna wala nikujaribu tuu..
Nway kuna mganga mmoja
namfahamu mwehhhh
Huyo atakusaidia kwa lolote na chochote
....... Muombe tu basii .......

Sasa idara ya mapishi waionaje dear??

Mi ni mpya but ninfatiliaji sk nyingi, hongereni sana ndugu.

Karibu mgeni..
Uketi na kufurahia..
vifijo, nderemo na mambo motomoto..
Zamu yako ifikia, lakheri kuwatakia ..

Back
Top Bottom