Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Taarifa ya Maendeleo ya Kuchangia Wahanga Wa Mafuriko.
Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania (TPN) Kwa kushirikiana na www.issamichuzi.blogspot.com na www.jamiiforums.com na kampuni ya Push Mobile ambayo inatuunganisha na mitandao ya simu ya ZAIN; TIGO na VODACOM imekuwa ikiendesha kampeni ya kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyoikumba Tanzania ambayo ilizinduliwa tangu tarehe 12-01-2010 kwa ajili ya familia zaidi ya 8,000 zilizoathirika kwa kukosa makazi, vyakula, na huduma za afya na kupoteza mali nyingi. Misaasa yote itakayopatikana inapelekwa Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania ambao wako mstari wa mbele katika kuwasaidia wahanga. Awamu ya kwanza ilikwisha wakilishwa.
TPN na wadau wake inaendelea kuratibu harambee ya kuchangia wahanga wa mafuriko haya kwa kukusanya misaada ya vitu mbalimbali na pesa kwenda kwenye ofisi za Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania ambacho kiko mstari wa mbele kuongoza juhudi za kusaidia walioathirika ikishirikiana na taasisi mbalimbali binafsi na vyombo vya serikali. Michango inayopokelewa ni pamoja na fedha na Magodoro, Mahema, Vyandarua, Vyakula (visivyoharibika), Maji safi (masanduku ya chupa za maji), Madawa ya kuzuia maambukizi (ambayo hayajaharibika au kufunguliwa), Vifaa kwa ajili ya matumizi ya kina mama na watoto, Makaratasi ya kujipangusia (clean wipes), nguo, vyakula n.k.
TPN inapenda kuwahakikishia Wanachama na wadau wote waliofanya mawasiliano nasi kuwa TPN haijihusishi na kampeni yoyote mpya zaidi ya ile ya mwanzo iliyoiratibu na wadau wake na inazidi kutoa wito kuwa wote wanaopenda kuchangia wanaweza kufanya hivyo kupitia makato ya kila siku ya muda wa maongezi wa simu za mkononi (Tigo; Zain na Vodacom) kwa Kuchangia Shs 150 kwa siku kwa muda wa siku 30 kwa kutuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Awali utakatwa Shs 250 kama ada ya kujisajili (Makato yote yanahusisha kodi na gharama za kuunganishwa). Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047
TPN na Wadau wake ilikabidhi awamu ya kwanza ya misaada kwa Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania iliyokusanywa (haihusishi michango ya SMS) ikiwa ni pamoja na Ndoo za Plastic; Maji; Magodoro; Magodoro; Sembe; Chumvi; Mafuta ya kupikia; Miswaki na dawa za miswaki;Sabuni; Majani ya Chai; Mablanketi na Vyandarua vyote vikiwa na thamani ya TZS 1,381,000. Pia tulikabidhi pesa taslimu TZS 1,068,364.80. Tunawashukuru wote waliotoa. Misaada inayoendelea kukusanywa itakabidhiwa katika awamu ya pili siku ya Ijumaa tarehe 29-01-2010.
Misaada pia inaendelea kupokelewa katika makao makuu ya Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania Jijini Dar-es-Salaam Masaki na ofisi zake zote Tanzania. Unaweza pia kuchangia vitu mbalimbali kwa kuvilet ofisi za TPN zilizopo Barabara ya Nyerere; Jengo la TOHS (Dar Group); Ghorofa ya 1 karibu na Radio Tanzania au piga simu namba: 0715 740 047 ili ofisa wa TPN avifuate (utalipia usafiri). Hakuna msaada mdogo au usio na maana na misaada yote itapokelewa.
Pamoja Tunaweza!
Imetolewa na:
Mtandao Wa Wanataaluma Tanzania
(Tanzania Professionals Network)
25-Januari-2010