Press Conference ya Kova, ni halali?

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Kamanda Kova amefanya press conference, baada ya Jeshi la polisi, Kanda Maalum ya Dar es salaam, kukamata watu kadhaa kwa tuhuma za makosa mbalimbali. Mmoja wao amekamatwa kwa tuhma za kujifanya kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Kova amemwita huyu bwana tapeli, na amemtambulisha mbele ya vyombo vya habari kuwa ni tapeli, kikubwa zaidi ni kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Ilala, nae akaja mbele ya kamera ili kuthibitisha madai ya jeshi la polisi, na kutoa testimony yake.
Source: Clouds TV, DONDOO ZA HABARI.
My take: Mchakato uliofanyika mbele ya waandishi wa habari umechukua sura ya kimahakama, huku Kova akiwa ndio delegate wa JAJI wa mahakama hiyo isiyo rasmi. Naona haki kwa mtuhumiwa haikutendeka hapa, kwani ameishatambulishwa kuwa ni tapeli.
Nimeona niilete kwenu wanajamvi mnipe maoni yenu.
Karibuni!
 
Kova nae tapeli ndo maana kaweza kumuhukumu huyo jamaa, matapeli wanajuana.
Zile nyuzi za Alshabab zilikuwa ni uongo au kiuzuri ni za kitapeli
 
Kova nae tapeli ndo maana kaweza kumuhukumu huyo jamaa, matapeli wanajuana.
Zile nyuzi za Alshabab zilikuwa ni uongo au kiuzuri ni za kitapeli

jana wana-KAFU wa jimbo la Wawi wameandamana kuunga mkono tamko la kamati kuu. Sijui hakukuwa na tisho la Al-Shaabab huko?
 
Mbona na nyie mmekuwa ma judge, na nyie matapeli

hatujakuwa ma-judge mkuu.
Wewe unaona ni sawa kumweka mtuhumiwa mbele ya kamera, huku ukimwita tapeli na maneno kama hayo? Mi sidhani kama jamaa alitendewa haki, kisheria na kibinadamu...
 
duh?
Kumbuka huyu ameapa kuilinda katiba, akiwa law enforcer, sasa nini tena?

...ata majaji na mahakimu wameapa hivyohivyo lkn wanopelekewa mtuhumiwa wanasema hana atia na kibaya zaidi wanadai ushaidi hautoshi ili hali hawasemi ni ushaidi upi utawaridhisha, sasa Kova ndo maana anamaliza mambo.
 
Mbona wakina Rostam na Kagoda yao iliyojaa matapeli mbona hawakamati?Au aliishawahukumu
 
Mara nyingi sana nimekuwa nikisema kuhusu lack of skills za polisi. Kwa kesi ambayo imejikita mwenye utambuzi kitendo cha kuuanika mtuhumiwa kabla ya kesi kuanza ni kuuanika kesi yako.

Sass on a baada ya hapo kesi itpelekwa mahakamani na kule mapolisi watasema upelelezi bado haujakamilika, kwa vipi usiwe umekamilika wakati Mtu ameanikwa mwenye vyombo vya habari.
 
Ngojeni kidogo...kidogo tu... Huyu Jamaa Kova ni yule aliyewaweka mbele ya kamera wale jamaa waliokamatwa na Muro akatuambia ni Matapeli na ni wa kuogopwa sana... Lakini mwisho wa siku wakaachiwa huru na Mahakama.
 
jana wana-KAFU wa jimbo la Wawi wameandamana kuunga mkono tamko la kamati kuu. Sijui hakukuwa na tisho la Al-Shaabab huko?

Kule si Tanganyika mkuu,kuna utawala mwingine kabisa, apparently al shaabab si kitisho kwao
 
Ngojeni kidogo...kidogo tu... Huyu Jamaa Kova ni yule aliyewaweka mbele ya kamera wale jamaa waliokamatwa na Muro akatuambia ni Matapeli na ni wa kuogopwa sana... Lakini mwisho wa siku wakaachiwa huru na Mahakama.

Kumbe wameachiwa wote huru.nilidhani ni Murro pekee,anyway Kova hana umakini wowote.kumbuka inshu ya wastaafu wa East Africa na taarifa za kufa kiongozi wao aivofanya mbwembwe kwa kumwita jukwaani huyo aliyedaiwa kufa
 
Yale yale ya Jerry Muro!

inaonekana yameshakuwa mazoea.
Unaona nini kifanyike? Kova hawezi kuburuzwa mahakamani kwa udhalilishaji huu wa kumwita mtu tapeli wakati vyombo vya sheria havijathibitisha?
 
inaonekana yameshakuwa mazoea.
Unaona nini kifanyike? Kova hawezi kuburuzwa mahakamani kwa udhalilishaji huu wa kumwita mtu tapeli wakati vyombo vya sheria havijathibitisha?

Unayo haki ya kufanya hivyo na kudai fidia sema wabongo hawajali haki zao.
 
Back
Top Bottom