Precisionair Yakatiza safari baada ya kuruka dakika 10

Mfumwa

Kwa kweli zinahitajika zifanyiwe matengenezo makubwa, mwaka jana nilitumia moja wapo ya ndege za Precision kuelekea kwenye jimbo langu la uchaguzi (Mwanza)....ndege ilkuwa na joto mle ndani utazani upo kwenye tanuru, nilikuwa na mtoto wangu wa kike akaniambia baba kwanini tusifungue madirisha....wahudumu walituambia nitatizo dogo kwenye mfumo wa hewa sijui kitu gani....hizi ni rasha rasha tusisubiri sunami!
kuna nyingine ya atc inapiga kelele kama DCM za mbagala...mara injini moja izimike mko angani mara iwake.....mkipata ajali rais anatoa salamu za rambi rambi mchezo umeisha....
 
Kosa la pilot ni nini? yeye kaona hatari na kurudisha ndege, sasa mlitaka nini? Watu wengine bwana unashindwa hata kuwaelewa!

Mr.Jimmy!
Pilot amejitahidi kuokoa ajali ambayo ingetokea. Ila hizo ndege zirekebishwe kiufundi siyo mzaha mzaha au mpaka ianguke tena na kuua ndo wahusika watajua how serious tatizo lilivyo. Kama tulivyozoea maafa yakitokea ndo akili inachaji kwa solution za kushtua shtua.
 
"Suala la ndege za PW na hasa hiyo ndege yao ya ATR (Sijui ni product ya nchi gani) soon or later itakuja kuleta maafa. Kwa hii ya leo tushukuru pilot alikuwa na busara akarudi kutua....."

***********************

Tiba: ATR hutengenezwa Ufaransa.
 
Hawa jamaa cha ajabu hawana hata ile chembe ya kumjali mteja utakuta wahudumu wanakujibu chochote kile wanachojisikia wao halafu wanajifanya wako bize kumbe hamna kitu. Mwezi wa Disemba nilikumbwa na hiyo dhahama baada ya ATC kufungiwa kuruka. Ilikuwa kama vile mchezo wa kuigiza hawana adabu. Hao Precision inabidi wajifunze sana mbinu za kuwajali wateja wao. Abiria wengi wanapata usumbufu usiokuwa wa lazima kwa sababu ya hao Precision kama vile ratiba kubadilishwa , kukatishwa kwa safari na kutokuwa na mawasiliano ya kimtandao baina yao na travel Agencies unaweza kukata tiketi yako ukafika uwanjani kuconfirm(Dar es salaam sana sana) ukaambiwa tiketi yako ina mtu mwingine ukienda deep hupati majibu ya kuridhisha. There are a lot of irregularities on Aviation Industry in this country someone has to talk about it. Utakuja sikia ya MV Bukoba au ya ajali ya Treni . Na baada ya hapo utaona watu wanazinduka na kuanza kuunda Tume. What a Shame! Huu ni ukora.
 
Back
Top Bottom