Jana tu KIA yametokea haya haya watu wameconfirm safari zao kuja Dar wanafika airport wanaambiwa ndege imejaa ikatokea pata shika pale hadi ikabidi wasafirishwe hadi nairobi ambao walipakiwa kwenye ndege ya PW 719 ambayo ilikuwa inatumika na KQ. Yaani Tanzania tunasikitisha!!
Mtz,
Hii si makala ya kwanza kuhusu hili swala. Kuna jamaa aliandika hapa kuwa walishushwa Arusha (wakiwa tayari ndani ya ndege wamekaa kwenye viti) na Wazungu wakaingizwa kwenye ndege. Hapa lazima ufahamu kuwa huyo travel agent wa hilo kampuni lililokuwa libebe Wazungu, atakuwa mtu mmoja mzito sana ambaye hata Precion Air wanamuogopa. Hilo wala usitilie shaka na kama mtu haamini, afuatilie ajue Wazungu walikuwa wanashughilikiwa na nani safari yao. Sidhani kama Wazungu walipata wazo la kuhonga au kutumia vitisho ili wasafiri siku hiyo na nyie mbaki.
Miaka kadhaa nyuma, nasikia meli ilichelewa kuondoka Bukoba. Watu ndani wameshonana kama magunia. Wamekaa zaidi ya saa moja na mwisho wanaona Benzi linaingia na anashuka Waziri Rwegasira??? na mizigo yake. Walipoingia tu ndani ya meli, meli ikaondoka..........
Kuna watu ile Tanzania ni nchi yao na watafanya wanachokitaka bila kujali wala kuogopa. Sasa hata akina Precion Air wanakuwa wanawaogopa wenye nchi. Wakija na kutoa amri, basi hawana cha kusema. Sidhani kama wanafanya hivyo bila kujali kuharibu jina la Kampuni nakukimbiza wateja.
Unajua airlines hasa katika kipindi hiko kigumu kinaathiriwa sana na 'no shows' ili kuthibitisha kama kweli hujabadili nia ya kusafiri siku hiyo iliyo kwenye tiketi yako inabidi ufanye hivyo vinginevyo ndege inaweza kuondoka na watu wachache kama wakitegemea hivyo ulivyofanya.Habarini za mchana
Jamani mimi kuna kitu kinanitatiza, nashindwa hata kuelewa. Kwa kawaida mtu unapokata ticket ya ndege as RETURN TICKET si huwa inaandika unaondoka lini na kurejea lini?
Sasa nimekuwa nashangazwa na baadhi ya ndege eti unapofika huko uendako say unatoka DAR umekwenda MWZ ukitaka kurudi lazima ufanye confirmation. Nijuavyo mimi baada ya kusafiri ndani na nje ya nchi kama sikupiga simu kwa airline nina maana kuwa nitarudi as per schedule. Nways, nimeshaona hata ndege za nje zinazotaka confirmation uwe unarudi on the day au unabadili schedule yako... SIIKUBALI ila ndio hivo tena.
Sasa tatizo lililonifanya niandike ni kuwa baada ya kufika MWZ kwa shuguli za kikazi, nimekaa kule nikapeleka ticket siku 3 kabla ya safari kuconfirm kuwa narudi siku hiyo iliyoandikwa. Tulikuwa group wakatupa OK kuwa tutaondoka na ndege ya Precision Air ya saa 2.35 asubuhi.
Tunafika airport kucheck IN eti wanasema kati yetu kuna watu kadhaa hawakutakiwa kuondoka na ndege ya asubuhi wataondoka saa 8 mchana. Kwa kweli habari hiyo haikukaa vizuri masikioni. Baada ya kubishana kwa muda kwamba kwa nini watupe OK tulipoconfirm na kutupa hata ticket kuonyesha tutaondoka asubuhi kisha siku ya safari tuwe tumekatwa?
Ati wakasema ilikuwa ije ndege ya watu 72, tumebadilisha kwa hiyo inabidi mwende mchana. Hivi unawezaje kuamua tu kubadili ndege gafla wakati unajua una wasafiri zaidi ya idadi ya hiyo ndege uliyoileta? Tukaja kugundua kuwa kuna wazungu walikuja kuconfirm baadae wakaamua kuwaweka wao kama 20 hivi na kuamua randomly kukata waswahili oh wana connection Dar... aliyekwambia hao uliowakata hawana commitment huko waendako ni nani?
Kwa kweli Precision hiki mfanyacho si sawa. Ticket mnatutoza karibia laki 4 return kisha mnatunyanyasa kama tunapanda dala dala haiko sawa. Hapo hapo mnafika Dar mizigo imebaki Mwz hivi kwa nini mnashindwa kufanya kazi zenu sawa sawa
HALAFU TUNASHANGAA KWA NINI HATUENDELEI TANZANIA. hivi vitu vidogo vidogo vinatufanya tuonekane hopeless na tunaendeleza upuuzi ktk maamuzi yetu ya kila siku.
Jamani samahanini kwa habari ndefu ila iliniuma sana, na wenyewe niliwambia MWZ na hata hapa Dar. Na for me I guess I will never waste my time with your airline again.
Mtz halisi\
ndege nyingi hapa kwetu lazima u comfirm...kucomfirm sio kwamba ugomvi inakusaidia mwenyewe br
in case umecomfirm na ndege imejaa siku hiyo wanapewa priority walio na ok
sasa ndege aiweze kuacha abiria kwasababu ya kupiga simu kusema ok wati waweke siti ya mtz..ok una tkt kweli ya kurudi ukija kama wamepiga watu na wengine wakapewa ok kama huna mama yangu utaabaki kuangalia mabawa yakiruka na huna jinsi
sasa basi kama ni mgeni jitahidi itakusaidia mwenyewe;kama uamini kata hndege ya kigoma atcl uone moto wake kama uja comfirm hapo utajua umuhimu wa cormfimation
please soma nilivoandika hapo mwanzo kabisa
i said, we as a group confirmed 3 days prior siku ya safari na tukapewa ok plus tukapata na ticket kwa ajili ya safari siku ya safari
kama kusafiri nimesafiri sana, ndani na nje ya nchi hakuna ugeni hapo
my concern was why get a confirmation and a ticket to show ni mmoja wa wasafiri kisha siku ya safari at the airport unaambiwa huwezi kwenda
by the way ingekuwa sijapata ok wasingenisafirisha na hiyo ndege on the day. Thanks anyways