Ppsss psss....

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,196
113,471
Nadhani wengi mmeshausikia huo mlio. Ni mlio ambao unatengenezwa kwa kukutanisha sehemu za juu na chini za mdomo (lips) na kuzifunga na hatimaye kuachia hewa iliyokusanyika kwa kuzifungua sehemu hizo kwa kutumia nguvu kidogo. Matokeo yake ndio huo mlio.

Sasa nilipokuwa dogo, mtaani nilikuwa nikiwaona wakubwa zangu wakipiga huo mlio pindi waonapo mdada ambaye amewavutia akipita barabarani. Walikuwa wakifanya hivyo ili kuvuta nadhari yake kwao (draw her attention).

Kuna wadada ambao hawakupenda kusikia huo mlio na kuna ambao walipenda. Sasa mimi sielewi asili ya huo mlio nini. Halafu ningependa kujua kama siku hizi bado hiyo tabia ipo. Wadada wa humu yameshawahi kuwatokea hayo ya kupigiwa ppsss ppsss? Na kama yamewahi kutokea ulijisikiaje? Ulichukia? Ulifurahi?

Nakaribisha michango yenu...
 
Nakiri kuwa nimefurahishwa na ufasaha wa lugha ya kiswahili uliyotumia "Walikuwa wakifanya hivyo ili kuvuta nadhari yake kwao (draw her attention)".
Turudi kwenye mada, kweli hizo ppss zimetumika na zinatumika lakini ni kwa watu wote sidhani kama zipo kwa wanawake tu. Nadhani si busara kwangu kuwasemea wanawake hujisikiaje pale pss hiyo inapotoka kwa mtu wa jinsia nyingine, natumaini watapita hapa kutujuza !
 
Siku hizi nazitumia kumuita barmaid or barman ili aniongezee kinywaji:becky::becky::becky:
 
hizo zinatumika sana bar kumwita barmaid na akiitwa anakuja mbio ndio ulikobaki huko
 
Mbona makonda wa daladala wanabusu mfpuuuu mfpuuuuu wakati wakumsimamisha dereva kwani hii haiwasisimui:becky::becky::becky:
 
:welcome:Hata kusimamisha bodaboda kwa hiyo wanawake wanajihisi ni taxi au bodaboda wakisikia pssss pssss psss:becky::becky::becky:
 
Bado inatumika mitaani ingawa inategemea na mtumiaji na mazingira
 
Nadhani wengi mmeshausikia huo mlio. Ni mlio ambao unatengenezwa kwa kukutanisha sehemu za juu na chini za mdomo (lips) na kuzifunga na hatimaye kuachia hewa iliyokusanyika kwa kuzifungua sehemu hizo kwa kutumia nguvu kidogo. Matokeo yake ndio huo mlio.

Sasa nilipokuwa dogo, mtaani nilikuwa nikiwaona wakubwa zangu wakipiga huo mlio pindi waonapo mdada ambaye amewavutia akipita barabarani. Walikuwa wakifanya hivyo ili kuvuta nadhari yake kwao (draw her attention).

Kuna wadada ambao hawakupenda kusikia huo mlio na kuna ambao walipenda. Sasa mimi sielewi asili ya huo mlio nini. Halafu ningependa kujua kama siku hizi bado hiyo tabia ipo. Wadada wa humu yameshawahi kuwatokea hayo ya kupigiwa ppsss ppsss? Na kama yamewahi kutokea ulijisikiaje? Ulichukia? Ulifurahi?

Nakaribisha michango yenu...

Kujambisha je....naona watu huwa wanarukaruka sana kwa uchungu wengine wakijambisha...hasa wanaume sijui inawadhuru vipi
 
Hata mimi siipendi!! Mara nyingi hata kama najua mtu ananiita mimi, huwa sihangaiki kugeuka! Kama unanijua please call me by Name! Otherwise don't pssssssss psssssssssss me!:shocked:
 
NN Sheria ya unyanyasaji wa jinsia (sijui ndo inaitwa hivyo?) inakataza. Ilivyotoka iliondoa mambo mengi ya mazoea kama kukonyeza nk
 
NN Sheria ya unyanyasaji wa jinsia (sijui ndo inaitwa hivyo?) inakataza. Ilivyotoka iliondoa mambo mengi ya mazoea kama kukonyeza nk

Duh! yaani hata kukonyeza/zwa kunakuwa legislated? Khatari kubwa hii
 
Kwa hali yoyote na kwa maoni yangu sidhani kama ni njia ya kistaarabu ya kumwita mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom