Power of love

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,189
Jamani naombeni kuelimishwa power of love ni nini? Maswali mengine yatafata baadae. Hiyo ni homework nimepewa na ticha wangu wa tuition na kesho natakiwa kusubmitt.
Msichakachue hadi mnipe majibu kwanza.
Ahsante!
 
Sababu jibu ni jibu tu mwambie ni wimbo ambao uliimbwa na Jennifer Rush na kurudiwa na kina celine dion...

Seriously though ni nguvu ya mapenzi ambayo hupelekea jambo fulani kufanyika ambapo bila upendo lisingetendeka (mfano kumsamehe aliyekutenda..., kuhatarisha maisha yako sababu ya mpendwa wako, sacrifice n.k.)
 
pawa of lav ni nguvu ya kufanya ya kijinga na ya akili yote kwa sababu ya unavyojisikia kwa mtu fulani
 
walimu wa siku hizi..
anamtafuta mrembo siku ya sherehe za pasaka na kumwambia
homework yako ni kutafuta maana ya 'power of love'

akishapata hiyo atamwambia njoo nikufundishe 'power of good sex'...

na wazazi wamelipa ada wanajua mtoto anatengeneza future....
 
Jamani naombeni kuelimishwa power of love ni nini? Maswali mengine yatafata baadae. Hiyo ni homework nimepewa na ticha wangu wa tuition na kesho natakiwa kusubmitt.
Msichakachue hadi mnipe majibu kwanza.
Ahsante!

sema ukweli kuwa yamekufika.....................maji umeyavulia nguo sasa huna budi kuyaoga...................lol..................power of love ni kujitambua kuwa unahitaji kumhudumia mwenzako bila ya masharti yoyote kama vile Bwana Yesu Kristu alivyotoa maisha yake kwa ajili yetu sisi wenye dhambi kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwetu sisi pamoja na ukorofi wetu.......

kwa hiyo power of love ni kuwa ukishikwa basi shikamana bila ya kuweka zengwe kuwa leo nimechoka au sijisikii wakati unatakiwa kubeba majukumu yako khalali kabisa.........
 
akishapata hiyo atamwambia njoo nikufundishe 'power of good sex'...

na wazazi wamelipa ada wanajua mtoto anatengeneza future....

kama power of sex hii nayo ni future basi ujue tumekwisha.....................
 
sema ukweli kuwa yamekufika.....................maji umeyavulia nguo sasa huna budi kuyaoga...................lol..................power of love ni kujitambua kuwa unahitaji kumhudumia mwenzako bila ya masharti yoyote kama vile Bwana Yesu Kristu alivyotoa maisha yake kwa ajili yetu sisi wenye dhambi kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwetu sisi pamoja na ukorofi wetu........

Mkuu sidhani kama nakubaliana na wewe ni kujitambua kwamba unahitaji kumuhudumia mwenzako..., wengi tunatambua umuhimu wa kutoa huduma ila hatufanyi...,

Power of love ni kufanya kile hata kama ulikuwa hutaki kufanya au kitakuumiza unakifanya sababu tu ya mapenzi / kupenda (ambavyo vinginevyo kwa kawaida usingefanya) ingekuwa ni kutambua kuhitaji kumuhudumia mwenzako bila masharti (ingeitwa power of wajibu wako, au ubinadamu)
 
To me POWER OF LOVE is that willingness of going extra mile for the sake of love,be doing something good or bad for the sake of it
 
Sababu jibu ni jibu tu mwambie ni wimbo ambao uliimbwa na Jennifer Rush na kurudiwa na kina celine dion...

Seriously though ni nguvu ya mapenzi ambayo hupelekea jambo fulani kufanyika ambapo bila upendo lisingetendeka (mfano kumsamehe aliyekutenda..., kuhatarisha maisha yako sababu ya mpendwa wako, sacrifice n.k.)

hiyo nguvu ya mapenzi mtu anazaliwa nayo au?
 
To me POWER OF LOVE is that willingness of going extra mile for the sake of love,be doing something good or bad for the sake of it

Do you have that? I mean that power to love someone n going extra mile to do even bad thing for the sake of ur love?
 
walimu wa siku hizi..
anamtafuta mrembo siku ya sherehe za pasaka na kumwambia
homework yako ni kutafuta maana ya 'power of love'

akishapata hiyo atamwambia njoo nikufundishe 'power of good sex'...

na wazazi wamelipa ada wanajua mtoto anatengeneza future....

hahahahaha! Sawa tu ila dunia hii tunatakiwa kujifunza mambo mengi incl mapenzi.
 
sema ukweli kuwa yamekufika.....................maji umeyavulia nguo sasa huna budi kuyaoga...................lol..................power of love ni kujitambua kuwa unahitaji kumhudumia mwenzako bila ya masharti yoyote kama vile Bwana Yesu Kristu alivyotoa maisha yake kwa ajili yetu sisi wenye dhambi kwa mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwetu sisi pamoja na ukorofi wetu.......

kwa hiyo power of love ni kuwa ukishikwa basi shikamana bila ya kuweka zengwe kuwa leo nimechoka au sijisikii wakati unatakiwa kubeba majukumu yako khalali kabisa.........

hapo umemaanisha sex? Halafu na wewe toka lini umekuwa mpiga madongo! Hayajanikuta, nataka nikamilishe assignment ya ticha.
 
hiyo nguvu ya mapenzi mtu anazaliwa nayo au?
kila mtu anayo tangia anazaliwa just imagine ni mangapi unaweza kufanya kwa mpenzi wako, watoto wako (ukipata :) ), wazazi wako, marafiki n.k.

Na sio watu tu hata wanyama nimeshaona mifugo mingi mama yupo radhi, kufa njaa au kufa kwa kuwa-protect watoto wake.., kwahio in short ndio power of love ipo and there is no stronger power than this one.., yaani mtu unajisahau nafsi yako kwa ajili ya mwingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom