Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Aisee huyu jamaa alivuma sana miaka ya 80 but sadly I never got to see him. Kulikuwepo na story kibao kuhusu uwezo wake wa nguvu za misuri, mambo kibao yaliongelewa, mfano:

-- Alikuwa anaweza kunywa kreti nzima ya soda kwa mkupuo
-- Alikuwa anaweza kutegesha kifua na tairi la nyuma la trekta kupita bila kuumia
-- Alikuwa anaweza kuvuta lorry lenye shehena kubwa kwa kutumia nywele
-- n.k.

Were these just a bunch of childish myths kutufanya tukimbie mchakamchaka na kuwahi namba shuleni or was there a grain of truth in them? Tafadhali sana naomba wale waliobahatika kuyaona maonesho ya jamaa watupatie ushuhuda hapa.

Pia naomba kuuliza, je yuko wapi siku hizi, kuna mwenye picha? Bado yupo, au..??
Akhsanteni!!
 
Ni kweli huyo jamaa, alikuwa na nguvu kweli kweli, nasikia alikuwa ni mtu wa Musoma, Mara uko...! Hayo ni mambo ambayo kweli alikuwa anafanya, na alikuwa ana uwezo wa kunywa chupa za orange squash mpaka mbili bila ya kuzimua.

Si hivyo tu, alikuwa anauwezo wa kuzuia piki piki kwa kutumia nywele na wakati mwingine meno. Na hata kuzuiya gari kwa kutumia nywele zake. Na alikuwa akivunjiwa jiwe kubwa kifuani kwake.

Pia kulikuwa na mwingine anaitwa power Bernard, na wakaja mwishoni mwishoni kina power Bukuku, ila wengine nimewasahau.

Gonga hapa mkuu, kuna uzi kama huyo.

Power-mabula-moris-nyunyusa-na-mwinamila-tz-imewaenzi-vipi.html
 
I knew him personally and I always have a story to tell about him. You can hit me up whenever is convenient for you and I'll be glad to share it with you. He is the source of my lifelong passion.

Will link up, thanks!

I really wish to have seen the dude, possibly could've been part of inspiration in some aspects of my life too!
 
nilimuona mara kadhaa kwenye maonesho wakati nikiwa primary skul. ni kweli alikuwa anafanya hayo yote yaliyotajwa,ilikuwa inaogopesha aisee.mara ya mwisho niliskia habari zake kuwa aliokoka na akatolewa mapepo mengi.

Ilisemekana alikuwa anatumia nguvu za giza na hizo kreti za soda walikuwa wanakunywa majini (sijamuona live baada ya kuokoka).ila naskia aliacha mazingaombwe.umenikumbusha mbali sana
 
Hivi mzee morris nyunyusa bado yupo?alikuwa na issue ya kufuatilia copy right ya ule wimbo wake wa ngoma za taarifa ya habari sijui iliishia wapi. inasikitisha,inanifanya niwaze 30, 40 yrs to come nitakuwa wapi!

Poa mkuu, watu kama kina power Mabura na wengine kama Mzee Moris Nyunyusa, ndio walikuwa maselebu wa wakati huo. Lakini ndio hivyo tena sidhani kama kuna kumbukumbu zozote zilizo ifadhiwa kuwepo kwao duniani.
 
hivi mzee morris nyunyusa bado yupo?alikuwa na issue ya kufuatilia copy right ya ule wimbo wake wa ngoma za taarifa ya habari sijui iliishia wapi. inasikitisha,inanifanya niwaze 30, 40 yrs to come nitakuwa wapi!
Hao wote nilio wataja hapo juu, wameshafariki zamani, akiwemo Mzee Mwinamila. Kumbuka kuwa Mzee Moris alikuwa ni kipofu, na alikuwa ana uwezo wa kupiga ngoma mpaka kumi na sita.



Mzee Moris Nyunyusa
 
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na vipindi vya michezo ya kwenye radio, kama vile, Mahoka (Na kicheko chake, mama mbavu zangu x2 eh eh eh eh eheeeeeeeeeeeeeeeeeH AAAH) na Pwagu na Pwaguzi...!

Kuna mchezo mmoja wa Pwagu na Pwaguzi, walianzisha mradi wa zahanati ya kung’oa meno huku wakiwa hawana mafunzo yoyote ya udaktari wa meno, nje ya ofisi yao waliweka bango kubwa likionesha kuwa wao ni wataalamu wa kung’oa meno.

Mteja akifika anapokewa mapokezi na mwenzake Pwaguzi, baada ya kulipia pesa ya matibabu anakwenda chumbani aliko Pwagu na kuanza kung’olewa meno kwa kutumia koleo za mafundi baiskeli, Ah ah ah ah.

Issue inakuja kwenye kuulizia fedha ambazo mteja alitoa, Pwaguzi siku zote alikuwa anamdhurumu mwenzake, uwa anadai kuwa zilishapotea katika purukushani za kukimbia...!

Nakumbuka kuna mradi mwingine, walikuwa wanakusanya damu za mbuzi, na kuzipeleka Hospitali, eti wanadai wanatoa msaada kwenye benki ya damu, ah ah ah ah. Hawa jamaa walikuwa mwisho.

Nawakumbuka magwiji wa michezo ya kuigiza yaani maselebu wa ukweli, kama Marehemu Mzee Hamis Tajiri (Janja au Meneja Mikupuo), Marehemu Bi Tunu Mrisho (Mama Haambiliki), Mwanaheri Ng’andu, Justin Kilumbi, Ali Manjunju (Ngosha), Marehemu Mzee Batholomeo Milulu (Masawe) na Marehemu Mzee Ibrahim Raha (Mzee Jongo) Mzee Fundi Said (Kipara) na wenginewe nimewasahau.
 
kweli mtu kama power mabula-those days alihit sana-kama kuna mwenye picha yake japo atuwekee hapa tumuone tena
nakumbuka kulikuwa na nyimbo zake kama............mabula yeeee.....nyie MNAJIBU ...yeeeee......*4-

Alikuwa akifika shuleni-hiyo siku vipindi vyote vinakufa-hakuna kinachofanyika tena.....ni kuchek shoo tu
 
Nilishasickia jina la power mabula wa2 wakili2mia but ckuwa najua huyu m2 alikuwa akifanya nini mpaka akaitwa power mabula!!!
 
nikweli pawa mabula alikuwa akifanya maonesho yake ya kutumia maguvu..!! na baadaye alistaafu na kisha akaokoka na sasa anihubiri injili yake MUNGU.

Kwa mara ya mwisho nimemshuhudia akihubiri vijijini sehemu za magu..!!

na kwa asili mimi nafahamu kuwa yeye ni musukuma...!!
 
Duh...zamani.

Mimi nilimuona mara moja miaka ya 83/84 hivi. Ni kweli alikuwa na nguvu za ajabu. Nakumbuka alikuwa na maonesho mengi tu ya kudhihirisha nguvu zake ambayo kwa hakika sio rahisi kuyasahau:

1. Wanafunga kamba ya katani nyuma pikipiki halafu anauma kwa meno hiyo kamba na kuzuia pikipiki isiende mbele
2. Analala chini (chali) wanamwekea ubao across kifuani halafu gari inapitisha tairi kufuata huo ubao (i.e. anakanyagwa na gari)
3. Anafanya 'tag of war' kwa kutumia mkono mmoja na wanaume 'walioshiba' kama ishirini hivi na kuwashinda!

Sijafanikiwa mpaka leo kujua ni ujanja gani walikuwa wanatumia. Miaka hiyo kulikuwa pia na 'maprofesa' kibao tu wa mazingaombwe, mmoja wao Prof Singira. Cha ajabu watu wa namna yao hawasikiki sana siku hizi...sijui kwa nini! Sijui walikuwa wanatumia ujanja gani kufanya yote hayo...nilitamani ningejua siku moja. Mara kadhaa huwa napata hisia baadhi ya madhehebu si ajabu wakawa wanatumia maujanja hayo hayo kujikusanyia waumini na baadae pesa (ni hisia tu!).

Kweli kila zama na kitabu chake!
 
Back
Top Bottom