Power mabula, moris nyunyusa na mwinamila ....tz imewaenzi vipi ?

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
49
Wanajamvi sijui km nimetua ukumbi husika, km sio mtanisahihisha.

Napenda kujua hawa ndg zetu waliwahi kuvuma sana enzi zao katika sanaa.

Power Mabula alikuwa na nguvu za ajabu kuuia au kuvuta magari km Scania n.k au hata gari kupita kifuani kwake bila kudhurika.

Mzee Moris Nyunyusa hadi leo ngoma zake zinapigwa kabla ya taarifa ya habari ya TBC, ile midundo aliipiga yeye. Mzee Moris aliwahi kuonyesha maajabu ya kupiga ngoma kumi kule Japan hadi Mbaraka Mwinshehe akamtungia wimbo ule wa "Maonyesho japani yalifana sana,.....

Mzee Mwinamila pia alikuwa msanii maarufu sana enzi hizo za TANU na wanasiasa wengi walimtumia katika kuburudisha jamiii.Mzee huyu alikuwa na uwezo wa kupiga samasoti kama kijana kabisa.

sasa nauliza kwa wale wanaojua hawa wazee TZ imewaenzi vipi au taha familia zao tu, au ndio mtu akitoweka ndio anasahaulika kabisa?

kwangu mie, naona hawa walikuwa ni ma-celebrities wa ukweli hapa bongo.

nawasilisha km nimekosea sehemu mnisahihishe sio kunishambulia.

wasaalaaam.
 
Hujakosea kaka! Hawa ni macelebrity wa ukweli kabisa, wengine wa sasa wanatafuta kwa nguvu lkn hao walifahamika kutokana na kazi zao za maajabu
 
lakini huyu ndugu Power Mabula yuko wapi? wazee wengine walikwisha tangulia mbele ya haki je huyu jamaa yuko wapi? kuna yeyote anaye weza eleza alipo na anafanya nini?
 
Hawa jamaa walikula sana pesa zetu enzi nikiwa shule ya msingi. Leo hii nimeshtukia kwamba wale jamaa walikuwa matapeli tu ndio maana ile profession imeingia mitini.
 
lakini huyu ndugu Power Mabula yuko wapi? wazee wengine walikwisha tangulia mbele ya haki je huyu jamaa yuko wapi? kuna yeyote anaye weza eleza alipo na anafanya nini?

Niliwahi Kumuona kwenye magazeti kama sikosei ni mwaka jana au juzi siku hizi ni mchungaji kwenye kanisa moja pale iringa mjini na alikua kilalamika kutupwa na serikali na wananchi ....
 
Huyo mchungaji wa Iringa nadhani ni Power Mwasekaga; Power Mabula ni mchungaji kanisa moja liko Tanga
 
Walikuwa wana mazingaobwa...wacha wapoteeee...wale hawakujua hata wanafanya nini..labda leo wakiona mieleka wanawazakuwa wangekuwa uko.
 
Wanajamvi sijui km nimetua ukumbi husika, km sio mtanisahihisha.

Napenda kujua hawa ndg zetu waliwahi kuvuma sana enzi zao katika sanaa.

Power Mabula alikuwa na nguvu za ajabu kuuia au kuvuta magari km Scania n.k au hata gari kupita kifuani kwake bila kudhurika.

Mzee Moris Nyunyusa hadi leo ngoma zake zinapigwa kabla ya taarifa ya habari ya TBC, ile midundo aliipiga yeye. Mzee Moris aliwahi kuonyesha maajabu ya kupiga ngoma kumi kule Japan hadi Mbaraka Mwinshehe akamtungia wimbo ule wa "Maonyesho japani yalifana sana,.....

Mzee Mwinamila pia alikuwa msanii maarufu sana enzi hizo za TANU na wanasiasa wengi walimtumia katika kuburudisha jamiii.Mzee huyu alikuwa na uwezo wa kupiga samasoti kama kijana kabisa.

sasa nauliza kwa wale wanaojua hawa wazee TZ imewaenzi vipi au taha familia zao tu, au ndio mtu akitoweka ndio anasahaulika kabisa?

kwangu mie, naona hawa walikuwa ni ma-celebrities wa ukweli hapa bongo.

nawasilisha km nimekosea sehemu mnisahihishe sio kunishambulia.

wasaalaaam.
Mzee Morris Nyunyusa; Historia itamkumbuka

Jr
 
Back
Top Bottom