Ndahani
Platinum Member
- Jun 3, 2008
- 18,119
- 9,049
Ndahani,
Wakati mwingine uvivu wa watanzania na mazingira ya kazi. Chukua kima cha chini ambacho analipwa mfanyakazi wa serikali. Siwezi kumlaumu mfanyakazi yoyote anayepokea kima hiki kufanya kazi kwa uvivu. Je katika sekta ya umma wapo watu wangapi wenye kupokea mishahara hii? Wengi.
Zakumi,
Always it is a situation of what started between chicken and egg. Naamini serikali imejaza watu wengi....na asilimia kubwa ya waliomo ndani yake sijui wana uwezo na elimu ya kiasi gani! Kama wameelimika vema na wanakubaliana na hali hiyo, kwanini serikali ione haja ya kubadili hali ya mambo? Tukumbuke most of the good things in life come with a price...we earn them by our sweat and not favors. Mindset zetu leo ni kuwa twende serikalini tupokee mishahara midogo ila tupige deal kubwa kubwa!
Wanaochangia hali hiyo ni sisi wenyewe...kama leo atakuja kiongozi ambaye ataamua kupunguza ajira za maelfu ya watu wanaoenda ofisini bila kufanya kazi yoyote na ku modernize mambo mengi ili yaweze kufanywa na watu wachache wenye uwezo, efficiency itaongezeka.
Tujiulize kwanini wawekezaji wanaangalia sana structure za kampuni zao na wako radhi waajiri wasomi wachache na kuwalipa hela nyingi ila wanahakikisha wanawavuna kwa asilimia 100??