Nisingetofautiana sana na William lakini nina ya kuongezea:
1) Hofu ya nini CHADEMA inasimamia: Pamoja na kuwa na ilani nzuri yenye mvuto, CHADEMA walipata shida sana kuielezea na kuwaaminisha wapiga kura ingetelezeka. Sio kwa kuwa hawakuwa na maelezo bali kwa sababu CCM kwa kutumia mtandao wake waliibeza kwa hisia kali na kuichafua. Mifano ni mingi! Hii ilihusu hasa mapendekezo ya sera kuhusiana na ujenzi wa nyumba kwa bei nafuu, elimu bure na sera za majimbo. Hata wasomi pale UDSM walisikika wakikituhuma kwa nguvu kabisa CHADEMA wanatafuata cheap popularity, na ni chama cha wachagga! Ndio walisema Slaa ni Mchagga na mwanzoni sikuona hii kama issue kubwa lakini kuna hisia kwamba Mchagga akichukua uongozi wa taifa basi taifa litakuwa limeisha au vile, lakin kweli kuna hofu! Na hawa wasomi (niwaite uchwara) wanakazia hoja yao kwamba haitowezekana kamwe mtu wa kabila la kichagga au kihaya akawa Raisi. Angalizo hapa ni SIASA TAKA ZA UKABILA na hofu iliyopandikizwa na wale ambao ni wapinzani wa Chadema.
2) Sio bahati mbaya kwamba CUF na CCM ilipata kukubalika zaidi maeneo ya Pwani, miji katika reli ya kati na kule kusini kwa mchomba(lindi na Mtwara). SIASA TAKA ZA UDINI zilitawala. CHADEMA walishindwa kabisa kusafisha madongo yalitupwa kwake kwamba mgombea wake ni Mdini na alikuwa ametumwa na Dini yake kugombea.
Ili Chadema wafanikie kuna kila sababu ya kutafuta jinsi ya kufuta hizi hisia ndani ya wapiga kura, pengine ni kuelekeza operesheni kama Sangara maeneo haya zaidi. Hilo la ukabila linazidi kupotea kwa kadiri CHADEMA wanalyozidi kupata wabunge na viongozi kutoka sehemu mbalimbali nchini. Kazi ya kupigana na CCM yenye mizizi na fedha nyingi, uchoyo wa madaraka na isiyo na haya kudanganya haikuwa rahisi hata kidogo. Ukifikiri ingekuwa rahisi kwa mpiga kura kuamini ahadi za CHADEMA kuliko kumwamini Kikwete na ahadi za Viwanja vya ndege, bandari, kujenga mto wa maji, reli nk. Lakini mashine ya propoganda za CCM ni kubwa!