Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY (NCAA)
JOB OPPORTUNITY
1.CONSERVATOR OF NGORONGORO
Salary and Remunaration:
SG 17 (NCAA Salary Grade), i.e. TZS 4,285,000/= X 121,000/= 4,500,000/= per month.
Halafu mnataka WABUNGE wabaki hivohivo?
 
sitaki hata ku-comment chochote naweza kuishia kutukana niopate dhambi buree
 
Huko mbali sasa, hapa ofisini kuna baadhi ya watu wanalipwa hadi dollar 10,000 kwa mwezi na bado nyumba wanalipiwa, usafiri wanalipiwa na watoto wanasomeshewa, huwa natamani hata kulia sasa hao wanataka tena waongezewe hayo mapesa, mmmh sijui tutaishia wapi huko, si tutakuwa tunawazalishia wachache tu???
NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY (NCAA)
JOB OPPORTUNITY
1.CONSERVATOR OF NGORONGORO
Salary and Remunaration:
SG 17 (NCAA Salary Grade), i.e. TZS 4,285,000/= X 121,000/= 4,500,000/= per month.
Halafu mnataka WABUNGE wabaki hivohivo?
 
Huko mbali sasa, hapa ofisini kuna baadhi ya watu wanalipwa hadi dollar 10,000 kwa mwezi na bado nyumba wanalipiwa, usafiri wanalipiwa na watoto wanasomeshewa, huwa natamani hata kulia sasa hao wanataka tena waongezewe hayo mapesa, mmmh sijui tutaishia wapi huko, si tutakuwa tunawazalishia wachache tu???

Ofisi ya Serikali?
 
HII NI HATARI.....KATIBA IJAYO IELEZA NAMNA WABUNGE WATAKAVYOLIPWA MISHAHARA NA POSHO , C KUJIPANGIA KAMA WANAVYOFANYA SASA'''':lol::lol:

Katiba haitakuwa for you,it will be for them.Watatumia kila ushenzi kuhakikisha hilo linafanikiwa.
 
Angalau wangikuwa wapo serious na kufanya utafiti wakina wa hoja zao kama Mnyika, kweli angalau tungewafikiria, lakini... kuuchapa usingizi... akimka naunga mkono asilimia mia... ndiooo. Jioni wapo kwenye tafrija na weekend ama Dar au semina za ukimwi na mifuko ya fedha, au matamasha kwa jiingizia posho zaidi! Majimbo hata hatuwaoni... nadhani hata kaposho kidoko tu hawaistili... Katiba mpya itapaswa kuwafanya wakae majimbo!
 
Wapandishe posho na huku kwingine ili na sisi tufaidi matunda ya uhuru kwa sababu kama ni kazi sote tunafanya
Huko kungine ni jitihada zenu tu. Wizara ya Nishati na Madini ni serikali kwa 100%. Umeona maposho ya kufa mtu yanavyolipwa kule? Turudishe SCOPO. Watu wanahomola kikatili sana kwenye taasisi za UMMA.
 
Huko mbali sasa, hapa ofisini kuna baadhi ya watu wanalipwa hadi dollar 10,000 kwa mwezi na bado nyumba wanalipiwa, usafiri wanalipiwa na watoto wanasomeshewa, huwa natamani hata kulia sasa hao wanataka tena waongezewe hayo mapesa, mmmh sijui tutaishia wapi huko, si tutakuwa tunawazalishia wachache tu???
Waandishi wa habari waende mbali zaidi ya Wabunge. Waende EWURA, TPDC, TPA, SUMATRA, DAWASA, DAWASCO( pamoja na kuwa Dar haina maji), TANESCO( pamoja na umeme wa kugawana), TCRA,....
Watuulizie mishahara ya vigogo wa taasisi hizi za UMMA pamoja na posho za bodi za wakurugenzi. Huenda Wabunge tunawaonea tu.
 
Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi

by zittokabwe Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.

Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.

Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.

Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho.

Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?

Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.

Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.

Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.
 
Monday, 28 November 2011 08:24
Kikao cha Bunge kikiendelea mjini Dodoma
bungeletu.jpg

ZAPANDA KUTOKA SH70,000 HADI 200,000, NI ZAIDI YA ASILIMIA 150

Fredy Azzah

HUKU mjadala wa kufutwa au kwa posho za wabunge na watumishi wengine wa Serikali ukiwa umefifia, posho za vikao (sitting allowance) za wabunge zimepanda kutoka Sh70,000 kwa siku hadi Sh200,000, imefahamika.
"Zimeongezeka kutoka Sh70,000 mpaka 200,000, wameanza kulipwa Bunge lililopita hili ni ongezeko la karibu mara tatu, yaani asilimia 154," kilieleza chanzo chetu kutoka ndani ya Ofisi za Bunge.

Kutoka na ongezeko hilo, kwa sasa kila mbunge atakuwa akilipwa Sh80,000 ikiwa ni posho ya kujikimu (perdiem) anapokuwa nje jimbo lake, posho ya vikao (sitting allowance) Sh200,000 na mafuta ya gari Sh50,000 kila siku, ambazo jumla yake ni Sh330,000 kwa siku.

Kutokana na ongezeko hilo, Bajeti ya Bunge kwa ajili ya posho za vikao vya wabunge imepanda na kufikia Sh28 bilioni kwa mwaka.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa sababu siyo msemaji wa wabunge, bali Ofisi ya Bunge.

"Ni nani kawapa hizo taarifa bwana, au ni vyanzo vyenu vya habari?" alihoji Dk Kashililah.

Baada ya kuelezwa kuwa taarifa hizo zimetoka kwenye vyanzo vyetu vya kuaminika alisema "Hao wana utaratibu wao bwana, labda mtafute Spika ndiye msemaji wa Wabunge."

Juhudi za kumpata Spika, Anne Makinda kutoa ufafanuzi wa suala hili, hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita wakati wote bila kupokewa hata pale alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) hakujibu. Hata simu zote za Naibu wake, Job Ndugai hazikupatikana.

Hata hivyo, Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe alisema kuongezeka kwa posho hizo kunatokana na wabunge kuwa wanalipwa mishahara midogo kulingana na kazi wanayofanya.

Alisema endapo wawakilishi hao wa wananchi wangekuwa wanalipwa mishahara inayolingana na kazi wanayofanya, kusingekuwa na sababu ya kuongezeka kwa posho hizo.

"Ninachosema mimi, siyo wabunge peke yao, lakini watumishi wote wa umma wanalipwa mishahara midogo sana mimi binafsi sitegemei posho za Bunge, kabla ya kuingia bungeni nilikuwa nimefanya kazi kwa miaka 14 na nilikuwa napata mshahara mzuri tu," alisema Filikunjombe.

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa alisema amezisikia taarifa hizo za kuongezeka kwa posho lakini siyo kwa undani. Hata hivyo alisema hakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumza suala hilo.

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema walivyokuwa wakipinga posho hizo wakati zilivyokuwa Sh70,000 waandishi wa habari walichukua suala hilo kama ajenda ya Chadema, hivyo kupandishwa kwa posho hizo ni matokeo ya watu kuwapuuza walivyokuwa wakizipinga.

"Msimamo wetu sisi tulishautoa tangu wakati posho zikiwa Sh70,000 wakati sisi tukipinga hizi posho waandishi wa habari na Watanzania mlichukulia suala hili kama ajenda ya Chadema, sisi wenyewe tupo wachache bungeni, tulichotaka ni kuonyesha jinsi fedha za Watanzania zinavyotumika vibaya," alisema na kuongeza:

"Achilia mbali hizo 200,000 za wabunge kuna watu huko serikalini wanalipwa mpaka Sh400,000 au Sh1 milioni kwa siku nyie ulizeni."

Alipoulizwa kama amechukua posho hiyo ya Sh200,000 alisema hajafanya hivyo kwa sababu hazifuatilii.

"Sijui hata kama zimeanza kulipwa au la kwa sababu huwa sizifuatilii na haka kama suala la posho hilo zilijadiliwa wakati wa vikao vya mwanzo mimi sikuwepo kwa sababu tulikuwa kwenye kesi yetu Arusha na bungeni tulikuja mwishoni wakati wa Muswada wa Katiba," alisema Mbowe.

Ongezeko hili la posho za wabunge limekuja wakati Watanzania wakiendelea kuishi kwenye maisha magumu yanayochangiwa na mfumuko wa bei ambao mpaka mwisho mwa Oktoba ulikuwa umefikia asilimia 17.9.

Pia ongezeko hili limekuja wakati Watanzania wakiwa na matumaini ya posho hizi kupunguzwa baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutangaza bungeni kuwa Serikali imekubali pendekezo la kutafakari na kuziangalia upya posho mbalimbali wanazolipwa wabunge na watumishi wote umma.

Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali alisema kuwa hawezi kuzungumza chochote juu ya posho hizo kwa kuwa hajapata barua rasmi juu ya kupanda kwake.

"Sijapata barua yoyote, nikiuliza na kupata majibu kwa wahusika nitakuwa na uhakika na nitakupa maoni yangu na msimamo wangu vizuri kabisa, lakini kwa sasa siwezi kusema chochote," alisema Mkosamali.

Juni 7, mwaka huu Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Zitto Kabwe, aliwasilisha barua Ofisi ya Bunge akikataa posho akisema watumishi wa Serikali na wabunge, hawastahili kulipwa posho wanapohudhuria vikao rasmi vya uwajibikaji wao wa kawaida.

Zitto alisema posho hiyo haistahili kulipwa kwake, wabunge wengine wala watumishi wa umma kwa kuwa kuhudhuria vikao ni sehemu ya kazi zao.

Alisema kitendo cha Waziri Mkuu kueleza kuwa watatafakari na kuangalia upya na kwamba suala la posho ni sera ya taifa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, ni ishara ya kiongozi huyo wa juu kukubali wazo la Chadema na safari ya kufuta posho hizo.

Awali, mara baada ya Chadema kutangaza msimamo huo, Spika Makinda alipinga uamuzi wa kususia posho akisema suala hilo lipo kisheria na kwamba hakuna mtu ambaye anaweza kuamua kuliondoa.

Alisema wabunge wa Chadema wataendelea kulipwa posho za vikao kupitia akaunti zao za benki na watatakiwa kusaini fomu ya mahudhurio ya Bunge, vinginevyo watajiweka katika wakati mbaya.

Hata hivyo, akihitimisha hoja za wabunge katika hotuba yake ya makadirio ya matumizi ya ofisi yake na zilizo chini yake juzi, Pinda alisema suala la posho lipo kwenye mchakato wa kuangaliwa upya.
 
Here u can clearly see how human being we are full of psychological biases, we want to see things in way that please us and not in reality.

Hii mada kwa kuwa cdm nao wamelamba posho utaona washabiki wa cdm wanajaribu kuikwepa, wengine wanasingizia eti ccm ndo wamepitisha.
Mbowe alidanganyia shangingi kuwa atarudisha kumbe wapi bana.

Zitto ur right, iko siku watu watauona unafiki huu wa hali ya juu.
 
Bunge limepokea na kutafakari kwa kina michango ya mawazo ya John Nangale Shibuda maswa-chadema na Joseph Selasini-rombo chadema na kuamua kupandisha kiwango hicho cha posho ili kukidhi maisha ya sasa ya mtanzania wa hadhi ya ubunge..........binafsi sikubaliani na ongezeko hilo kwani ni kiwango kikubwa mno kwa hali halisi ya uchumi wa nchi yetu kwa sasa.
 
Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi

by zittokabwe Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.

Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.

Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.

Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho.

Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?

Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.

Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.

Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.

ndio maana wakina kafumu wameacha mishahara ya 5m wakakimbilia ubunge knye maposho ya kufa mtu, hawa dawa yao ni ndogo sana watanzania wenzangu tutafute kombeo na manati tujifunze kulenga(shabaha) ukiona mbunge au gari ya mbunge inapita ni kulenga tu..........................
 
Here u can clearly see how human being we are full of psychological biases, we want to see things in way that please us and not in reality.

Hii mada kwa kuwa cdm nao wamelamba posho utaona washabiki wa cdm wanajaribu kuikwepa, wengine wanasingizia eti ccm ndo wamepitisha.
Mbowe alidanganyia shangingi kuwa atarudisha kumbe wapi bana.

Zitto ur right, iko siku watu watauona unafiki huu wa hali ya juu.
Hii issue ya posho sasa ni mtaji wa kisiasa kwa ccm wameongeza ili wapate pa kuwasema wapinzani kama wewe si mgeni wa siasa za bongo nafikiri utakumbuka ruzuku za vyama vya siasa zinavyoleta mitafaruku kwenye vyama hivyo. Sasa hivi ccm inajaribu kila mbinu kuinyamazisha pipoz na hapa kwenye posho wanatekeleza hilo nafikiri utayakumbuka yaliyoipata nccr mageuzi miaka ile.
 
Hii kweli ndiyo bongo! Je hizi hela zilipiotishwa kwenye bajeti au? Mbona wafanyakazi kuwaongezea sh 10,000/= tu inakuwa shida?
 
Wizi mtupu huu!! Nadhani tulifute Bunge, kwanza halina tija yeyote zaidi ya kufuja fedha zetu...
Tumepata tulicholipia! Si mliwachagua wenyewe sasa mwalalama nini?
Anyway...na zile nyumba walizokuwa wanajengewa zimefikia wapi?
UBUNGE NI BONGE LA DILI!
 
kilo 1 ya mahindi leo songea ni sh 200 jee nilime au niende kwenye ubunge ambapo kila siku nitavuna gunia 10 sawa na posho 200 000 za kusinzia kikaoni?Mnadanganya wananchi walime halafu nyie mnakula jasho lao lote inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom